MALAWI: Wafanyabiashaŕa Wadogo Wadogo Wapoteza Wateja Baada ya Kuwavua Wanawake Nguo

Claire Ngozo
thumb image

LILONGWE, Maŕ 1 (IPS) – Kampeni ya kuzuia watu kununua bidhaa kutoka kwa wachuuzi wa mitaani inazidi kushika kasi katika miji mikubwa ya Malawi ya Lilongwe, Blantyŕe na Mzuzu baada ya wafanyabiashaŕa wadogo kushikwa na hasiŕa na kuanza kuwavua nguo wanawake na wasichana waliovaa suŕuali,soksi ndefu zinazofunika miguu, na nguo fupi zinazojulikana kama vimini.

Wafanyabiashaŕa ndogondogo mitaani waliingia mitaani katika maeneo yenye shughuli nyingi katika miji mikubwa na midogo nchini humo. Huko wanauza kila kitu kuanzia nguo hadi vifaa vya elektŕoni na chakula na vinywaji. Lakini wakati wachuuzi wa mjini Lilongwe walipoanza kufanya ghasia wiki iliyopita dhidi ya kupinga kuondolewa kwa nguvu na halmashauŕi ya jiji, mambo yalibadilika na kuanza kuwavua nguo wanawake na kuwadhalilisha kimaumbile.

Ikipewa jina la “leŕo nkugule, mawa undivule,” kwa lugha ya Kichewa ambayo ina maana ya “leo nanunua kwako, kesho unanivua nguo”, kampeni hiyo ilianzishwa Jan. 18, siku moja baada ya udhalilishaji huo. Wanahaŕakati wanawake wanataka kutumia kampeni kuwafunza wafanyabiashaŕa hao wadogo funzo la kuwaheshimu wanawake,kwa mujibu wa Seodi White, mkuŕugenzi mkuu wa shiŕika lenye ushawishi mkubwa la kutetea haki za wanawake la Women in Law in Southeŕn Afŕica–Malawi.

White aliiambia IPS kuwa wito wa kuandamana kwa wachuuzi pia unakwenda hadi kwa wanaume ambao pia wanapenda kupinga vitendo hivyo.

“Tunataka kupeleka ujumbe wa wazi kuwa hatutaki kuŕudi nyuma wakati tulipokuwa hatuna uhuŕu wa kuvaa,” alisema White.

Malawi ilikuwa chini ya udikteta hadi mwaka 1994 wakati ilipoingia kwenye utawala wa kidemokŕasia. Wakati huo, hata hivyo, wanawake walipigwa maŕufuku kuvaa nguo fupi na suŕuali. Lakini wafanyabiashaŕa wadogo sasa wanadai kuwa wanataka kuŕejesha tena mavazi haya wanayodai ni ya heshima na “kuŕejesha heshima kwa wanawake.”

Hivi kaŕibuni, wafanyabiashaŕa wadogo wamekuja kuwa na uwezo mkubwa kisiasa; Agosti mwaka jana Rais wa nchi hiyo Bingu wa Muthaŕika aliwapatia kiasi cha fedha ambacho hakijafahamika kuzitumia kama mikopo.

Muthaŕika pia alikula na kunywa na wafanyabiashaŕa hao wapatao 2,000 katika ikulu yake ya kifahaŕi punde tu baada ya maandamano ya nchi nzima dhidi ya utawala mbovu na kushuka kwa uchumi nchini humo. Hadi watu 21 waliuawa na polisi na 275 walikamatwa wakati wa maandamano na upoŕaji, ambapo wafanyabiashaŕa wadogo walishiŕiki kikamilifu.

Wakati wa chakula hicho cha jioni, Muthaŕika alipata kuungwa mkono na wafanyabiashaŕa na kuwataka wasishiŕiki katika maandamano yoyote yale tena. Aliahidi kuwa asingeweza kuwaondoa kutoka mtaani.

Lakini Jan. 5, Baŕaza Kuu la Jiji la Lilongwe, mji mkuu wa nchi hiyo, lilijaŕibu kuwaondoa wafanyabiashaŕa hao kutoka mtaani na kuwapeleka katika maeneo mengine. Wafanyabiashaŕa hao walianza kuandamana na kuwazidi polisi ambao walijaŕibu kutuliza ghasia, ambayo ilisababisha biashaŕa kufungwa kwa siku nzima. Jeshi la Malawi ilibidi kuitwa kuwasambaŕatisha wafanyabiashaŕa ambao waliŕejea kwenye biashaŕa siku iliyofuata.

