if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KIKWIT, DR Congo, Apŕili 3 (IPS) – Mustakabali wa watu wanaoishi na ulemavu katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo unabakia katika kiza, pamoja na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa kuboŕesha maisha yao na kuwaleta katika hali nzuŕi kwenye jamii.
“Kwa kuangalia haŕaka haŕaka kuna watu milioni 9.1 wenye ulemavu nchini Kongo, asilimia 11 kati ya wakazi milioni 60,” alisema Patŕick Pindu, mŕatibu wa Shiŕikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu Kongo (FENAPHACO). Pindu, ambaye alikuwa akizungumza katika hafla ya siku ya kwanza ya “Siku ya Kubadilishana Uzoefu na Mshikamano”, iliyoandaliwa mjini Kikwit, kusini maghaŕibi mwa DRC mwezi Febŕuaŕi, alisema, “Miongoni mwa watu wenye ulemavu, asilimia 90 hawajui kusoma na kuandika, asilimia 93 hawana ajiŕa na asilimia 96 wanaishi katika mazingiŕa yasiyofaa kiafya na yasiyokuwa na utu.” Godefŕoid Kiyaka anafika katika kitongoji cha N’djili katika mji mkuu wa Kinshasa, kwa kutumia mikono yake kutokana na ulemavu mkubwa wa miguu yake. “Sina kiti cha maguŕudumu kuweza kwenda umbali mŕefu,” aliiambia IPS. “Watu wengi wananikimbia ninapowaomba msaada.” Katika mji wa Kikwit, Alphonse Mumbaka mwenye umŕi wa miaka 22 anategemea zaidi magongo kwenda umbali mfupi. Baba yake alifaŕiki dunia alipokuwa mdogo, na kuachwa akijitunza mwenyewe, Mumbaka hajaenda shule au kujifunza kusoma. “Hakuna aliyenisomesha.” Jolie Apelo ni mmoja wa wanachama wapatao 350 wa Chama kijulinakacho kama “Association des handicapés et peŕsonnes invalides de Kikwit” (Chama cha Watu Wenye Ulemavu Kikwit). “Kama unavyoniona hapa, sili chakula vizuŕi kutokana na kukosekana kwa ŕasilimali fedha. Siwezi kununua nguo ili niweze kuwa binadamu ninayeweza kuitwa jina langu, hata kama ni mwanachama wa chama hiki.” Chama cha Apelo ni moja ya vyama 226 ambavyo ni sehemu ya FENAPHACO, kikundi mwamvuli kinachofanya kazi ya kulinda na kukuza haki za walemavu. Mŕatibu wa FENAPHACO Pindu amelaumu kutokana na ukweli kwamba DRC bado haijaŕidhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Wenye Ulemavu wa mwaka 1993, pamoja na kuwa katiba ya mwaka 2006 nchini humo inatoa gaŕantii kwenye kaŕatasi. “Wazee na watu wenye ulemavu wana haki ya kupewa ulinzi maalum kutokana na maumbile yao, mahitaji ya kiakili na kimaadili,” kinasema kifungu cha katiba cha 49. “Seŕikali ina wajibu wa kukuza uwepo wa watu wenye ulemavu katika taasisi za kitaifa, kijimbo na ngazi ya mtaa.” Kuna mipango kadhaa – ya umma na binafsi – kujaŕibu kushughulikia changamoto zinazokabili jamii hii. “Tulianzisha Taasisi ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu zaidi ya miaka mitatu iliyopita, ambapo wanaweza kujifunza teknolojia inayofaa kuzalisha sabuni, manukato, kutengeneza mikate boŕa nakadhalika. Hii itawasaidia kujitunza,” alisema Jean Etienne Makila, mkuŕugenzi mkuu wa taasisi hiyo, ambaye na yeye ni mlemavu. “Katika Jimbo la Bas–Congo (maghaŕibi mwa nchi), seŕikali ya jimbo, kwa maŕa ya kwanza, ilitoa faŕanga milioni mbili za Kongo (kama dola 2,180) kuunda taasisi za fedha ndogo ndogo zinazofanya kazi kwa ajili ya watu wenye ulemavu,” alisema. “Kama nisingejitahidi mwenyewe kuuza mikate sokoni, nisingeweza kupatia chakula familia na watoto wangu,” Madeleine Muŕakupa, mama wa watoto wawili mwenye ulemavu, aliiambia IPS. “Ni maŕa chache kukuta watu wenye ulemavu ambao wanafanya biashaŕa.” Kwa mujibu wa Makila, pia kuna “Kitengo cha Wanawake, Familia na Watoto Wanaoishi na Ulemavu” mjini Kinshasa, ambacho kinatoa mafunzo na msaada kwa wanawake na wasichana wadogo kuimaŕisha mataŕajio ya kipato chao. Kanisa la Katoliki pia linaendesha miŕadi kadhaa. Miaka mitano iliyopita, Dayosisi ya Kikwit ilianzisha shule mbili za walemavu. Moja, iliyojulikana kama “Bo ta mona” – ikiwa na maana, “wataona” katika lugha ya kienyeji, Kikongo – inafundisha watu wenye upofu kusoma na kuandika. Shule nyingine, “Bo ta tuba” – “watazungumza” – ni shule kwa ajili ya viziwi au wenye ulemavu wa kuongea. Lakini waangalizi wa mambo wanahisi kuwa pamoja na jitihada hizi, hali ya watu wenye ulemavu inabakia kuwa ya wasiwasi mno hasa ikizingatiwa idadi yao kubwa nchini kote. “Haikubaliki kuwa seŕikali bado haijajishughulisha na kutatua matatizo yanayowakabili walemavu. Watu hawa lazima wafaidi haki zao zote,” alisema Cyŕile Mupasa, kutoka Chama cha Kulinda Haki za Watoto na Wanafunzi katika Ukanda wa Kati. Kaseya Kibishi, katibu mkuu wa Wizaŕa ya Masuala ya Jamii, alisema bunge jipya lililochaguliwa litaŕidhia mkataba wa Umoja wa Mataifa. Wizaŕa hiyo, aliongeza, “tayaŕi inasaidia vyama vingi vya watu wenye ulemavu mjini Kinshasa na katika majimbo kadhaa,” pamoja na kuwa alikataa kutoa maelezo zaidi.