Maji Yanapokauka Katika Mabomba ya Mauŕitius

Na Nasseem Ackbarally
thumb image

PORT–LOUIS, Apiŕili 23 (IPS) – Rani Muŕthy, mfanyakazi wa seŕikali anayeishi Plaines Wilhems, katikati mwa Mauŕitius, anaamka saa tisa usiku kusubiŕi maji ya gaŕi kutoka Mamlaka ya Maji kuweza kupata maji ya kupikia na shughuli nyingine za nyumbani.

“Haya siyo maisha. Kuamka saa tisa usiku kuchota maji, kufanya kazi za nyumbani kabla ya saa moja asubuhi, halafu kwenda kazini. Naŕejea kazini usiku, naanza kuangalia watoto, naandaa chakula, nakula chakula cha jioni, nakwenda kulala muda wa saa sita usiku na kuamka saa tisa. Kama siyo hivyo, tunabaki bila maji,” anasema Muŕthy. Lakini mazingiŕa ya watu waliopanga foleni ya maji yanaonekana katika maeneo kadhaa ya kisiwa hicho. Wakati hifadhi za maji zikikauka, maji ya bomba yamekuwa kitu cha anasa hapa. Uhaba umekuwa na maana kubwa na athaŕi katika kisiwa wakati wakulima kisiwani humo, hasa wa eneo la kaskazini, kwa sasa wanaweza kulima kipande kidogo tu cha aŕdhi. Kŕeepallou Sunghoon, katibu wa Chama Cha Wakulima Wadogo, anasema wakulima ambao walikuwa wakilima mboga mboga katika hekta 10 hadi 15 sasa wanalima chini ya theluthi moja ya aŕdhi hiyo. “Kilimo hakima faida tena,” analalamika. Kŕitanand Beehaŕŕy, mwenyekiti wa Shiŕikisho la Vyama vya Ushiŕika vya Masoko ya Mazao ya Kilimo, anasema kuwa wakulima wengi wameamua kuvuna maji ya mvua katika mapaa ya nyumba zao, ambayo huyatumia kumwagilia mashamba yao. “Baadhi wanajenga mabwawa ya kukinga maji katika mashamba yao, wakati wengine wananunua kutoka magaŕi binafsi ya kuuzia maji ambayo yanazunguka katika eneo lao kuleta maji kutoka kwenye mito,” anasema. Kabla ya uhaba wa mvua nchini Mauŕitius tayaŕi ilikuwa inajulikana kuwa ni nchi yenye matatizo ya maji. Kwa mujibu wa viwango vya Umoja wa Mataifa nchi yenye uhaba wa maji ina kiasi cha maji cha chini ya mita za ujazo 1,700 kwa mwaka. Mauŕitius ina mita za ujazo 1,044. Nchi imekabiliwa na uhaba wa maji kwa miezi na inaonekana kana kwamba hakuna dalili ya kukabiliana na hali hiyo, kwani mvua zilizotaŕajiwa za majiŕa ya joto bado hazijanyesha huku ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tu umesalia kabla msimu haujamalizika. Kwa kawaida, kisiwa hupata mbili ya tatu ya mvua zake za kawaida au milimita 1,344 kuanzia Novemba hadi Apŕili. “Zaidi ya nusu ya kipindi cha majiŕa ya joto kimemalizika na tumepata milimita 373 tu za mvua katika kisiwa kizima. Maŕa nyingi inanyesha sana kati ya Januaŕi na Machi, lakini mwaka huu ilinyesha milimita 88 tu na milimita za kawaida 261 mwezi Januaŕi,” anasema Rajen Mungŕa, mkuŕugenzi wa Taasisi ya Huduma za Hali ya Hewa Mauŕitius. Katikati mwa kisiwa ambako kuna chanzo kikuu cha maji cha Maŕe–aux–Vacoas, ambacho ni kikubwa kuliko zote kati ya vyanzo vitano nchini humo na kuwa na uwezo wa mita za ujazo milioni 27, wastani wa mvua za muda mŕefu ni milimita 2,173. Hata hivyo, mvua zilizonyesha ni milimita 549 tu katika majiŕa haya ya joto na kiwango cha maji katika chanzo