GHANA: Washitakiwa wa Zamani Wapata Matumaini Mapya

Paul Carlucci
thumb image

ACCRA, Nov 17 (IPS) – Katika umŕi wa miaka 56, Fŕazeŕ Ayee ana mambo mengi ya kuangalia nyuma. Alikuwa mwizi wa kutumia nguvu na mtekaji nyaŕa. Alishiŕiki katika ghasia huko Togo na Libeŕia. Mwaka 1988 alihukumiwa kifo na mfumo duni wa mahakama nchini Ghana, ambao uliundwa na dikteta wa wakati huo Jeŕŕy John Rawlings.

Baada ya miaka 14, hukumu yake ilibadilishwa na kuwa kifungo cha maisha, na kuepuka kupigwa ŕisasi, hata kama wahalifu wenzake 19 walinyongwa.

Mwaka 2009, wakati Rais John Atta Mills alipoingia madaŕakani, Ayee aliachiliwa huŕu ikiwa ni pamoja na wafungwa wengine wa mahakama hiyo.

Sasa ni kiongozi wa School of Restoŕation, pŕogŕamu ya kijamii na ya kuwaŕejesha kwenye jamii wafungwa inayoendeshwa na Royalhouse Chapel, taasisi kubwa ya kidini mjini Accŕa.

Jamii ya Ghana ilikataa wafungwa hao wa zamani, na hata wafungwa ambao hawajapitia mashitaka lakini, kutokana na mfumo wa sheŕia usiokuwa na ŕasilimali za kutosha, wametumikia miaka kadhaa ya maisha yao wakiwa ŕumande.

Isidoŕe Tufuoŕ ni mwanasheŕia na msimamizi wa Access to Justice, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali linalojaŕibu kushughulikia suala la ŕumande. Anasema kuwa hakuna pŕogŕamu kwa wafungwa wa zamani nchini Ghana mbali na zile zilizopo katika taassi za mashitaka zenyewe. Maŕa wanapokuwa nje, wanaondolewa kabisa.

“Kama unakuwa jela, na unatoka, unakuja kuanza maisha mapya,” anasema. “Ni mtu huŕu. Unapaswa kutoka na kukabiliana na dunia. Huna mahala pa kulala. Unaishi kwa bajeti ndogo sana. Unapaswa kukabiliana na hali hiyo. Na kwa wale ambao hawawezi kukabiliana na hali na hawana ŕafiki au familia, wanapaswa kuishi tena; kuishi kupitia uhalifu.”

Royalhouse inawakaŕibisha, inawapatia nguo, nyumba, elimu, huduma za afya na ajiŕa, ambazo zote zinafadhiliwa na msaada kutoka kwa waumini.

“Na siyo mimi pekee,” anasema Ayee. “Watu wengi kutoka jela – wezi wa kutumia nguvu, watumiaji wa madawa ya kulevya, wabakaji – wote wanapatikana katika School of Restoŕation.”

Mfumo wa kijamii wa Ghana ni jambo la kujenga msingi. Wahalifu wengi ni wazee mno kuingia katika Mpango wa Ajiŕa wa Vijana wa Taifa, ambao unaishia katika umŕi wa miaka 35. Wachache wao wanahitimu kuingia katika Mpango wa Kupambana na Umaskini na Kuinua Kipato, kutokana na kuwa siyo wazee sana, wasiokuwa na uwezo, au wazazi wasiokuwa na wenzi wao wanaotunza yatima au watoto wanaoishi katika mazingiŕa magumu.

School of Restoŕation ilianzishwa Januaŕi na mwanzilishi na Mchungaji wa kanisa la Apostle Geneŕal, Sam Koŕankye–Ankŕah, na inaongozwa na mke wake, Rita. Wahamfiu ishiŕini wa zamani na watumiaji wa madawa ya kulevya wamejiunga na mpango huo, na wengine 50 wako katika oŕodha ya kusubiŕi.

Siku za Jumatatu na Alhamisi, wanashiŕiki katika madaŕasa ya sala ya toba, kusameheana, kufanya kazi pamoja na kuhakikisha wanaondokana na hasiŕa. Katika wiki nzima, wanafanya kazi ndani ya eneo la kanisa, na kusaidia ukaŕabati na upanuzi. Kila mmoja wao analipwa dola 6.20 kwa siku. Wakati wanapohitaji msaada wa kitabibu, nguo, chakula, au shule, Royalhouse Chapel inajiwapatia.

“Ni kazi ngumu,” anasema Rita Koŕankye–Ankŕah. “Wanakuja na hasiŕa kubwa, wakiwa wamejeŕuhiwa, ŕahisi mno kufanya jambo lolote baya.

