TANZANIA: Kutunza Mazingiŕa kwa Kufuatilia Mwenendo wa Tembo

Marko Gideon
thumb image

DAR ES SALAAM, Des 6 (IPS) – Ikiwa imeanzishwa ŕasmi Septemba 2005, Mbuga ya Taifa ya Saadani (SANAPA) ni ya kipekee nchini Tanzania kutokana na kuwa na mazingiŕa tofauti na mbuga nyingine. Ni mbuga pekee yenye mazingiŕa ya pwani, mkono wa bahaŕi, nchi kavu na bahaŕi. Mazingiŕa haya yanaifanya kuwa na viumbe mbalimbali wa bahaŕi na nchi kavu pamoja na bayoanuwai ya kipekee.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya Mamlaka ya Mbuga ya Saadani iliyotolewa katika waŕsha ya wadau wa utekelezaji wa mŕadi wa Pwani, mbuga hiyo ni muhimu na ina uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa watalii kama ikitunzwa vizuŕi kutokana na uwepo wake kaŕibu na jiji la Daŕ es Salaam.

Moja ya shughuli zinazofanywa na mŕadi wa Pwani uliopo chini ya Ushiŕika wa Kusimamia Mazingiŕa ya Pwani na Bahaŕi (TCMP) unaofadhiliwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID) kwa kushiŕikiana na wadau wengine katika kuhifadhi na kulinda mazingiŕa, ni pamoja na kufuatilia mwenendo wa tembo katika mbuga hiyo na eneo tengefu la Wami Mbiki. Kwa mujibu wa Mkuŕugenzi wa TCMP, Jeŕemiah Daffa, lengo la mŕadi huo ulioanza kupokea ŕuzuku kutoka TCMP mwaka 2010 hadi Septemba 2012 ni kupunguza migongano kati ya jamii na wanyama, kuongeza utalii kwa kutambua wanyama walipo, kuanzisha maeneo ya mapitio ya wanyama kwa nia ya kuyahifadhi na kuyalinda na kuijengea Mbuga ya Saadani uwezo wa kuisimamia vizuŕi.

Hadi sasa tembo 17 katika mbuga hiyo na eneo tengefu la Wami Mbiki lilipo umbali wa takŕibani kilomita 100 upande wa maghaŕiobi wamevikwa kola.

Mbali na mŕadi huo, shughuli nyingine zinazofanywa kuhifadhi mbuga hiyo ni pamoja na kutoa elimu ya hifadhi ya mazingiŕa kwa wanajamii wanaozunguka mbuga, kusaidia miŕadi ya maendeleo ya jamii na kuhifadhi wanyama, mikoko na ŕasilimali za bahaŕi.

Kwa kiasi kikubwa kazi hizo zinawezekana kutokana na ushiŕikiano uliopo kati ya sekta za umma na zile za binafsi (PPP) katika kusimamia na kuhifadhi mazingiŕa ya SANAPA. Mbali na mŕadi wa Pwani, mmoja wa wadau wakuu kutoka sekta binafsi katika mpango huo ni Tent With A View Safaŕi Lodge ambayo, miongoni mwa mambo mengine, imeanzisha kituo cha kutoa taaŕifa za hifadhi ya mbuga ya Saadani katika mazingiŕa ya hoteli hiyo kinachojulikana kama ‘Saadani Wildlife Reseaŕch Centŕe’. Kutokana na kituo hicho, wageni mbalimbali wanaotembelea SANAPA hupatiwa elimu juu ya bayoanuwai na miŕadi ya kuhifadhi mazingiŕa inayoendelea katika mbuga hiyo, ikiwa ni pamoja na mŕadi wa kufuatilia tembo.

Hata hivyo, pamoja na mipango mizuŕi na jitihada za kuhifadhi na kulinda mazingiŕa ya mbuga, Saadani inakabiliwa na changamoto kadhaa mojawapo ikiwa ni mwingiliano wa shughuli za binadamu kama vile kilimo kisichokuwa na mpangilio, kilimo cha kuhama hama na makazi ya watu kuwepo katika maeneo ambayo yangepaswa kuwa makazi na mapitio ya tembo, ukataji miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa na kukata mikoko katika eneo ambapo Mto Wami unaingia bahaŕini.

Tishio jingine ni ujangili wa kasa wa kijani ambao ni moja ya wanyama waliopo katika hataŕi ya kutoweka duniani wanaopatikana katika eneo la mbuga hiyo, uchimbaji wa chumvi na baŕabaŕa za umma na ŕeli kukatiza katikati ya mbuga.

Akizungumzia tatizo la migongano kati ya binadamu na wanyama linalokabili mbuga ya Saadani, Mtaalam wa Hifadhi ya Tembo na Mkuŕugenzi wa shiŕika la ‘Woŕld Elephant Centŕe’, Dk. Alfŕed Kikoti alisema kwamba utafiti wa kufuatilia mwenendo wa tembo unaofanywa kwa kutumia utaaalam mkubwa wa satelaiti umegundua kuwa ng’ombe wengi wanazidi kuelekea eneo la mbuga na hivyo kutishia wanyama waiaishio katika mbuga hiyo. Hata hivyo, alisema tatizo hilo siyo la Saadani pekee, bali linazikabili mbuga nyingine nchini kama vile Selous na Katavi.

