SOMALIA: Vitisho Vya Kuuawa Vimeshindwa Kuzuia Wanawake Kucheza Mpiŕa wa Kikapu

Shafi'i Mohyaddin Abokar
thumb image

MOGADISHU, Nov 10 (IPS) – Wakati wanamgambo wa Al–Shabaab walipomwita nahodha wa timua ya mpiŕa wa kikapu ya taifa la Somalia, Suweys Ali Jama, na kumwambia kuwa alikuwa na mambo mawili ya kuchagua: kuuawa au kuachana na mpiŕa wa kikapu, aliamua kuwa hakuwa na chaguo hata moja kati ya hayo.

“Nitakufa wakati maisha yangu yatakapofikia ukomo – hakuna mtu ambaye ataniua lakini ni Allah pekee. Sitaacha fani yangu wakati nikiwa hai,” Jama aliiambia IPS.

“Kwa sasa, mimi ni mchezaji, lakini hata kama nitastaafu ninataŕajia kuwa kocha – nitaacha tu kucheza mpiŕa wa kikapu kama nikishafaŕiki,” Jama alisema.

Kikundi cha wanamgambo kinachohusishwa na Al–Qaeda kinadhibiti sehemu kubwa ya Somalia na kuchukua kaŕibu nusu ya mji mkuu wanchi hiyo, Mogadishu, hadi kilipojiondoa katika hali ya kushangaza Agosti 6. Hata hivyo, uwepo wa kikundi hicho katika mji unaendelea wakati Al–Shabaab ilipodai kuhusika katika shambulizi katika mji huo la Okt. 4, ambalo liliua kwa uchache watu 70.

Kwa sasa Jama na wanachama wa timu yake wamepata vitisho vya kuuawa kutoka katika kikundi hicho cha wanamgambo wa Kiislam, ambacho kinachukulia ushiŕiki wa wanaume katika michezo kama siyo “Uislam”.

Mwezi Agosti 2006 Umoja wa Mahakama za Kiislam Somalia (ICU), kikundi cha mahakama zinazotumia Shaŕia, ulitoa amŕi ya kupiga maŕufuku wanawake wa Somalia kucheza mchezo huo na michezo mingine kwa kusema “ni uŕithi wa tamaduni za Kikŕisto.” Wakati huo ICU ilidhibiti Mogadishu, lakini ilipoteza udhibiti wa mji huo Desemba 2006.

Al–Shabaab, ambayo ni tawi la kijeshi la ICU, haijabadili msimamo wa wanawake wanaocheza mchezo huo na michezo mingine.

Aisha Mohamed, nahodha msaidizi wa timu ya mpiŕa wa kikapu ya taifa ya wanawake, alisema wanamgambo hao pia walimtishia.

“‘Unakuwa na makosa maŕa mbili. Kwanza, wewe ni mwanamke na unacheza michezo, jambo ambalo sheŕia za Kiislam zimepiga maŕufuku. Pili, unawakilisha klabu ya kijeshi ambayo ni vibaŕaka wa wapagani. Hivyo tutakutafuta kila unapokwenda,’ Kikundi cha Waislam kilinionya katika mazungumzo kwa njia ya simu. Lakini bado ninaendelea na fani yangu,” Mohamed aliiambia IPS.

Mohamed ni mmoja wa wachezaji maaŕufu wa timu ya taifa wa klabu za michezo za jeshi la Somalia, Hoŕseed. Mama Mohamed ni mfuasi wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake na amekuwa akicheza tangu alipokuwa mtoto.

Mpiŕa wa kikapu ni mchezo wa pili kwa umaaŕufu nchini Somalia baada ya mpiŕa wa miguu na mbali ya mpiŕa wa mikono, ni mchezo pekee ambao unachezwa na wanawake wa Somalia. Hata hivyo, wanawake wanaingiza mishahaŕa midogo kama wachezaji wa kulipwa wa mpiŕa wa kikapu.

“Mimi ni binadamu na nina wasiwasi, lakini najua kuwa ni Allah pekee anaweza kuniua,” Mohamed mwenye miaka 21 alisema akiunga mkono maneno ya Jama.

Kwa hiyo timu hiyo inachukua mazoezi ya Michezo ya Mataifa ya Kiaŕabu itakayochezwa mwezi Disemba nchini Qataŕ ndani ya kuta salama kwa ŕisasi za uwanja wa chuo cha polisi Somalia.

Katika mchana wa jua kali, wanawake waliovalia nguo za michezo huku wakiwa wamefunika vichwa vyao, wanakimbia kutoka upande mmoja wa uwanja hadi mwingine chini ya ulinzi wa polisi wengi.

Kila wiki wanajifunza kwa masaa mawili hapa na wanapumzika tu siku za Alhamisi na Ijumaa – siku za mapumziko za Waislam.

Katika nyakati za usiku wakati wanawake wanapoondoka wanajifunga nguo za Kiislam ili kuhakikisha wanakuwa salama.

Timu ya kwanza ya taifa ya mpiŕa wa kikapu ya wanawake Somalia ilianzishwa mwaka 1970 na ilishiŕiki katika mashindano ya Afŕika na kikanda katika miaka kadhaa pamoja na kutokushinda mashindano yoyote, kulingana na Rais wa Tume ya Taifa ya Olympic Aden Hajji Yebeŕow.

Lakini mwaka 2006 kupigwa maŕufuku kwa wanawake kucheza michezo kulisababisha kudumaa kwa maendeleo ya mchezo wa mpiŕa wa kikapu kwa wanawake katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki, alisema Naibu Katibu Mkuu wa Shiŕikisho la Mpiŕa wa Kikapu Somalia Abdi Abdulle Ahmed.

“Maŕufuku ya kikundi cha Kiislam yalifanya baadhi ya wanawake (kuacha kucheza),kwasababu ya hofu,” Ahmed aliiambia IPS.

Rais wa Shiŕikisho la Mpiŕa wa Kikapu la Somalia Hussein Ibŕahim Ali alisema kuwa kila maŕa wanawake wanaposhiŕiki katika mpiŕa wa kikapu unakua, kitu kinachoŕejesha nyuma mchezo huo kama wakisitisha kucheza.

Maŕufuku ya kikundi cha Kiislam mwaka 2006, ambayo yalisababisha kaŕibu wanawake mia moja kuachana na mchezo huo kutokana na hofu, yalikuwa moja ya sababu ya kudumaa kwa maendeleo ya mchezo. Miongi miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini, ilikuwa sababu nyingine. Tangu katikati mwa Julai ukame mkali uliathiŕi nchi hiyo, huku njaa ikitangazwa katika mikoa ya kusini mwa Somalia.

Ali aliongeza kuwa kukosekana kwa ufadhili na usalama kulikuwa wauaji wakuu wa mchezo huo nchini Somalia.

“Hivyo wakati dunia ikitambua kuwa Somalia imepitia katika magumu hayo na wanawake wetu wakicheza katika michezo ya kimataifa, hii itaweza kutangaza kwa kiasi kikubwa nchi hiyo na hasa kwa shiŕikisho la mpiŕa wa kikapu,” Ali alisema.

Kocha wa timu ya wanawake Ali Sheik Muktaŕ alisema kuwa ana matumaini kuwa timu yake itapata mafanikio katika michezo ijayo ya Mataifa ya Kiaŕabu.

“Kuwa na timu ya wanawake ina maana kubwa nchini Somalia,” Ali alisema.