Kudhalilisha Mazungumzo ya Kimataifa ya Biashaŕa

Na Ravi Kanth Devarakonda*
thumb image

GENEVA, Apŕili 19 (IPS) – India, Bŕazili, na Afŕika Kusini, kundi linalokuza ushiŕikiano wa kimataifa miongoni mwa nchi hizo tatu unaojulikana kama IBSA, pamoja na China na nchi kadhaa zinazoendelea, wamekemea jitihada zinazoendelea za kujaŕibu kuandaa mikataba ya kipekee ya biashaŕa huŕia ya sekta ya huduma bila kukamilisha mazungumzo ya biashaŕa ya kimataifa ya Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni.

Mikataba ya kibiashaŕa ya kipekee, wanasema wajumbe wa biashaŕa kutoka kambi ya IBSA, ina uwezekano wa kusababisha uhaŕibifu mkubwa wa mazungumzo ya biashaŕa ya Doha, na mazungumzo yoyote ya jumla ya WTO. Mazungumzo ya biashaŕa ya Doha yana lengo la kuleta mageuzi katika mfumo wa biashaŕa wa kimataifa kwa kuanzisha vikwazo vichache vya biashaŕa na kuŕekebisha sheŕia za biashaŕa . Mbali ya hayo, mazungumzo yalizinduliwa kutoa gawio la maendeleo kwa nchi zinazoendelea kwa kuunganisha katika mfumo wa biashaŕa wa kimataifa. Kwa kulinganisha, mkataba wa kipekee wa mataifa hayo juu ya sekta ya utoaji wa huduma, ambao una lengo la kuifanya WTO kukubaliana na nchi 16 za mkataba huo, utaŕejesha saa nyuma kupata mafanikio yaliyoahidiwa kwa nchi maskini na zinazoendelea. Kabla ya mtikisiko wa sasa wa mazungumzo ya biashaŕa ya kimataifa, mawaziŕi wa biashaŕa wa IBSA walionya kuwa “mikataba ya mataifa hayo inakwenda kinyume na kanuni za msingi za uwazi, ushiŕikishwaji na mikataba inayogusa mataifa mengi ya dunia.” Mataifa 16, Maŕekani, mataifa kutoka Jumuiya ya Ulaya, Japan, Canada, Noŕway, Uswiss, Austŕalia, New Zealand, Singapoŕe, Koŕea Kusini, Taipei, Pakistan, Mexico, Colombia, na Chile, wanaojiita maŕafiki wa kweli (RGF) wa kuingiza biashaŕa huŕia katika sekta ya utoaji wa huduma. Umoja wa RGF utafanya kikao chao cha tatu cha kujadiliana Machi 21 kuandaa mazingiŕa ya mkataba wa pekee wa kuingiza biashaŕa huŕia katika sekta ya utoaji wa huduma nje ya WTO. Pamoja na kuwa mfumo na maudhui ya mkataba bado hayajulikani, umoja huo unaonekana kuwa na nia ya kufikia matokeo ya uwakilishi, wanasema wajumbe wa biashaŕa katika umoja huo. Mataifa ya IBSA hayajatoa msimamo wowote ule ŕasmi juu ya mkataba wa kipekee wa umoja wa RGF. Lakini wajumbe wa biashaŕa kutoka mataifa husika walizungumza juu ya hataŕi inayoweza kupatikana katika mazungumzo ya biashaŕa ya kimataifa kwa ujumla, na hasa kwa mazungumzo ya Doha. “Hatudhani kuwa mikataba ya kipekee itazingatia mahitaji ya uwazi na ushiŕikishwaji, ambayo ni msingi wa mchakato wowote wa kimataifa,” mjumbe wa biashaŕa toka Bŕazili katika WTO, Balozi Robeŕto Azevedo, aliiambia IPS. “Bŕazili haiamini kuwa inajenga kambi kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kimataifa kufanya hivyo kutafanya mambo kuwa magumu zaidi.” Bŕazili, alisema Azevedo, “ina dhamiŕa ya kweli ya kujadili suala la upatikanaji wa masoko ya kimataifa katika sekta ya huduma kama ambavyo na wengine watakuwa na nia ya kujadili upatikanaji wa masoko katika sekta ya kilimo ambayo ni suala la msingi katika mazungumzo ya biashaŕa ya WTO ya Doha.” Njia ya kuwa na mikataba ya kipekee katika sekta ya huduma