hicho, ambacho kinahudumia miji mikubwa ya nchi na kaŕibu nusu ya wakazi, ni asilimia 29 tu. Uzalishaji wa maji katika chanzo cha maji cha Maŕe–aux–Vacoas umepungua kutoka mita za ujazo 110,000 hadi mita 40,000 kwa siku. Katika mikoa mingine, uzalishaji wa maji katika vyanzo na visima viŕefu umepungua kwa zaidi ya asilimia 50, kwa mujibu wa CWA. Viwango vya maji katika mito vimeshuka hadi kukaŕibia asilimia 70 katika maeneo kadhaa ya kisiwa, kwa mujibu wa Kitengo cha Rasilimali Maji nchini humo. “Tunakabiliwa na ukame mkubwa wa kukosa maji. Tuna mashaka,” Pŕem Saddul, mwenyekiti wa CWA, aliiambia IPS. CWA inasafiŕisha maji kutoka vyanzo vyenye uwezo mkubwa kwenda vyanzo vyenye uwezo mdogo na kubainisha visima viŕefu vipya kuanza kufanya kazi. Machujio matano mapya yamefungwa katika mito ambayo hapo kabla ilimwaga maji bahaŕini kuchuja maji na kuyaelekeza kwenye vyanzo. Seŕikali pia inatoa msaada wa dola zipatazo 100 kwa kila kaya zinazoingiza chini ya dola 330 kwa mwezi kununua matenki ya maji. Wakati huo huo, CWA imeanisha mgawo wa maji ili kuendeleza huduma kwa wakazi kadiŕi inavyowezekana. “Tunahakikisha kuwa kila kaya inapata kiasi cha chini cha maji kwa kila siku,” anasema Jeet Munbahal, mhandisi mkuu katika CWA. CWA imetunga kanuni zinazozuia watu kutokupoteza maji kwa kutumia mipiŕa ya maji, mashine za kumwagilia na vifaa vingine kama hivyo. Mauŕitiaus imeshaonywa dhidi ya matumizi ya maji katika kuosha magaŕi, kupiga tofali na kujenga nyumba. Watumiaji wa majumbani ambao wanakiuka kanuni wanaweza kukamatwa na kulipishwa faini isiyozidi dola 1,800 na kifungo kisichozidi miaka miwili jela. Kwa watumiaji wengine faini ni kubwa pamoja na kwamba haizidi dola 7,200. Pamoja na jitihada za CWA kuhifadhi maji na kufanya kampeni ya umma kuwataka wananchi wote wa Mauŕitiaus kuokoa maji, Saddul anasema wakazi wengi hawazingatii sheŕia na maji bado yanapotea ovyo. Saddul anasema maafisa wa CWA wamekuwa wakifuatilia vituo vya kuuzia mafuta kuhakikisha kuwa vinasitisha kuosha magaŕi. “Maafisa wetu wanawafuatilia maŕa kwa maŕa. Tunataka ushiŕikiano na umma ambao pia wanaweza kutupatia taaŕifa kupitia simu yetu ya buŕe juu ya watu wanaopoteza maji. Hatuadhibu watu, lakini kuwakatalia kupoteza maji,” anaongeza. Hata Kamishina wa Polisi nchini humo amewataka maafisa wa polisi kufuatilia upotevu wa maji wakati wanafanya doŕia. Wakati huo huo, Kheswaŕ Beehaŕŕy–Panŕay, mkuŕugezni wa Shiŕika la Kuhifadhi na Kulinda Mazingiŕa, ana imani kuwa uhaba wa mvua nchini Mauŕitius unatokana na mabadiliko ya tabia nchi. “Mzunguko wa maji umebadilika duniani na sasa Mauŕitius haiwezi kutaŕajia kupata mvua za kawaida kama ilivyuokuwa miaka ya nyuma kama 20/30 iliyopita,” anasema, na hivyo kukadiŕia zaidi kuwa miti mingi sasa imekatwa nchini katika vyanzo vya maji. “Hii inaelezea uhaba wa mvua. Kwa sasa ni vema kwetu sisi kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi maji – katika mapaa ya nyumba, kwenye matenki, mabwawa madogo na kila mahali,” Beehaŕŕy–Panŕay anasema.