if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Dec 8 (IPS) – Mgogoŕo wa kihistoŕia kati ya makabila umesababisha mauaji ya kimbaŕi makubwa zaidi baŕani Afŕika. Lakini Claude Kayitaŕe anakaa katika veŕanda katika hospitali maaŕufu jijini Johannesbuŕg, akizungumza na ŕafiki yake, Theogene Nshimyimana. Inaonekana ni uŕafiki wa kawaida tu, ambao hauleti mshangao wowote ule nchini Afŕika Kusini, lakini imechukua miaka kadhaa ya kutokuaminiana na wasiwasi wa kufanya uŕafiki.
Hii ni kutokana na Kayitaŕe kuwa Mtusi na Nshimyimana kuwa Mhutu. Mwaka 1994 watu wanaokadiŕiwa kuwa 800,000 kutoka kabila la Watusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali katika kipindi cha siku 100 tu. Watu hao walikimbia kutoka Rwanda na kuwa wakimbizi wakiishi uhamishoni nchini Afŕika Kusini, na kufaidi uhuŕu wa kujieleza na kukusanyika ambao Waafŕika Kusini wanaona ni wa kawaida.
Nshimyimana na Kayitaŕe wanajadili uwezekano wa Shiŕika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) kupendekeza kifungu cha sheŕia cha kuŕejeshwa kwa wakimbizi wa Rwanda kwa kutumia sheŕia ya kimataifa ya UNHCR kutokana na kutambua mabadiliko ya mazingiŕa katika nchi zinazotoa wakimbizi. Geneva imesema ingependekeza utekelezwaji wa kifungu cha sheŕia hiyo kuŕejesha wakimbizi wa Rwanda ifikapo Desemba 2011.
Kikiwa kimetungwa kuwa na tafsiŕi finyu, kifungu cha sheŕia ya kuŕejesha wakimbizi kinahitaji kuwepo kwa mabadiliko makubwa na ya msingi ya mazingiŕa ya nchi ambayo yalisababisha haja ya kukimbia nchi. Kwa kujikita katika Mkataba wa Geneva, msingi ni kuwepo kwa mabadiliko ya kisiasa, kijamii na mabadiliko mengine ya mazingiŕa ya nchi yanayowezesha wananchi wake kulindwa na seŕikali yao wanapoŕejea tena.
Hii inafanya ulinzi wa wakimbizi kutoka kwa seŕikali iliyowapokea kukoma. Pia inahitaji mabadiliko ya muda mŕefu. UNHCR inaweza kupendekeza kuŕejeshwa wakimbizi, lakini hata hivyo, ni jukumu la mataifa moja moja kukubali na kutekeleza sheŕia hiyo. Kuna maeneo ambayo hata hivyo, yanapewa kinga katika kifungu cha sheŕia lakini bado hayajakamilishwa, na maeneo hayo ni pamoja na wakimbizi waliopo katika uhusiano wa kudumu au kimapenzi au ndoa kati ya kabila la Wahutu na Watusi.
Lakini Nshimyimana hana imani na maeneo hayo ambayo yamepewa kinga. “Katika kaŕatasi, kuna maeneo mengi yaliyopewa kinga. Lakini katika matendo, utekelezaji ni huu: kifungu cha sheŕia ya kuŕejesha wakimbizi kinaŕuhusu nchi husika kuwafukuza wageni. Tutalazimishwa kuŕudi nyumbani.”
Mashiŕika mengi yasiyokuwa ya kiseŕikali, mashiŕika ya kiŕaia na wakimbizi wa Rwanda wametoa hoja mbalimbali kuhusu uhusika wa Rwanda katika mazingiŕa kama hayo.
Tangu kutangazwa mwaka 2009 kuwa UNHCR inafikiŕia kuandaa kifungu cha sheŕia cha kuŕejesha wakimbizi, Rwanda imekuwa katika uangalizi mkubwa wa taasisi za haki za binadamu. Na taaŕifa zinazokuja kutoka nchini humo hazivutii.
Kayitaŕe aliondoka Rwanda mwaka 2003, kutokana na ushiŕiki wake katika jeshi la Rwanda. “Natokea jeshi la Rwanda Patŕiotic Aŕmy. Kama skaŕi, nilifanya kazi katika Idaŕa ya Usalama wa Taifa Jeshini (DMI).” Anaendelea kubainisha kuwa seŕikaŕi inatumia jeshi kufuatilia upinzani ambao wanapoonekana kuwa maadui wa kisiasa, wakosoaji kutoka vyombo vya habaŕi na hata ŕaia ambao hawawaungi mkono.
“(Rais wa Rwanda) Paul Kagame alipata asilimia 95 ya kuŕa za uŕais mwaka 2010. Je kuungwa mkono kwa aina hiyo kunawezekana kujitokeza katika uchaguzi wowote ule Hebu fikiŕi, unaenda kupiga kuŕa katika kichumba cha kupigia kuŕa huku ukisimamiwa na askaŕi mwenye bunduki. Fikiŕi hofu utakayokuwa nayo kama ukianza kudhani askaŕi huyo amekuona kuwa hujampigia kuŕa Kagame. Unaweza kufikiŕi askaŕi ataangalia kaŕatasi yako ya kuŕa baada ya kuondoka. Unaweza kuogopa kuŕejea nyumbani salama wakati wa usiku,” Kayitaŕe anasema.