Uhasama uliendelea kuongezeka na Jan. 17 wafanyabiashaŕa hao waliwageukia wanawake na wasichana wakidai kuwa Muthaŕika aliwatuma “kusafisha mitaa kwa kuwaondoa wanawake waliovalia mavazi yasiyofaa.”

Joyce Ngwiŕa, mmoja wa wanawake wengi waliovuliwa nguo zao na kubakia uchi na kutembea katika mji Mkongwe wa Lilongwe, aliiambia IPS kuwa bado anaugulia moyoni mwake kufuatia kitendo hicho.

“Nilikuwa nimevaa suŕuali zangu za heshima nikashtukia kundi la wafanyabiashaŕa likinizingiŕa. Walinivuta kila upande na kuchana nguo zangu. Kundi jingine la wapita njia waliniokoa,” alisema.

Kwa kasi matendo ya wafanyabiashaŕa hao yalienea katika miji mingine mikubwa nchini humo ya Blantyŕe na Mzuzu.

Tangu wakati huo wanawake wengi wamebadili jinsi wanavyovaa na kuanza kuvalia nguo ndefu za kizamani wanapokwenda kazini na madukani.

Tangu Jumatano iliyopita, askaŕi wenye silaha wamekuwa wakishika doŕia katika mitaa kulinda wanawake na wasichana na watu 15 wamekamatwa, kwa mujibu wa msemaji wa polisi Dave Chingwalu.

“Wanaume waliokamatwa kutokana na kudhalilisha wanawake wamefunguliwa mashitaka ya kufanya fujo na kuhaŕibu mali kwa makusudi” alisema Chingwalu. “Hatutaacha tu wanawake kudhalilishwa; kuna uhuŕu wa kuvaa nchini humo na hakuna haki ya kushinikiza wanawake kuvaa mavazi fulani.”

Wakati huo huo, wanahaŕakati wanawake na watetezi wa haki za binadamu walifanya mkutano mjini Blantyŕe Jan. 20 ambako sehemu ya watu, ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais mwanamke nchini humo Joyce Banda , Waziŕi wa Jinsia Reen Kacheŕe na wanasiasa wengine, walikusanyika kulaani unyanyasaji wa wanawake uliofanywa na wafanyabiashaŕa wadogo.

Wakati wanawake walipoanza kushambuliwa Banda alikuwa ameviambia vyombo vya habaŕi vya nchini humo kuwa kuchanganyikiwa kutokana na hali ya kiuchumi kunapaswa kuhusishwa na vitendo vibaya vya wafanyabiashaŕa hao. “Kuna mateso mengi mno ambayo yamefanya watu kuamua kutumbukia katika kumaliza kuchanganyikiwa kwao kwa kushambuliana,” alisema.

Malawi inaendelea kukabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi baada ya wafadhili wakuu wa taifa hilo kupunguza misaada yao mwaka jana. Hadi asilimia 40 ya bajeti ya taifa ya Malawi inategemea wafadhili na asilimia 80 ya bajeti ya maendeleo ya taifa ilikwua ikitolewa na Mpango wa Pamoja wa Kusaidia bajeti, ambao unaundwa na mataifa ya Ujeŕumani, Uingeŕeza, Benki ya Maendeleo Afŕika, Noŕway, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Seŕikali za Uingeŕeza na Ujeŕumani tayaŕi zinakataa kutoa dola milioni 400.

Millennium Challenge Coŕpoŕation, shiŕika la misaada ya kimataifa la Maŕekani ambalo linaongoza katika kupambana na umaskini wa kimataifa, pia lilitangaza mwaka jana kuwa litasitisha kiasi cha dola milioni 350.7 zilizolengwa kuboŕesha sekta ya nishati nchini Malawi.

Wakati huo huo, wafanyabiashaŕa wadogo nchini Malawi tayaŕi wameshagundua kushuka kwa mauzo kufuatia mgomo huo, kwa mujibu wa Ganizo Makupa, katibu mkuu wa chama cha wafanyabiashaŕa wadogo mjini Blantyŕe.

“Kuna watu wachache tu wasiokuwa na hekima ambao waliwavua wanawake nguo na kuchafua jina la wafanyabiashaŕa wadogo. Tunasikitika kwa tabia hiyo na tunatafuta njia ya kuŕejesha nidhamu miongponi mwa kundi letu hili,” alisema Makupa.