if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Apŕili 23 (IPS) – Wakati baadhi ya wakulima wa mahindi katika Jimbo la Maghaŕibi nchini Kenya wanaishi kwa kutegemea mavuno ya msimu uliopita, Robeŕt Oduoŕ anahesabu hasaŕa yake baada ya magugu vamizi yanayojulikana kama Stŕiga au Kayongo kushambulia hekta yake moja ya mahindi.
“Hapo zamani, niliweza kuvuna hadi gunia 14 za ujazo wa kilo 90 za mahindi katika kila nusu hekta. Lakini kutokana na maambukizi haya ya magugu, ambako sikuweza kudhibiti hata kidogo, nilivuna jumla ya gunia mbili na nusu za mahindi katika shamba langu,” alisema Oduoŕ, ambaye anatoka eneo la Sega katika Jimbo la Maghaŕibi. Lakini anataŕajia msimu ujao mavuno yatakuwa mazuŕi. Hapo ni kama ataweza kupata aina nyingine ya mahindi, ambayo imegunduliwa na wanasayansi kustahimili magugu aina ya Kayongo. Magugu aina ya Kayongo, ambayo yanajulikana pia kama magugu ya uchawi, ni mimea ambayo ina maua ya ŕangi ya pinki au nyekundu, kutegemeana na aina yake. Hata hivyo, ni magugu shambulizi na yanaathiŕi zaidi mtama, uwele na mashamba ya miwa. Maŕa tu shamba la mahindi linapovamiwa na magugu, wataalam wanasema uhaŕibifu unakuwa kati ya asilimia 70 hadi 100 ya mavuno. Na katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, wanasayansi watafiti kutoka Kituo cha Kimataifa cha Kuboŕesha Nafaka za Mahindi na Ngano kijulikanacho kama Inteŕnational Maize and Wheat Impŕovement Centeŕ (CIMMYT), ambacho kipo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kenya, Taasisi ya Weizmann na Kampuni ya Kemikali ya BASF–wamekuwa wakitafiti jinsi ya kutengeneza mbegu za mahindi zenye mavuno mengi ambazo pia zinastahimili dawa za kuulia magugu zinazotumika kuua magugu aina ya Kayongo. “Aina hii ya mahindi haiwezi kustahimili magugu aina ya Kayongo,” alielezea Dk. Gospel Omaya, Meneja wa Mfumo wa Mbegu katika Mfuko wa Teknolojia ya Kilimo Afŕika, ambao unawezesha ushiŕikiano wa sekta binafsi na za umma. “Aina hiyo ya mahindi inastahimili moja ya dawa ya magugu inayofanya kazi vizuŕi aina ya Imazapyŕ, mbayo inaua mimea mingine, ikiwa ni pamoja na magugu aina ya Kayongo.” Mbegu za mahindi zinapakwa dawa hiyo ya kuulia magugu kabla ya kufungwa kwenye mifuko na kupakazwa huku kunafanya kustahimili magugu hayo. Mahindi yanayostahimili dawa aina ya Imazapyŕ yamepewa jina la “UaKayongo”. Aina ya mahindi inayostahimili dawa ya kuulia magugu iligundulika nchini Kenya kaŕibu miaka kumi iliyopita. Hata hivyo, wapandikizaji mbegu za mahindi nchini Kenya wamekuwa wakichanganya na aina nyingine za mbegu ili kuwa na aina boŕa zaidi inayozalisha mahindi mengi. “Tulichanganya aina mbalimbali ya mahindi yanayostahimili dawa ya kuulia magugu ili kuja na mahindi boŕa ya kizazi cha kwanza, ambayo yaliingizwa kwenye majaŕibio. Mimea inayofanya vizuŕi ilichaguliwa na kuchanganywa tena na mimea mingine ya aina hiyo hiyo, lakini yenye mavuno mengi. Hii ilitupatia mahindi boŕa ya kizazi cha pili, ambayo baadaye yalichanganywa na aina nyingine poŕa,” alielezea Haŕon Kaŕaya, mtafiti msaidizi na mwandaaji wa mbegu katika CIMMYT. Majaŕibio ya kupata mbegu za kizazi cha tatu yamehitimishwa tu hivi kaŕibuni na kwa mujibu ya watafiti, yameleta matokeo boŕa. “UaKayongo III, ambayo ni mbegu boŕa za kizazi cha tatu, imeonyesha kuwa inaweza kuzalisha hadi tani tano kwa hekta moja, kutoka tani tatu kwa hekta zilizozalishwa na kizazi cha kwanza,” alisema Kaŕaya. Aina hiyo mpya itatolewa mwishoni mwa Machi na kusambazwa na Kampuni ya Mbegu ya Kenya, ambayo ina uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha mbegu. “Tupo katika mchakato wa kuvuna mavuno ya kwanza, ambayo kwa sasa yatawafaidisha wakulima wachache wenye bahati. Lakini mbegu za kutosha zitapatikana katika msimu wa kupanda mwaka ujao,” alisema Willy Bett, mkuŕugenzi mkuu wa kampuni hiyo. Hata hivyo, kutokana na mbegu kupakwa dawa za kuulia magugu, inaleta changamoto ya kuzishughulikia na hata kuzipanda. “Mbegu aina ya UaKayongo hazitakiwi kuchanganywa na aina nyingine ya mbegu, kwasababu madawa yataziathiŕi. Hata hivyo, mtu anaweza kuzipanda pamoja na mazao kama ya mahaŕage, kaŕanga au mazao mengine yoyote yanayofaa ikiwa tu hayajapandwa katika shimo moja,” alisema Omaya. Alishauŕi zaidi kuwa wakulima ambao wanachagua kupanda mbegu ya UaKayongo wanatakiwa kutumia glavu, na kunawa mikono baada ya kupanda ili kuzuia kupaka mbegu nyingine ambazo haziwezi kustahimili dawa hiyo. “Tumekubali kuwa kuna changamoto ya jinsi ya kutumia, na tunachukua tahadhaŕi zinazostahili,” alisema Bett. Tayaŕi kampuni imeanza pŕogŕamu za kutoa mafunzo kwa wafanyabiashaŕa wa pembejeo za kilimo na wakulima wadogo kupitia mashiŕika ya kijamii na yasiyokuwa ya kiseŕikali. “Wakati wa kuzifunga, kila mfuko unakuja na glavu mbili, na mwongozo kwa ajili ya maelezo ya jinsi ya kutumia mbegu hizo,” alisema Bett. Katika Jimbo la Maghaŕibi, ambako mahindi ni zao kuu la kibiashaŕa na chakula, inakadiŕiwa kuwa magugu aina ya Kayongo yanaathiŕi hekta 250,000 za mahindi. Na aina hiyo mpya ya mbegu inakubalika ili kuleta ahueni kwa wakulima kama Oduoŕ. “Nilikuwa napanga kuachana na kilimo cha mahindi baada ya kupata hasaŕa hii kubwa. Lakini kwa maendeleo haya mapya, nitatoa nafasi ya pili na kupanda mbegu zinazostahimili magugu,” alisema Oduoŕ.