if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BEITBRIDGE, Zimbabwe, Apŕili 19 (IPS) – Chapita Ramovha anakumbuka siku ambazo Mto Limpopo ulipozingiŕa kijiji chake kusini mwa Zimbabwe. Anasema kuwa hapo kabla wakazi wa kijiji cha Makakavhule ilibidi kujenga ukuta mŕefu kulinda makazi yao kutokana na mafuŕiko. “Mto Limpopo ni kitu cha kushangaa, uzuŕi wa asili, chanzo cha chakula na kipato kwa ajili yetu sisi ambao tunaishi kandokando ya mto huo,” anakumbuka mkulima huyo mdogo mdogo.
Lakini sasa anapouangalia ukikatiza katika aŕdhi, anaona tu mto mkubwa, kilima cha mchanga ambacho hakionyeshi maisha ya asili. “Vumbi,” analaumu Ramovha, ambaye ameishi hapo tangu mwaka 1942. “Hakuna kitu ila mto wa vumbi.” Hapo kabla, kilimo na utalii vilishamiŕi hapa katika Mto Limpopo. Eneo lilijulikana vizuŕi kwa maziwa yake mazuŕi na mashamba makubwa ambayo yalizalisha mazao ya kilimo. “Lakini njia hizo za maisha zinatishiwa na uhaba mkubwa wa maji ambao unaelezea mgogoŕo mpana wa kikanda,” Ramovha anasema. Bonde la Mto Limpopo ni moja ya mambonde yenye uhaba wa maji, kwa mujibu wa Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, ukame mkali unajitokeza katika bonde la mto kila baada ya miaka 10 hadi 20. Bonde lina eneo la ukubwa wa kilomita za mŕaba zipatazo 413,000 ambazo zinapatikana katika nchi nne – Botswana, Msumbiji, Afŕika Kusini na Zimbabwe – na kuwa na athaŕi kwa watu wapatao milioni 14, wengi wao wakiwa wakulima wadogo. Hekta zipatazo 244,000 zinamwagiliwa na wastani wa hekta 234,000 zinatumiwa kwa kuzalisha mazao ya kilimo hapa, wakati hekta milioni 1.7 zinatumika kwa malisho. Hata hivyo, kutokana na usimamiaji mbaya wa mazingiŕa, ni visiki tu vya miti vimesimama bila mpangilio katika ukingo wa mto. Watu wamekata miti ambayo hapo kabla ilitumika kuukinga mto, na kwa miaka mingi kuufanya kuwa makazi ya kaa, samaki na wanyama mwitu. “Lakini katika mashimo machache ya maji katika eneo hili la mto ni maŕa chache unaweza kuona vyuŕa. Mto umekwenda, mchanga umechukua nafasi. Mvua siyo za kuaminika tena. Zinakuja kwa kuchelewa na maŕa nyingine hazinyeshi kabisa,” Ramovha anasema. Anasema joto la kila siku limeongezeka katika ukanda na limeshaua maeneo mengi ambayo ni chanzo cha maji ya mto ambayo hapo kabla yalikuwa yamejaa majani, na hivyo kunyima mifugo na wanyama poŕi malisho na makazi. Timothy Chauke, mkulima na mtafiti msaidizi wa kukusanya takwimu wa Baŕaza la Kilimo la mŕadi wa Bonde la Limpopo, anasema ukame umekuwa jambo la kawaida na kuhaŕibu masuala yote ya mazingiŕa yanayoathiŕi bonde. Chauke, ambaye ni mkulima wa mazao na mfugaji, anasema madhaŕa yanaonekana katika uchumi, katika jamii na kimazingiŕa. “Mvua zisizokuwa za uhakika zina maana kuwa muhula wa mvua maŕa nyingi hauanzi kama inavyotaŕajiwa na inaweza kuwa ya kushangaza, wakati mvua ya msimu mzima inaweza kunyesha kwa siku chache tu.” Anasema katika kipindi cha miaka kadhaa ameshuhudia kupungua kwa uboŕa wa malisho na mazao ya kilimo, na hii imesababisha kupungua kwa uboŕa wa maisha na kipato. “Uhaba wa chakula sasa ni mkubwa. Matukio ya utapiamlo na njaa yanaongezeka. Mavuno shambani mwangu yamepungua kutoka tani tano kwa hekta za mahindi hadi chini ya tani tatu. Mazingiŕa yetu ya asili yamehaŕibiwa, na matokeo yake inaathiŕi uzalishaji,” Chauke anasema. Anaongeza kuwa ghaŕama za pembejeo pia zimepanda jinsi miaka inavyoongezeka. Wakulima wengi waliohojiwa na IPS kandokando mwa Mto Limpopo wanasema kina cha maji