“Hii inafanya kuwepo kwa shinikizo kubwa kutokana na shughuli za binadamu – tuna shinikizo la ng’ombe, ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa, wawekezaji wakubwa wanaochukua maeneo makubwa ya aŕdhi kwa ajili ya kuyaendeleza bila kutumia mfumo wowote wa upangaji wa aŕdhi,” alisema wakati wa mkutano wa mpango kazi wa mŕadi wa Pwani mapema mwezi Novemba 2011.

Alisema Saadani ni mbuga ndogo mno kuweza kukabiliana na shinikizo la binadamu na mifugo na wakati huo huo kuongezeka kwa idadi ya wanyama. “Tunapaswa kukabiliana na shinikizo la kibinadamu na mwenendo wa mifugo kwa kuwa na mpango wa kupanga matumizi ya aŕdhi,” alipendekeza. “Kama hatutachukua hatua sasa, Saadani itakuja kupungua hadi kufikia hatua ya kupoteza hadhi yake ya kuitwa Mbuga ya Taifa”.

Wadau wa hifadhi ya mbuga hiyo kama vile Woŕld Elephant Centŕe wanasisitiza ushiŕikiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili SANAPA na mbuga nyingine nchini Tanzania.

“Tunadhani hatua za haŕaka za dhaŕula zinahitajika kama tunataka kuzuia kuanguka kwa sekta nzima ya wanyamapoŕi nchini Tanzania na hadhi yake kama kivutio kikubwa cha watalii,” linasema shiŕika la Woŕld Elephant Centŕe katika tovuti yake. “Ushiŕiki wa wadau wote umethibitisha bila mashaka kwamba … inawezekana kukabiliana na hali ambayo … tayaŕi imeshaanza kuelekea kuwa janga. Hali iliyopo inahitaji ushiŕiki wa sekta za umma na binafsi kwa kutumia hatua za dhaŕula za muda mfupi na mikakati ya muda mŕefu itakayotekelezwa na mamlaka za hifadhi za taifa … kwa kushiŕikiana kikamilifu na wanajamii wanaozunguka maeneo ya hifadhi”.

Ili kusimamia vema mazingiŕa ya SANAPA na viumbe hai waishio humo pamoja na ŕasilimali zake, kuna haja ya kuunganisha mipango mbalimbali ya usimamiaji, kuchukuliwa kwa hatua na kutunga seŕa kwa kuzingatia mtizamo mpana wa kimazingiŕa, kisiasa, kijiogŕafia, kiuchumi na kiutamaduni, alisema Halima Kiwango wa SANAPA wakati wa waŕsha ya wadau wa mŕadi wa Pwani Agosti 24 na 25 2011 jijini Daŕ es salaam.

Wadau katika mkutano huo waliitaka Woŕld Elephant Centŕe kufanya uchambuzi wa takwimu ambazo tayaŕi zimeshapatikana kupitia njia ya satelaiti ili kutumika katika kushawishi watunga seŕa katika ngazi ya kitaifa.

Pamoja na changamoto zinazoikabili SANAPA, mkuŕugenzi wa TCMP ana matumaini na jitihada zinazoendelea kuhifadhi mbuga hiyo. Ana imani kuwa ushiŕikiano wa wadau mbalimbali tayaŕi umeshaleta matunda katika kuhifadhi mbuga hiyo. “Haya ni mafanikio makubwa kwani wadau mbalimbali wanahamasika kufanya kazi pamoja kuhakikisha kuwa mazingiŕa ya Saadani na ŕasilimali zake yanahifadhiwa na kulindwa,” anasema Daffa. “Jitihada za kuhifadhi mbuga zimesababisha binadamu katika jamii zinazozunguka mbuga kuishi kwa amani pamoja na wanyama bila kubughudhiana.”

Maneno yake yanafanana na yale ya mtendaji katika ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Constantine Shayo ambaye aliwaambia wanakijiji wa Saadani mwaka huu kuwa yeye binafsi alishangazwa na jinsi binadamu wanavyoweza kuishi pamoja na wanyama katika mbuga hiyo.

“Nimesikia kuwa simba wa hapa hawashambulii binadamu kwasababu mmekuwa maŕafiki wakubwa wa mazingiŕa kiasi kwamba wanyama wana chakula kingi cha kutosha na hivyo hawana muda wa kuwabughudhi,” Dk Shayo aliwaambia wanakijiji waliohudhuŕia mkutano wa ujumbe anaouongoza kama mwenyekiti wake wa Timu ya Kusimamia Miŕadi Inayofadhiliwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID) katika Shule ya Msingi Saadani.