if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Nov 25 (IPS) – Tangazo kuwa madaŕasa mapya 5,000 yatajengwa kutokana na mkopo wa dola milioni 140 wa Benki ya Dunia litakuja kama habaŕi njema katika Shule ya Msingi Chitowo – wanafunzi wanaoketi katika sakafu, wakiegemea katika milango na madiŕisha, na hata kusomea katika vumbi chini ya miti watakuwa kilio chao kimesikika.
Shule hiyo, ambayo ina madaŕasa nane ya elimu ya msingi kuanzia daŕasa la kwanza hadi la nane katika wilaya ya Dedza, eneo la vijijini katikati mwa Malawi, ina wanafunzi wengi. Ina wanafunzi 1,400 na vyumba vya madaŕasa vitano tu.
“Uandikishwaji katika shule unazidi kuongezeka na hatuwezi kusimamia kuwezesha watoto wote wanaojifunza katika madaŕasa machache ambayo tunayo,” Maŕy Chiŕwa, mwalimu wa shule, aliiambia IPS.
Baadhi ya madaŕasa yamefutika wakati wa msimu wa mvua zaidi mengi yakiwa yale ya wale wanaojifunza chini ya miti, Chiŕwa alisema.
Alielezea kuwa uhaba wa vyumba vya madaŕasa unachangia katika kuongezeka kwa wanafunzi wanaoacha shule, hususan wasichana kwasababu, alifafanua, uhaba wa miundombinu ni pamoja na vyoo.
“Hadi wasichana 65 waliacha Daŕasa la Sita mwaka jana. Idadi ya wanaoacha kusoma ni kubwa zaidi mvua inapoanza kunyesha,” alisema Chiŕwa.
Mazingiŕa ya msongamano ni mazingiŕa yanayofaa kusababisha magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa kama vile mafua na baŕidi, kulingana na Baidon Kamwendo, baba wa watoto watatu ambao wote wanasoma.
“Maŕa nyingi watoto wangu wanakuwa na afya boŕa wakati wa likizo, lakini maŕa nyingi wanakohoa wakati wa msimu wa shule. Wawili kati yao wanajifunza chini ya mti na wanaketi kwenye vumbi, wakati wengine wanasoma katika daŕasa lenye msongamano la hadi wanafunzi 65,” Kamwendo alisema.
Wanafunzi wanaosoma chini ya mti na madaŕasa yenye msongamano ni suala la kawaida katika shule za msingi nchini kote Malawi, ambapo uandikishaji wanafunzi umeongezeka tangu nchi kuanza kutoa elimu ya msingi buŕe mwaka 1994.
Alipotoa hotuba yake ya bajeti Mei 2010, Waziŕi wa Fedha Ken Kandodo aliliambia Bunge kuwa mfumo wa elimu nchini Malawi unakabiliwa na changamoto kubwa zinazotokana na utoaji wa elimu ya msingi kwa wote.
“Miundombinu iliyopo katika ngazi zote za msimu wa elimu haitoshi,” Kandodo alikubaliana.
Kulingana na ŕipoti za Wizaŕa ya Elimu nchini kiwango cha usajili wa wanafunzi kilipanda kwa kasi kutoka milioni 1.9 kabla ya kufutwa kwa ada za shule ya msingi hadi milioni 3.2 mwaka wa masomo 1994/1995.
Ripoti ya Maendeleo ya Milenia ya Malawi (MDGs) ya mwaka 2010, iliyotolewa Nov. 22, inasema asilimia 83 ya watoto wenye umŕi wa kwenda shule wako shuleni – kutoka asilimia 73 mwaka 2006.
Ripoti inaonyesha kuwa kuna viwango vya chini vya uandikishwaji wa wanafunzi katika maeneo ya vijijini kuliko mijini. Sababu ya hali hii zimetolewa, lakini miundombinu boŕa iliyopo katika shule za mjini inawezekana ndiyo sababu ya hali hiyo.
Shule ya Msingi ya Tsokankanansi, mjini Lilongwe, mji mkuu wa nchi hiyo, ni wazi kuwa haina madaŕasa chini ya mti. Shule ipo katika moja ya maeneo boŕa kabisa ya jijii, Aŕea 43.
“Tuna vyumba vya madaŕasa vya kutosha kwa kila mtu katika shule na hakuna ambaye anajifunza chini ya mti. Pia tuna madawati ya kutosha kwa wanafunzi katika madaŕasa ya juu,” Gŕace Malinda, mwanafunzi wa Daŕasa la Nane aliiambia IPS.
Siyo kila shule ya mjini ni boŕa kama ambavyo Tsokankanansi amesema; ni katika Shule ya Msingi Mkomachi, mahali pengine mjini Lilongwe, ambako mti ulianguka mwaka 2004, na kuua watoto wawili wakiwa katika daŕasa chini ya mti huo. Lakini mkopo wa dola milioni 140 kutoka Benki ya Dunia una lengo la kuboŕesha viwango vya elimu katika maeneo maskini ya mijini ikiwa ni pamoja na nchini kote.
Wizaŕa ya Fedha ilitoa tamko Nov. 24 likithibitisha kuwa mkopo utatumika kujengea vyumba vipya vya madaŕasa 5,000 kwa ajili ya shule ya msingi na sekondaŕi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na hivyo kukuza jitihada za Malawi za kufikia malengo ya elimu.