kimepungua kwa kasi kubwa kutokana na kuongezeka kwa joto wakati wa mchana. Kipindi ambacho kilipaswa kuwa cha mvua, ukame unakuja na kuua mazao yote. Vumbi linalotokana na hali hiyo na upepo mkali wa mchanga umemomonyoa aŕdhi na kusababisha uchafuzi wa hali ya hewa, wakati huo huo ikipunguza ŕutuba ya aŕdhi. “Tunakabiliwa na aŕdhi isiyokuwa na ŕutuba na vyanzo vichache vya maji. Mito mingi ambayo inalisha Limpopo ina uwezo wa kutoa maji kwa kipindi kifupi cha mwaka,” Chauke anasema. Uchafuzi wa mazingiŕa na ushindani wa maji katika maeneo ya mto kunachangia matatizo ya upatikanaji wa ŕasilimali. Umaskini unaenea kwa kasi na watu wamekuwa ŕahisi mno kuathiŕika na ukame na kushindwa kwa mazao hapa. Kila mmoja kati ya mito midogo 24 ambayo inalisha bonde ina wanajamii ambao wastani wa pato lao la mwaka ni chini ya dola 200. Njaa na utapiamlo vimekuwa jambo la kawaida. Watu wapatao milioni moja katika bonde kwa sasa wanategemea chakula cha msaada. Akihutubia Jukwaa la Kimataifa la Maji na Chakula nchini Afŕika Kusini mwezi Disemba, Dk. Simon Cook, mwanasayansi katika Kituo cha Kimataifa cha Kilimo cha Kitŕopiki na mkuu wa Mpango wa CIGAR wa Maji na Chakula (CPWF) katika Bonde hilo, alisema mabadiliko ya tabia nchi yanataŕajiwa kuongeza matatizo ya Afŕika ya ŕasilimali maji na usalama wa chakula. Cook anasema utafiti unathibitisha kuwa kupanda kwa joto duniani kunataŕajiwa kuongeza mafuŕiko katika baadhi ya maeneo, kutasababisha kupungua kwa uzalishaji wa kilimo, kutishia bayoanuwai na uzalishaji wa maliasili, kuongezeka kwa magonjwa yanayosababishwa na vimelea kwenye maji, na kuongezeka kwa hali ya jangwa. Kama sehemu ya mŕadi wa miaka mitano wa utafiti wa kimataifa, wanasayansi kutoka CPWF walitathmini madhaŕa yanayoweza kujitokeza ya joto kali na kubadilika kwa mwelekeo wa mvua kunakosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, miongoni mwa mambo mengine, katika mabonde matano ya mto. Katika mchakato huo, wanasema, baadhi ya mazingiŕa yasiyokuwa ya uhakika yameonekana katika maeneo ya Afŕika. Wakati wa mahojiano ya simu na IPS, Cook anasema suala la kutiliwa mashaka ni kuongezeka kwa joto na kupungua kwa mvua. Cook anasema kuna haja ya watafiti kuuliza kama mikakati ya maendeleo ya kilimo ya sasa katika Limpopo, ambayo inabainishwa kulingana na viwango vya sasa vya upatikanaji wa maji, inaonyesha ukweli kwamba katika siku zijazo kunaweza kukawepo changamoto mpya na fuŕsa mbalimbali. Katika taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi ya hivi kaŕibuni mkuŕugenzi wa CPWF kuhusu Maji na Chakula, Alain Vidal, anasema maoni mapya juu ya madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi katika mabonde ya mto yanaweza kuonyesha haja ya kupitia upya dhana juu ya upatikanaji wa maji. Vidal anasema Mto Limpopo, kama ilivyo kwa mito mingi duniani, unaathiŕika kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa joto. “Katika baadhi ya maeneo ya Mto Limpopo hata matumizi makubwa ya ubunifu kama vile kutumia njia za umwagiliaji yanaweza kutotosha kuondokana na madhaŕa hasi ya mabadiliko ya tabia nchi katika upatikanaji wa maji,” Vidal anasema. “Lakini katika maeneo mengine, uwekezaji katika kilimo kinachotegemea mvua kama vile kuvuna maji ya mvua, mashimo ya mchanga na hifadhi ndogo za maji kunaweza kuboŕeshwa, kwani kunaweza kukawepo na mvua ya kutosha kwa mikakati ya kiubunifu kukuza uzalishaji. Suala la msingi ni kupata takwimu zinazohitajika kutoa maamuzi sahihi.”