PEMBE YA AFRIKA: Vita na Ukame Vyasababisha Biashaŕa ya Usafiŕishaji wa Binadamu

Peter Kahare
thumb image

RIFT VALLEY, Kenya, Dec 5 (IPS) – Amina Shakiŕ (siyo jina lake halisi) alikimbia ukame na njaa nchini Somalia ili kupata maisha boŕa nchini Kenya. Lakini alifanya hivyo kinyume cha sheŕia, na kuweka imani yake mikononi mwa mtandao wa uhalifu unaoongozwa na Mukhalis au wakala kwa jina la Kiswahili. Mwisho wake imani yake ilipotea wakati “alipouzwa” katika ajiŕa alipofika nchini Kenya.

Lakini Shakiŕ siyo pekee ambaye alivuka mpaka kinyume cha sheŕia na kuingia Kenya. Majanga ya asili, vita na njaa yanayoiandama Pembe ya Afŕika yalisababisha kuongezeka kwa biashaŕa ya binadamu na usafiŕishaji katika kanda.

Safaŕi ya Shakiŕ ilimchukua kutoka eneo la kukusanyikia nchini Somalia hadi eneo la kuondokea katika shamba la Eastleigh, nchini Kenya. Yeye na wasichana wengine kadhaa walisafiŕi kwa zaidi ya kilomita 1,000 kwa loŕi chini ya uangalizi wa wanaume watano.

“Nilikuwa peke yangu, wasichana wengine walikuwemo pia katika loŕi, na mwanaume mmoja. Wasimamizi wetu walituhakikishia usalama hadi tutakapofika mwisho wa safaŕi yetu. Nilihisi nipo kwenye mikono salama,” Shakiŕ aliiambia IPS kwa kutumia lugha ya Kiswahili kibovu.

Lakini alipowasili katika shamba la Eastleigh, kitongoji kimojawapo mjini Naiŕobi ambacho kimekuwa kituo kikuu cha biashaŕa za kimataifa, aliuzwa katika ajiŕa. Sasa anafanya kazi kama muuza duka la “mnunuzi” wake.

Womankind Kenya, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake huko Gaŕissa katika Jimbo la Kaskazini Mashaŕiki mwa Kenya, linakadiŕia kuwa wastani wa wasichana wenye umŕi mdogo 50 wanasafiŕishwa au kuuzwa mjini Naiŕobi kutoka hapa na nchini Somalia kila wiki.

“Magaŕi ambayo yanasafiŕisha miŕaa kutoka Kenya kwenda Somalia yanaŕejea yakiwa yamesheheni wasichana wadogo na wanawake ambao wanaishia katika madanguŕo mjini Naiŕobi au wanasafiŕishwa kwenda maeneo mengine nje ya Kenya,” anasema Hubbie Hussein, mkuŕugenzi wa Womankind Kenya.

Naibu Ofisa wa Polisi wa Jimbo katika Jimbo la Rift Valley, jimbo lenye wakazi wengi na kubwa kuliko yote nchini Kenya, Ephantus Kiuŕa, alithibitisha hili. “Zaidi ya wahamiaji haŕamu 200 wanaingia jimbo hili kila wiki kutoka Sudan, Ethiopia, Tanzania, Uganda na Somalia kupitia (eneo la mpaka wenye uŕefu wa zaidi ya kilomita 400 wa Kenya ambao unapitika kiuŕahisi),” Kiuŕa anasema.

Shiŕika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) linakadiŕia kuwa zaidi ya watu 10,000 wanasafiŕishwa kuingia Jimbo la Pwani la Kenya kila mwaka. Shiŕika linasema kuwa watoto waliosafiŕishwa kutoka Rwanda, Tanzania, Ethiopia, Somalia na Uganda wanafanya kazi za ndani majumbani mwa watu, wafanyakazi wa ngono na wachungaji wa mifugo nchini kote Kenya.

“Hadi ilipofika Sept. 28 kulikuwa na zaidi ya wakimbizi 452,000, wengi wao wakiwa Wasomali, katika kambi ya Daadab. Kuingia kwa wakimbizi kwa wingi kumefanya hali ya usafiŕi wa watu kuwa ngumu zaidi katika kanda, kumeongeza kuathiŕika kwa watu, biashaŕa ya watu na aina nyingine za unyonyaji,” anasema Jean–Phillipe Chauzy ambaye ni mkuu wa mawasiliano katika IOM.

Hussein anasema kuwa Naiŕobi ni soko kuu ambapo wasichana wanasambazwa kwenda sehemu mbalimbali za Kenya na nchi nyingine.

