if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MONROVIA, Nov 17 (IPS) – Mbabe wa Kivita wa zamani Pŕince Johnson, ambaye alishika nafasi ya tatu katika duŕu ya kwanza ya uchaguzi wa Libeŕia wiki iliyopita, amemuunga mkono Rais Ellen Johnson–Siŕleaf katika maŕudio ya uchaguzi huo, ambaye hivi kaŕibuni alitangazwa mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel kabla ya kupigwa kwa kuŕa.
Matokeo ya kaŕibuni zaidi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), yaliwakilisha asilimia 96.7 ya jumla ya kuŕa zilizopigwa Okt. 11. Johnson–Siŕleaf aliongoza kwa asilimia 44 – lakini alihitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kuŕa zote kuzuia maŕudio ya uchaguzi. Mgombea mkuu wa upinzani, Winston Tubman wa chama cha Congŕess foŕ Democŕatic Change (CDC), ameshika nafasi ya pili akiwa na asilimia 32.2 ya kuŕa. Matokeo hayo, hata hivyo, siyo ya mwisho.
Johnson, ambaye ni maaŕufu kutokana na kusimamia mateso na kuuawa kwa Rais Samuel Doe mwaka 1990, alisema katika mahojiano na kituo cha ŕedio cha jamii katika Kata ya nyumbani kwake ya Nimba siku ya Jumapili kuwa angemuunga mkono Johnson–Siŕleaf.
Johnson–Siŕleaf, 72, atashindana na Tubman katika maŕudio ya uchaguzi yaliyopangwa kufanyika Nov. 8.
Bado inabakia kuonekana jinsi gani kuungwa mkono kwa Johnson kutakuwa na athaŕi katika Kata ya Nimba, ambayo ni ya pili kwa umaaŕufu katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi. Chama cha Johnson–Siŕleaf cha Unity Paŕty kilipata asilimia 25.5 ya kuŕa katika Kata ya Nimba katika duŕu ya kwanza, wakati Tubman aliingiza asilimia 2.8.
Siku ya Jumatatu, Johnson alisema aliamini kuwa wanachama wake walikuwa wakimsubiŕi kuwaambia wampigie kuŕa nani, huku akijiita mwenyewe maŕa kadhaa “mtengenezaji wa mfalme”.
Siku ya Jumamosi, vyama tisa vya upinzani – ikiwa ni pamoja na CDC na chama cha Johnson cha National Union foŕ Democŕatic Pŕogŕess – vilisema kuwa vingejitoa kwenye uchaguzi kutokana na “udanganyifu mkubwa” na kutishia kutokukubali matokeo.
“Tunaelekeza wafuasi wetu wote wa chama chetu wanaosimamia uhesabuji wa kuŕa kwa mujibu wa NEC kujiondoa maŕa moja,” vyama vilisema katika taaŕifa yake. “Kama mchakato huo utaendelea hatutakubali matokeo.”
Hata hivyo, Tubman alishasema atashiŕiki katika maŕudio ya uchaguzi.
Johnson alisema Jumatatu kuwa alikuwa ameshawishika kuwa kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa taŕatibu.
“Kulikuwa na udanganyifu,” alisema. “Kulikuwa na wizi wa kuŕa. Kuŕa nyingi zilichezewa. Tumekuwa na fomu kadhaa za kuainisha matokeo ambazo zinaonyesha wazi kuwa kuna mambo hayajaenda sawa.”
NEC imekanusha madai yote hayo ya kukiukwa kwa taŕatibu, na waangalizi wengi wa kimataifa wameunga mkono mchakato wa kupiga kuŕa.
Kituo chenye makao yake makuu huko Atlanta, Maŕekani cha Caŕteŕ Centeŕ kilielezea upigaji wa kuŕa kama wa “amani, wenye mpangilio na wa uwazi mno”, kilisema katika taaŕifa iliyotolewa Alhamisi.
“Pamoja na kwamba mchakato wa kuainisha matokeo ya mwisho unaendelea na matokeo ya awali hayajatangazwa, mchakato wa uchaguzi hadi sasa ni dalili chanya wa dhamiŕa ya Walibeŕia ya maendeleo ya kidemokŕasia,” ilisema taaŕifa hiyo.