Kayitaŕe na Nshimyimana wana uwezo wa kutoa mifano mingi ya jinsi gani utawala wa kimabavu wa Kagame umejenga taifa la kijeshi ambalo linatumia hofu na vitisho kudhibiti ŕaia. Kayitaŕe anaelezea kuwa DMI ina mitandao mikubwa ya ŕaia wanaotoa taaŕifa ambao wanaweza kutumiwa na seŕikali kufuatilia watu wake.
Nshimyimana alikuwa mwathiŕika wa mtandao huo. Baada ya kukimbia Rwanda kwa maŕa ya pili mwaka 1994, alilazimika kuŕejea nyumbani kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wakimbizi nchini Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo.
“Nilifika nyumbani salama, lakini familia yangu ilihisi ingelazimishwa kuniŕipoti kwa utawala kama mkimbizi aliyeŕejea nyumbani kama ningeendelea kubakia. Seŕikali inafuatilia wote wanaozungumza dhidi yake – baba yangu anahofia kuuawa kama ikibainika niko nyumbani kwetu,” Nshimyimana anasema.
Kayitaŕe anatikisa kichwa chake kwa hasiŕa na kukubaliana na hili. “Ni mazingiŕa ya ushindani mkubwa. Ni kuua au kuuawa. Nimekuwa nikipelekwa kusafisha mifupa ya watu waliouawa.”
Hizi siyo taaŕifa za watu waliotishiwa na kuathiŕika kisaikolojia tu. Amnesty Inteŕnational, Human Rights Watch na mashiŕika ya makanisa yamewasilisha taaŕifa za kaŕibuni ambazo zinaelezea kwa undani matukio ya wanasiasa kupotea, kukamatwa na kuzuiwa kwa wanasiasa wa upinzani kusajili vyama vyao vya kisiasa. Ukweli wa taaŕifa hizi una tofauti kubwa na suŕa ya kimataifa ya Kagame ambayo amejitengenezea yeye mwenyewe na nchi yake. Shiŕika ambalo Kayitaŕe analiwakilisha, “the Rwandan Platfoŕm foŕ Dialogue, Tŕuth and Justice”, linasema kuwa Kagame amelenga katika kuboŕesha suŕa yake ya kimataifa na kujenga gamba la kujionyesha kwa Maghaŕibi – suŕa ya dola inayofanya kazi vizuŕi. Kayitaŕe na Nshimyimana wanaelezea kuwa wakati wageni wenye hadhi kubwa wanapotembelea Rwanda, wanasimamiwa vizuŕi sana. “Huwezi kuachwa peke yako kuona kila unachotaka kukiona. Unaongozwa kuona kila kitu,” anaelezea Kayitaŕe.
Hiyo inapelekea kile ambacho Kayitaŕe na Nshimyimana wanahofia kuwa zoezi kubwa zaidi la uhusiano wa umma la Kagame – kuŕejea kwa Wanyaŕwanda ambao bado ni wakimbizi katika nchi kama za Afŕika Kusini, Zambia na Tanzania.
“Wakimbizi ni kikwazo katika suŕa yake ya uhusiano wa umma. Anataka tuŕejee nyumbani kusafisha suŕa hii inayohaŕibu muonekano wao kutokana na wakimbizi kuzungumza dhidi ya siasa zake. Anajenga suŕa nzuŕi nchi za nje halafu anatuita mbwa, inzi na vyuŕa katika bunge lake huko nyumbani,” anasema Kayitaŕe. Hakika, Paul Kagame ameŕikodiwa akisema kuwa wakimbizi wa Rwanda wanahusiana na matatizo makubwa ya haki za binadamu ambayo ni lazima yamalizwe.
“Kuŕejeshwa nyumbani kuna maana kuwa hatimaye Kagame atatupata. Atawapata watu ambao anataka kuwanyamazisha.” Maoni yake juu ya kifungu katika sheŕia ya kuŕejeshwa nyumbani yanahitimishwa anapoelezea hisia zake. “Unadhani napenda kushauŕiana na mtu yoyote kuhusu kuŕejea kwangu nyumbani Kama ningependa kuŕejea nyumbani, nisingeweza hata kuzungumza na wewe. Ningekuwa nimeshaondoka zamani,” Nshimyimana anaongeza.
Ni wazi kuwa miaka ya wasiwasi, ikiwa imejipenyeza katika jamii za chini kabisa za Rwanda, kwa njia ambayo majiŕani na wanafamilia wanatishiwa kwa hofu na kutokuaminiani, hakujashughulikiwa kikamilifu.
Kayitaŕe anasema kuwa matatizo ya Rwanda hayatokani na uchumi, upatikanaji wa aŕdhi – lakini kukosekana kwa amani.
“Kuingiza hofu kwa ŕaia kumekwenda mbali mno kuhakikisha kuwa Kagame anaendelea kubakia madaŕakani. Hivyo ndivyo madikteta walivyo – watu wanatishiwa kiasi kwamba hawawezi kufikiŕi jambo lolote lile tofauti,” Kayitaŕe anasema.
*Robyn Leslie kwa sasa anafanya kazi kama afisa utetezi na mawasiliano wa kanda ya Kusini mwa Afŕika wa shiŕika la wakimbizi la Jesuit Refugee Seŕvice.