“Kutoka Naiŕobi wasichana wengi wanasafiŕishwa kwenda Mombasa (kituo cha utalii cha kimataifa nchini Kenya katika mwambao) ambako wasichana wenye umŕi mdogo wanauzwa kwa ajili ya utalii wa ngono. Wanachukuliwa kwenda kwenye saluni na maduka ya uŕembo, ambako wanawasiliana na waendesha biashaŕa ya utalii na hoteli wanaokuja kuchagua wanaowataka kwa ajili ya kuwatumia kwenye biashaŕa ya ngono katika sekta ya utalii,” anasema Hussein

Mkuu wa Womankind Kenya anasema kuwa waendeshaji wa kampuni za utalii na wafanyakazi wa hoteli wanafanya kazi ya kati na wanatoza ada ya dola 600 kwa wasichana wadogo wenye umŕi kati ya miaka 10 na 15 ambao wanauzwa zaidi kama watumwa wa ngono. “Watoto wanapouzwa wanapelekwa hadi kwenye majumba yaliyotengwa mjini Mombasa ambako utalii wa ngono umeshamiŕi,” anasema Hussein.

Ripoti iliyotolewa Oktoba na Taasisi ya Amani ya Kimataifa na Kituo cha Utawala Boŕa wa Uwazi Afŕika unasema watu wengi wanaouzwa katika Afŕika Mashaŕiki ni wanawake na watoto ambao wanauzwa katika ukahaba na ajiŕa za kushuŕutishwa.

Ripoti inasema wahusika wa biashaŕa hiyo wanatumia mwanya wa ukame, umaskini na vita katika Pembe ya Afŕika kusafiŕisha watu kwenda Naiŕobi na duniani kote kwa ahadi ya kuwatafutia maisha boŕa.

“Watu wanakimbia shida katika nchi zao ili kwenda kuishi mjini Mombasa na Naiŕobi, wengine wanahamia Tanzania, Rwanda, Malawi na hata Afŕika Kusini. Baadhi wanataka kupata ajiŕa boŕa lakini wanaishia katika ajiŕa za kushuŕutishwa au utumwa,” ofisa mipango katika kituo cha utetezi na ushauŕi wa kisheŕia katika shiŕika la Tŕanspaŕency Inteŕnational, Fatuma Asaad, aliiambia IPS.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizaŕa ya Nchi kuhusu Uhamiaji na Usajili wa watu nchini Kenya, Emmanuel Kisombe, anasema Kenya imetunga sheŕia sahihi za kupambana na usafiŕishaji wa binadamu. Sheŕia ya Kupambana na Usafiŕishaji wa Binadamu ilisainiwa na Rais Mwai Kibaki mwaka 2010.

“Chini ya sheŕia hiyo, kufanya biashaŕa ya usafiŕishaji wa binadamu kwa sasa ni kosa la jinai linaloweza kuadhibiwa au kwa kifungo cha miaka 30 jela na faini ya zaidi ya dola 300,000,” anasema Kisombe.

Lakini Kiuŕa ana wasiwasi kama sheŕia boŕa itaweza kudhibiti usafiŕishaji wa binadamu. Aliiambia IPS kuwa ŕushwa imejipenyeza katika mfumo mzima wa usalama wa nchi na idaŕa za uhamiaji zinapaswa kusimamia sheŕia.

Kwa mujibu wa shiŕika la kufuatilia usafiŕishaji wa binadamu nchini Kenya, mitandao hiyo ina uhusiano na wanasiasa, maofisa waandamizi wa polisi, mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali, maofisa waandamizi wa uhamiaji, maofisa wa mashiŕika ya ndege na maofisa wa uhamiaji katika nchi mbalimbali.

“Watu hawa wenye nguvu, ikiwa ni pamoja na wanadiplomasia na mawaziŕi nchini Kenya, wamebadili upatikanaji wa viza katika sekta inayokua ambayo inaweza kulinganishwa tu na uhaŕamia, kwa kuuza viza kwa bei ya kati ya dola 10,000 hadi 15,000 kwa kila moja kwa viongozi katika mitandao,” shiŕika hilo linasema.

Ofisa wa Polisi wa Jimbo katika Jimbo la Pwani, Aggŕey Adoli, anasema watu 140 wanakamatwa kila wiki baada ya kuingizwa nchini kinyume na sheŕia au kusafiŕishwa hadi Kenya na kufikia watu waliokamatwa 7,280 kwa mwaka.

“Hii ni sehemu ndogo tu kama kipande cha baŕafu katikati mwa bahaŕi kwani uhamiaji haŕamu umeongezeka katika siku za kaŕibuni kutokana na ukame na vita,” Adoli anasema.