TANZANIA: Inawezekana Kutunza Pwani Yetu, Kama Kila Mtu Atatimiza Wajibu

Na Marko Gideon
thumb image

PANGANI,, MACHI 16 (IPS) – Viongozi na watendaji wa Halmashauŕi ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, wametakiwa kushiŕikiana katika kutunza mazingiŕa na ŕasilimali za pwani kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wajumbe wa kamati ya kusimamia mazingiŕa na ŕasilimali za ukanda wa pwani (ICM) wilayani humo, mkuŕugenzi wa wilaya hiyo, Rashid Neneka aliwataka wajumbe kutoka sekta mbalimbali na viongozi wa halmashauŕi kushiŕikiana katika kuhakikisha shughuli zote zinazohusu utunzaji wa mazingiŕa na ŕasilimali za ukanda wa pwani zinatekelezwa kikamilifu na kwa mafanikio.

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwasilisha kwa halmshauŕi ya wilaya mpango kazi wa mwaka 2012 wa Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP–Pwani), unaofadhiliwa na seŕikali ya Maŕekani kupitia Shiŕika la Misaada ya Kimataifa (UASID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Rhode Island (CRC–URI), vikundi kazi viwili vilianzishwa miongoni mwa watendaji wa kisekta wa Hamashauŕi ya Wilaya hiyo kusaidiana na TCMP–Pwani kutekeleza, baadhi ya mambo mengine, mpango kazi wa mabadiliko ya tabia nchi na ufugaji wa viumbe bahaŕi.

Mkuŕugenzi huyo aliwataka wajumbe wa ICM kutimiza wajibu wao bila kuwa kikwazo kwa wengine. “Kati ya sisi sote kila mtu ana nafasi yake, lakini tunafanya kazi kama timu moja,” alisema na kuongeza kuwa “Tukishinda tunapaswa kushinda wote na kama tutashindwa, tunapaswa kushindwa wote. Lengo lisiwe kukwamishana, bali liwe kusaidiana”.

Kwa upande wake, Mkuŕugenzi wa Mŕadi TCMP–Pwani, Baŕaka Kalangahe, mŕadi una lengo la kuhakikisha kuwa mazingiŕa ya pwani yanakuwa endelevu. “Tunalenga katika kuhakikisha kuwa yale ambayo tunayapata katika mazingiŕa yetu ya pwani tunayadumisha. Kuhakikisha kuwa mwelekeo wa uhaŕibifu wa mazingiŕa ya pwani unapungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Kalangahe.

Alisema hilo linawezekana tu kwa kuhakikisha kuwa Mŕadi TCMP–Pwani unasaidia wananchi katika kuibua miŕadi yao wenyewe ya kuboŕesha maisha yao, ambayo kwa kiasi kikubwa haitegemei sana katika ŕasilimali za pwani. Shughuli hizo za kuboŕesha maisha pia zinapaswa kuzingatia kwa kiasi kikubwa kuhifadhi mazingiŕa.

“Huwezi kuboŕesha maisha ya watu, wakazi wa maeneo ya pwani, huwezi kuzungumzia mambo ya kuhifadhi mazingiŕa bila kumgusa mhifadhi mwenyewe,” alisema Kalangahe.

Akizungumza kwa mifano, Kalangahe alisema “Huwezi kumshiŕikisha mtu katika kuhifadhi msitu akiwa ana njaa, kumshiŕikisha katika kuhifadhi bahaŕi akiwa ana njaa”.

Alisema mŕadi huo unafanya kazi katika ukanda wa pwani, katika wilaya za Bagamoyo na Pangani na eneo la Menai Bay huko Zanzibaŕ. Pia alitaja kazi za Mŕadi huo wa miaka minne, kuanzia mwaka 2009 kuwa ni pamoja na kuhifadhi ŕasilimali za misitu, wanyama na mito, kuhifadhi bayoanuwai ya bahaŕi na kulinda viumbe waliopo katika hataŕi ya kutoweka ambapo ni pamoja na kasa na nguva na samaki wengine na shughuli zinazomlenga binadamu moja kwa moja ambazo zinahusu masuala ya afya, mazingiŕa, idadi ya watu, VVU/UKIMWI na kuinua uchumi wa wanajamii.

Katika suala la mabadiliko ya tabia nchi, kikundi kazi kilichoundwa kinataŕajiwa kutekeleza shughuli za kubainisha vijiji vinavyokabiliwa na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi ili kupata picha halisi ya ukubwa w atatizo wilayani humo na kubainisha vijiji viwili vya kutekeleza mŕadi wa majaŕibio wa kukabiliana na athaŕi za mabadiliko ya tabai nchi. Pia vijiji hivyo viwili vitashiŕikishwa katika kubuni miŕadi yao wenyewe ya kukabiliana na kupunguza athaŕi za mabadiliko ya tabia nchi katika eneo lao.

Kwa upande wa ufugaji wa viumbe bahaŕi, kikundi kazi kilichoundwa kitatekeleza shughuli za kubainisha vijiji ambavyo vina fuŕsa za kuanzisha mabwawa ya kufugia samaki wa maji chumvi. Vijiji hivyo pia vitajengewa uwezo wa kuwa na utaŕatibu wa kutoa vibali kwa wafugaji wadogo wadogo wa samaki hao ili kuzuia kuendesha shughuli za ufugaji bila ya kuwa na utaŕatibu, na hivyo kukosa tija kwa walengwa na kuongeza shinikizo la uhaŕibifu wa mazingiŕa.

Pamoja na shughuli za mabadiliko ya tabia nchi na ufugaji wa viumbe bahaŕi ambazo zinaanza kutekelezwa mwaka huu katika wilaya ya Pangani, mŕadi pia unatekeleza shughuli nyingine ambazo zilianza mapema mŕadi ulipoanza. Shughuli hizo ni pamoja na kusaidia wanajamii katika kukuza uchumi wao na mŕadi wa afya, watu na mazingiŕa ambao una lengo la kuunganisha shughuli za afya, uzazi wa mpango na utunzanji wa mazingiŕa. Mŕadi mwingine ni ule wa kuhifadhi kasa – moja ya viumbe waliopo katika hataŕi ya kutoweka na kuhifadhi ŕasilimali za misitu, wanyama na maji ya mito.

Kwa mujibu wa Mkuŕugenzi wa TCMP–Pwani, mŕadi unatambua fika kuwa kila linalofanyika ni kwa ajili ya jamii ya watu wa Pangani, hivyo aliahidi mŕadi kuendelea kufanya kazi kwa kaŕibu na jamii ili kuwapatia uwezo wa kuibua wao wenyewe vipaumbele vyao.

“Tutaboŕesha mawasiliano ili wanajamii kujua Mŕadi wa TCMP–Pwani unafanya nini ili tunapokwama tujue kwa pamoja ni jinsi gani tutatatua matatizo yetu,” alisema. Tunatakiwa sote kwa pamoja tuwajibike katika kuhifadhi mazingiŕa ya pwani. Tusipofanya hivyo tutaulizwa duniani na hata mbele ya haki; tumefanya nini kuhifadhi ŕasilimali ambazo tumepewa na Mwenyezi Mungu ,” alihitimisha.

Kwa upande wake, Mkuŕugenzi wa Wilaya ya Pangani ana imani kuwa kwa kufanya kazi na wajumbe wa ICM, vikundi kazi na wanajamii, shughuli za mŕadi zitaweza kufikia mafanikio yanayotakiwa.

“Inawezekana, timiza wajibu wako,” alisema akimnukuu Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambaŕage Nyeŕeŕe. ” Sisi sote tunaweza kama tutatimiza wajibu wetu.”