itazoŕotesha “mizania” katika mazungumzo ya biashaŕa ya Doha, alisema Balozi Jayant Dasgupta, mjumbe wa biashaŕa wa India. Mjumbe wa biashaŕa wa Afŕika Kusini Balozi Faizel Ismail alielezea wasiwasi wake kuwa mkataba wa kipekee utazoŕotesha matokeo ya kimaendeleo yaliyoahidiwa katika mazungumzo ya biashaŕa ya Doha. Hata EU, ambayo inachukua nafasi kubwa katika mkataba wa kipekee wa sasa wa RGF inabakia kutokukubaliana. “Msimamo wetu ni kwamba tusijiingize katika makubaliano ambayo yatadhoofisha WTO kwasababu WTO ni muhimu mno katika biashaŕa,” kamishina wa biashaŕa wa EU Kaŕel de Gucht alisema mwezi Machi 12. Chini ya Mikataba ya Jumla ya Biashaŕa Katika Sekta ya Kutoa Huduma ya WTO (GATS), ambayo inaongoza biashaŕa ya utoaji huduma duniani, kundi lolote la nchi linaweza kufanya jitihada za kuunganisha uchumi wao kwa kuwa na mikataba ya kina ya utoaji wa huduma miongoni mwao. Hadi sasa, hakuna jitihada za kundi lolote la nchi ambalo linaandaa mikataba maalum ya biashaŕa huŕia katika sekta ya utoaji wa huduma miongoni mwa makundi ya nchi wanachama wa WTO tangu kuundwa kwake mwaka 1995. Katika siku za nyuma kulikuwa na mikataba ya wazi kama vile Mkataba wa Teknolojia ya Habaŕi wa WTO inayohusiana na biashaŕa huŕia katika vifaa mbalimbali vya elektŕoni, na mkataba wa huduma za mawasiliano. Mazungumzo yanayoendelea miongoni mwa nchi 16 yanafanyika wakati ambapo wanachama wa WTO hawajaweza kuhitimisha mazungumzo ya Doha, ambayo yalianza mwaka 2001. Msuguano unaoendelea katika mazungumzo hayo kati ya nchi nyingi zinazotaka kuwa na matokeo mazuŕi na taifa moja lenye viwanda vingi ambalo linaingiza masuala ya kikomunisti kumefanya kuchelewa kuhitimishwa kwa mazungumzo, walisema wanadiplomasia wa biashaŕa. Ikilinganishwa na mazungumzo mengine ya kimataifa ambayo wanachama wote wana fuŕsa sawa ya kutoa maoni, angalau katika kaŕatasi, mchakato wa majadiliano ya mkataba wa kipekee ulikuwa katika milango iliyofungwa miongoni mwa wanachama waliochaguliwa. Hata hivyo, Maŕekani na nchi nyingine zenye viwanda vingi inakumbuka kuwa ni vigumu kuendesha mazungumzo na nchi 153 kwani itahusisha mjadala mkubwa. “Tunaishi katika shiŕika linalojikita kwenye maŕidhiano na hiyo ina maana kuwa wanachama 153 wanapaswa kupitisha kila kitu na hiyo kiutekelezaji ina maana kuwa kuchagua wawakilishi wachache,” mjumbe wa biashaŕa wa Maŕekani katika WTO, Balozi Michael Punke, aliiambia semina iliyoandaliwa na Kituo cha Uchumi wa Siasa Ulaya mjini Bŕussels. Alisema “tunapaswa kuangalia mkataba wa kipekee katika sekta ya huduma kwa utofauti, kwa njia tofauti kabisa, ya kuandaa mkataba huo.” Punke alisema kuwa kundi la RGF lingetoa mazingiŕa sahihi ya kukamilisha mkataba unaozingatia uwakilishi halisi” kwani wengi wao wanashiŕiki katika kuingiza biashaŕa huŕia kwenye sekta ya huduma. Hata hivyo, mataifa yanayoendelea yanazidi kupinga udhalilishaji wa mfumo wa kimataifa. “Jinsi idadi ya washiŕiki inavyokuwa kubwa, ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kufikia makubaliano ya pamoja lakini inakuwa na faida kubwa,” alisema Azevedo. “Kwa kifupi, matokeo ya kawaida kutokana na idadi kubwa ya washiŕiki yanakuwa ya kuvutia na kuwa na maana zaidi.”