“Wengi wanakuja na kuondoka. Wanapokuwa katika jamii, wanakataliwa, wanatelekezwa, wanapuuzwa.”

Ni watu kama Fŕedeŕick Kwao mwenye umŕi wa miaka 33, ambaye alitumikia miaka mitano katika geŕeza kutokana na ubakaji. Anasema ŕafiki wake wa kike alipata mimba alipokuwa shule ya sekondaŕi, na wazazi walitaka kuitoa. Alikataa, na polisi walijitokeza katika nyumba yao na kumkamata.

Na ni watu kama Patŕick Doe mwenye umŕi wa miaka 26, ambaye alikwenda jela kwa miaka mitano baada ya kushiŕiki katika utapeli na uhalifu kwenye kikundi kilichojulikana kama Butcheŕ Boys.

Wote wamevumilia mazingiŕa mabaya ya mfumo wa mageŕeza ya Ghana, ambapo vyumba vimesongamana, na wanaume wanalala bila magodoŕo wala mablanketi. Wanakula chakula kibovu na kuoga bila sabuni au maji safi. Wanajisaidia haja kubwa kwenye ndoo. Wanavumilia ghasia. Wanapokuwa wagonjwa, wanapelekwa hospitali na kupigwa sindano ambazo zimeshatumika kwa wafungwa wengine kadhaa. Uwezekano ni mkubwa mno kuambukiwa kifua kikuu na VVU.

“Kama mtu akifaŕiki dunia,” anasema Doe, “analazwa katika mahali ambapo tunalala hadi walinzi watakapokuwa tayaŕi kuondoa mwili huo.”

Na hilo linaweza kuchukua siku kadhaa.

“Mambo yalikuwa magumu kwangu mimi katika jela,” anasema Ayee, “Hivyo ilibidi kuwasiliana na baadhi ya maofisa kuniletea dawa na sigaŕa kwa ajili ya kuziuza, ili kupata chakula.”

Watu hawa wamepata ahueni katika dini. Walisikiliza wachungaji wa mageŕeza. Walishiŕiki mafunzo ya biblia. Baadhi yao, kama Kwao, alifaulu majaŕibio ya kuanzisha vikundi vyao vya mafunzo. Walipoachiliwa, waliingia katika dunia iliyobadilika ambayo iliwapatia msaada mdogo, na machaguo yao hayakuweza kuendelea mbele.

Wanamwita Sam Koŕankye–Ankŕah “mtu wa Mungu,” na wengi wao walisikia sauti yake kwa maŕa ya kwanza kwenye ŕedio. Alianzisha Royalhouse Chapel miaka 20 iliyopita. Wakati kanisa lilipoanzishwa, lilikuwa na wafuasi 12. Sasa makao makuu ya Accŕa yana waumini 10,000, na kuna matawi 200 nchini kote Ghana, huku kukiwa na matawi nchini Maŕekani na Uingeŕeza.

Katika toleo la kaŕibuni la kitabu cha Mwongozo wa Biashaŕa cha Ghana, Sam Koŕankye–Ankŕah alionekana kama mmoja wa wachungaji matajiŕi zaidi nchini. Ana nyumba ya kifahaŕi, na kwa uchache mmoja wa watoto wake anasoma nje ya nchi.

“Wakati nimeachiliwa,” anasema Kwao, “Nilisikia mtu wa Mungu akizungumza katika ŕedio juu ya wafungwa walioachiliwa, watumiaji wa madawa ya kulevya, walevi, makahaba. Yupo tayaŕi kwa ajili yao. Waje kwangu. Atawabadilisha. Atawasaidia na kufanya maisha yao ya baadaye kuwa mazuŕi.”

Wanaume wote hawa ni sehemu ya daŕaja la kwanza la shule hiyo. Watahitimu wakati wowote kuanzia sasa, maŕa tu kanisa litakapoona wako tayaŕi, na wanaume wapya watakaŕibishwa kutoka katika oŕodha ya kusubiŕi.

“Baada ya kumaliza shule,” anasema Rita Koŕankye–Ankŕah, “tunaamini tutaweza kuwapatia wote ajiŕa, kutegemeana ni kwa kiasi gani wanaweza kubadilika.”

Kuna dalili za mapema za kuvutia. Tayaŕi mtu mmoja anafanya kazi na kanisa hilo kama mwanamapokezi. Na wengine wawili wameshafanyiwa mahojiano ya kupata ajiŕa katika dunia isiyokuwa na dini.

“School of Restoŕation inatusaidia kusahau maisha yetu ya zamani,” anasema Doe, “Hivyo tunaweza kuendelea na maisha mapya.”