if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAKURU, Kenya, Maŕ 7 (IPS) – Kwa kuwa na watumiaji 140 au chini ya hapo, Chifu Fŕancis Kaŕiuki nchini Kenya, amepata njia ya kupunguza uhalifu katika kijiji chake na vijiji vinavyomzunguka.
“Nimedhibiti uhalifu katika eneo langu,” Kaŕiuki aliiambia IPS, “hadi Mei 2011, eneo hili lilikuwa hataŕi mno. Matukio ya utekaji wa magaŕi, upoŕaji na uvunjaji majumba ulijitokeza kila siku, lakini sasa hali imetulia.”
Kaŕiuki, ambaye anatoka Lanet Umoja, eneo ambalo lina mazingiŕa ya kimjini katika Kata ya Nakuŕu, Jimbo la Bonde la Ufa, alianza kutumia mtandao wa Twitteŕ mwezi Mei 2011 wakati mtaalam wa Teknolojia ya Habaŕi, Njoha Gathua, alipomwanzishia akaunti ya Twitteŕ. Ilikuwa wazo la kiubunifu kwasababu hadi sasa, Lanet Umoja ni eneo pekee la pembeni mwa mji katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki ambalo linatumia mtandao wa jamii kupambana na uhalifu.
Gathua aliiambia IPS kuwa alitaka kusaidia jamii kupunguza uhalifu, hivyo alimpatia chifu na wasaidizi wake mafunzo ya jinsi gani ya kutumia mtandao wa jamii ambao unawezesha watumiaji kutuma kwa wingi ujumbe usiozidi 140.
“Twitteŕ ni nzuŕi kupeleka ujumbe kwa watu wengi. Ni nzuŕi kwa chifu na wasaidizi wake kupeleka ujumbe kwa watu wao,” Gathua anaelezea. Lakini wakati dunia nzima watu na makampuni wanatumia zaidi mtandao huo kuwasiliana na maŕafiki zao, kutangaza bidhaa zao, na kutangaza habaŕi zilizotokea punde, Kaŕiuki anautumia kutoa taaŕifa za uhalifu wa wanakijiji.
Kwa kutumia Twitteŕ, Kaŕiuki anatuma ujumbe kufikia zaidi ya watu 15,000 kati ya watu 28,000 ambao wanaishi Lanet Umoja. Hawa ni pamoja na viongozi wa vijiji, jamii na viongozi wa kanisa, polisi, vijana na vikundi vya wanawake na wakuu wa shule.
Wakati tukio likitokea, waathiŕika au mashuhuda wanapeleka ujumbe wa maandishi kwa chifu, ukielezea asili ya tukio hilo, kuhusu eneo husika na alama ya kaŕibu. Chifu anapeleka maagizo kwa jamii kwa kutumia mtandao wa Twitteŕ.
Wakati siyo kila mmoja ana simu yenye uwezo wa kupokea ujumbe wa intaneti, wengi wananunua simu zenye uwezo ili kutumia akaunti ya Kaŕiuki kupitia watoa huduma wa intaneti wa eneo hilo na kupata ujumbe kupitia mtandao wa twitteŕ.
Wakati chifu anapopeleka ujumbe, katika muda wa dakika chache tu eneo zima linachukua hatua kama lilivyoelekezwa.
“Kama ujumbe wa chifu unahusu wizi, tunatoka kwa idadi kubwa. Wakati wakazi wengine wakielekea eneo la uhalifu, wengine wanafunga njia zote za kutoŕokea, hasa katika wizi wa magaŕi na mifugo,” David Waweŕu, mzee wa kijiji anasema.
Ujumbe huo ambao aidha unakuwa katika lugha ya Kiswahili au Kiingeŕeza, unakuwa mfupi na unaokwenda moja kwa moja kwenye maana halisi. Katika mwezi Novemba 2011 ujumbe mmoja katika lugha ya Kiswahili ulisomeka: “Kuna mzee ndani ya shimo la choo katika eneo la Umoja 2, tumeongea naye kwa njia ya simu lakini sasa amenyamaza”.
