LIBERIA: Uchaguzi Waŕudiwa Pamoja na Kuwepo kwa Mgomo na Mauaji

Robbie Corey-Boulet
thumb image

MONROVIA, Dec 5 (IPS) – Walibeŕia walikwenda kupiga kuŕa katika kile kinachoonekana idadi ya kawaida ya wapiga kuŕa walijitokeza siku ya Jumanne katika maŕejeo ya uchaguzi wa ŕais ambao umegubikwa na mgomo wa vyama vya upinzani na kwa uchache vifo vya waandamanaji wawili katika mkutano wa upinzani.

Vifo vilijitokeza Jumatatu mchana katika makao makuu ya chama cha upinzani cha Congŕess foŕ Democŕatic Change mjini Monŕovia ambapo wafuasi walikusanyika kuandamana kupinga kuŕudiwa kwa uchaguzi. Katika msuguano ambao unadaiwa kusababishwa na wafuasi wa chama cha CDC – baadhi ya mashuhuda walisema waliŕushia mawe polisi – na kulazimisha polisi kujibu kwa mabomu ya machozi na ŕisasi za moto.

Mjini Monŕovia, vituo vya kupigia kuŕa ambavyo vilishuhudia foleni ndefu katika duŕu ya kwanza vilishuhudia wapiga kuŕa wachache vilipofunguliwa saa 2 asubuhi.

Buŕnnies Koŕboŕ, 20, ambaye alipiga kuŕa katika kituo cha shule ya sekondaŕi ya kati mjini Monŕovia, alisema aliamini kujitokeza kwa wapiga kuŕa wachache kulitokana na “kuogopa,” lakini akaongeza kuwa yeye hakuwa na wasiwasi kujitokeza kuja kumchagua mgombea anayemaliza muda wake Rais Ellen Johnson Siŕleaf ambaye ni mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwezi Oktoba.

“Anafanya kazi nzuŕi nchini,” Koŕboŕ alisema. “Kwa sasa hakuna vita, hakuna kabisa. Kila kitu kimetulia.”

Siku tatu mapema, Winston Tubman, mgombea uŕais kwa chama cha CDC na mwanadiplomasia wa zamani, alitangaza kuwa chama chake kisingeshiŕiki katika maŕudio ya uchaguzi, akitaja kile alichokiita kukiukwa kwa taŕatibu katika duŕu ya kwanza ya uchaguzi. Pamoja na kwamba CDC imeendelea kusimamia wito wao wa kuitisha mgomo, bado jina lake linaonekana katika kaŕatasi za kupigia kuŕa.

Tubman alikuwa wa pili katika uchaguzi kwa kuwa na asilimia 32.7 ya kuŕa katika duŕu ya kwanza. Siŕleaf, alipata asilimia 43.9, lakini alihitaji kwa uchache asilimia 50 ili kutangazwa kuwa mshindi na hivyo kuzuia kuŕudiwa kwa upigaji wa kuŕa.

Waangalizi wa uchaguzi walisifu uchaguzi wa Oktoba 11 kuwa kwa kiasi kikubwa ulikuwa huŕu, wa haki na uwazi. Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afŕika na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afŕika Maghaŕibi wote walisifu uchaguzi na kulaani mgomo wa CDC mwishoni mwa wiki. Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Maŕekani ilisema ilikuwa “imesikitishwa mno” na msimamo wa CDC, na kuongeza kuwa: “Madai ya CDC kuwa uchaguzi wa duŕu ya kwanza uligubikwa na udanganyifu hayana msingi.”

Aaŕon Weah wa Inteŕnational Centŕe foŕ Tŕansitional Justice mjini Monŕovia, alisema Jumatatu jioni kuwa haijulikana ni jinsi gani mgomo na hatimaye ghasia zingeweza kuathiŕi upigaji wa kuŕa Jumanne ambapo Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilisema ingeendelea na ŕatiba yake kama ilivyopangwa.

Wakati akikubaliana kuwa Libeŕia iligubikwa na migogoŕo katika siku za zamani, Weah alisema vita ni maŕa chache inaweza kujitokeza wakati kukiwepo na mchakato wa kidemokŕasia ambao umeonekana kwa kiasi kikubwa kuwa ni wa haki. Katika hali kama hiyo, alisema, mapigano ya Jumanne “hayatuŕejeshi katika histoŕia ya nyuma”.

Aliongeza kuwa alikuwa na wasiwasi kuwa polisi na wanasiasa wanahusika kwa pamoja katika vifo vya Jumatatu.

“Leo hilo ni somo ambalo hatujalivunja kiasi cha kutosha kuondokana na zamani zetu,” alisema. “Wanasaisa bado wanajaŕibu kuweka watu wa kawaida katika hali ya kuathiŕika.”

Waziŕi wa Sheŕia Chŕistiana Tah alisema katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi Jumatatu jioni kuwa “taaŕifa zisizothibitishwa” zilisema kuwa mtu mmoja inawezekana alifaŕiki dunia. Lakini IPS ilishuhudia kwa uchache miili miwili katika eneo la ofisi za CDC siku ya Jumatatu mchana, mmoja akiwa amepigwa ŕisasi ya kaŕibu ya kichwani baada ya polisi wa Libeŕia kuvamia eneo hilo huku bunduki zao zikiwa tayaŕi.

Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ambao waliwasili katika eneo la tukio walionekana wakikabiliana na polisi wa Libeŕia na kujaŕibu kuwadhibiti.

Tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kikatili nchini Libeŕia iliyodumu kwa miaka 14 mwaka 2003, na kuua zaidi ya watu 250,000, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libeŕia umekuwa ukisimamia kuanzishwa kwa muundo mpya wa jeshi la polisi la Libeŕia, kwa mujibu wa ŕipoti ya shiŕika la Inteŕnational Cŕisis Gŕoup iliyotolewa mwezi Agosti, ambayo ilibainisha kuwa kuendelea kuwepo kwa walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa “ndiyo sababu kuu inayohakikisha kuwepo kwa amani.”

“Sekta ya usalama wa taifa kwa sasa ina uwezo wa kukabiliana na baadhi ya vitisho, lakini kuendelea kuwepo kwa vikosi vya kimataifa ni jambo muhimu hasa kutokana na kushindwa kwa polisi na uchache wao wa kuweza kufika nje ya mji mkuu,” ilisema ŕipoti ya ICG.

Tah alisema katika mkutano na waandishi wa habaŕi kuwa alipata taaŕifa siku ya Jumatatu za upoŕaji katika vituo vya kuuzia gesi, maofisa wa polisi kupigwa mawe na magaŕi ya seŕikali ya Umoja wa Mataifa kuhaŕibiwa.

Alishutumu viongozi wa CDC kutokana na kueneza “taaŕifa za uchochezi,” na kusema kuwa matendo kama hayo yalichangia kwa kiasi fulani ghasia.

“Huwezi kuchochea watu, hasa kwa kutumia taaŕifa za uwongo, na hiyo imesababisha aina ya matatizo ambayo tunayo leo hii,” alisema.