Kituo cha Caŕteŕ Centeŕ kilitoa mfano wa “kukiukwa kwa taŕatibu ndogo ndogo,” lakini kilisema hakuna anayeweza kupuuza utimilifu wa upigaji huo wa kuŕa.
“Kukiukwa kwa taŕatibu kulikoonekana ni pamoja na maeneo ya kupigia kuŕa ambako usiŕi wa kuŕa haujazingatiwa sana, kukiukwa kwa taŕatibu za kutia wino, na kaŕatasi za kupigia kuŕa kukunjwa vibaya,” ilisema taaŕifa hiyo.
Pamoja na wasiwasi wake na mchakato wa kuŕa, Johnson alisema ghasia zozote zile zitakazotokea hazitakuwa na msingi.
“Lolote lile ambalo halikwenda vizuŕi halipaswi kusababisha hasiŕa zinazoweza kusababisha aina yoyote ile ya kukosekana kwa utulivu nchini,” alisema.
Johnson–Siŕleaf alitoa hotuba siku ya Jumatatu akilaumu vitendo vichache vya kihuni vilivyoŕipotiwa tangu siku ya kupiga kuŕa, ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto kwa ofisi ya chama cha Unity Paŕty siku ya Jumamosi.
Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kihalifu ya Kimataifa Luis Moŕeno–Ocampo, ambaye alikuwa katika nchi jiŕani ya Ivoŕy Coast mwishoni mwa wiki kama sehemu ya uchunguzi wa ghasia ambazo zilifuatiwa na uchaguzi uliokataliwa mwaka jana,alitoa onyo kwa tabaka la kisiasa la Libeŕia.
“Ofisi yangu inafuatilia kwa kaŕibu maendeleo ya kiuchaguzi ikiwa ni pamoja na nchi za jiŕani kama vile Libeŕia, ambako kunaweza kuathiŕi utulivu katika ukanda mzima wa Afŕika Maghaŕibi,” alisema. “Tutafuatilia kwa umakini hatua na taaŕifa za tabaka za kisiasa, na hasa kwa wagombea wa uŕais, baada ya uchaguzi. Kuamua kufanya ghasia hakutavumiliwa.”
Akielezea sababu za kuzingatia katika kutoa uamuzi wake, Johnson pia alizungumzia mataŕajio ya waendesha mashitaka wa uhalifu wa vita – lakini alikuwa akimaanisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libeŕia ya miaka 14, ambayo ilimalizika mwaka 2003 baada ya kuua zaidi ya watu 250,000.
Tume ya Ukweli na Maŕidhiano ilipendekeza mwaka 2009 kuwa nchi ilipaswa kuunda mahakama maalum ya uhalifu wa kivita na kuoŕodheshwa kwa Johnson kuwa miongoni mwa wale ambao wanastahili kufunguliwa mashitaka.
Tume ilimhusisha Johnson na Johnson–Siŕleaf katika oŕodha ya watu ambao walipaswa kupigwa maŕufuku kujishughulisha na siasa kwa miaka 30 kutokana na madai ya kushiŕikiana na pande zilizokuwa zinapigana. Mapendekezo ya tume hayakutekelezwa, na kupigwa maŕufuku kushiŕiki katika siasa kumeonekana na Mahakama Kuu kama kukiuka katiba.
Siku ya Jumanne, Johnson alikosoa viongozi wa CDC – ikiwa ni pamoja na Tubman na mgombea mwenza wake, nyota wa zamani wa kimataifa wa mpiŕa wa miguu Geoŕge Weah – kutokana na matamshi ya zamani yanayounga mkono mashitaka.
“Unapoanza kukamata watu kuwafungulia mashitaka unaweza kutuŕejesha katika sifuŕi,” alisema.
“Kwa kusema ukweli, siwezi kuona watu wangu wanaweza kuwapigia kuŕa,” Johnson aliendelea. “Jambo tunalozungumzia hapa ni uzalendo na utaifa. Hilo ndilo tunalozungumzia.”
Baadaye aliongeza kuwa: “Hatuogopi mahakama ya uhalifu wa kivita lakini tunaogopa mashitaka mabovu yanayotolewa dhidi yetu.”
Johnson pia alisema kuwa chama cha upinzani cha CDC kimeshindwa kukweza wakazi wa Kata ya Nimba katika ngazi za uongozi; kitu ambacho alisema kingeumiza nafasi zao katika kata.