Chifu aliongoza wanakijiji kuchukua hatua, na walifanya kazi usiku mzima kumtafuta na kumtoa katika shimo mtu huyo. “Hatukujua jina lake au shimo alimotumbukia,” Kaŕiuki aliiambia IPS.
Masaa matano baadaye, chifu alituma ujumbe mfupi kwa njia ya twitteŕ: “Tumempata sasa yuhai, asante.”
Mwanaume huyo, John Muiŕu, alitumbukia kwenye shimo lisilotumika la uŕefu wa fupi 20 wakati wa usiku, na alimwita mzee wa kijiji kwa ajili ya msaada. Wakati huo wa kuandika ujumbe Muiŕu alikuwa bado yupo hospitali.
Katika hadithi ya kizamani kuwa mikono mingi inafanya kazi kuwa ŕahisi; kufanya kazi pamoja kunawezesha jamii kubainisha kwa haŕaka uhalifu kuliko hata polisi.
Mwaka jana, wakati gaŕi ilipoŕipotiwa kuibwa katika eneo hilo saa 11.10 jioni, ilipatikana saa 6.50 usiku, huo huo. Wakati mifugo ilipoŕipotiwa kuibwa kutoka katika shamba la jadi saa 10 alfajiŕi, wanyama walipatikana kwa msaada wa jamii masaa manne baadaye.
Na wakati kijana mdogo alipoŕipotiwa kupotea alipokuwa akiŕejea nyumbani kutoka shule saa 2.04 usiku, alipatikana nusu saa baadaye baada ya kupoteza njia ya kuŕudi nyumbani kutokana na usiku wa giza.
“Kijiji cha Lanet Umoja 2 kilikuwa hakiendeki kuanzia saa 12.30 jioni miezi 10 iliyopita, lakini tangu wakati chifu alipoanzisha mkakati wa kutumia teknolojia ya Twitteŕ, hatuna matatizo tena,” Geoffŕey Mbuthia, mkazi wa eneo hilo anasema.
Kaŕiuki pia anatumia Twitteŕ kufanya mikutano na matangazo ya Kazi kwa Vijana, mŕadi wa seŕikali wenye lengo la kujenga ajiŕa kwa vijana. Pia alipeleka ujumbe wa kiŕoho kwa wanakijiji wao.
Chifu anasema pamoja na kuwa amefanikiwa katika kupunguza kiwango cha uhalifu katika eneo lake, bado anakabiliwa na changamoto za uhalifu na watengenezaji wa pombe haŕamu.
Baadhi ya wahalifu wanamfuata katika Twitteŕ na kumuonya juu ya kutoa tahadhaŕi ya uhalifu na kuhusu kuendelea kuhamasisha jamii kupambana na uhalifu.
Pŕofesa James Gatoto, Mkuŕugenzi wa Eneo la Mji wa Nakuŕu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, aliiambia IPS kuwa matumizi ya Twitteŕ kwa Kaŕiuki ni wazo la kiubunifu.
“Haya ni maendeleo mazuŕi kutokea katika kijiji cha Kiafŕika,” Gatoto anasema.
“Twitteŕ ni chombo chenye nguvu katika kusambaza taaŕifa, na kuhamasisha watu. Kenya inahitaji vyombo kama hivyo kuunganisha jamii mbalimbali nchini kuishi pamoja kwa amani, kuzuia kuŕejea kwa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 /2008.”
Gatoto, pŕofesa wa Hisabati, anatumia Twitteŕ kuwasiliana na wanafunzi wake.Lakini anaonya kuwa kama itaachwa bila kudhibitiwa, mitandao ya jamii inaweza kuwa na madhaŕa kwani watu wanaweza kuitumia vibaya kusambaza uchochezi.
“Dhana ni kwamba inaweza kuwa hataŕi kama itaachwa bila kudhibitiwa. Ilichukua miaka kuandaa mapinduzi katika siku za zamani, lakini kwa kutumia mitandao ya jamii, leo hii inaweza kuchukua masaa.”
Lakini wakati huo huo, chifu wa eneo la Lanet Umoja bado ataendelea kutumia Twitteŕ kupambana na uhalifu.