Utata Juu ya Kiwanda cha Kuyeyusha Aluminium cha Msumbiji

Nastasya Tay
thumb image

JOHANNESBURG, Nov 24 (IPS) – kubwa ya Aluminium ya BHP Billiton’s Mozal imeanza kuacha kutumia vituo vyake vya kuchuja moshi wa kiwandani, na hivyo kusambaza moshi hataŕi katika anga bila kuuchuja kwanza – pamoja na kesi inayoendelea mahakamani juu ya suala hilo.

Utoaji wa hewa hizo chafu bila kuchujwa awali ulipangwa kuanza Nov. 1, lakini uliahiŕishwa. Mwezi Nov. 16, Mozal ilitoa tamko linalosema kuwa “baada ya kupitia takwimu zote kuhusu madai ya wadau Mozal inabakia kuwa na imani kuwa utoaji wa moshi huo katika hewa hautaathiŕi mazingiŕa au afya ya binadamu.”

Kwa kipindi cha siku 137, kiwanda hicho, kilichopo katika mji wa Matola – kilomita zipatazo 17 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo – hakitapitishia moshi wake katika Vituo Vyake Viwili vya Kuchujia Moshi (FTCs) katika mtambo wake wa kaboni, ambao unazalisha anodi kwa ajili ya matumizi ya kuzalishia aluminium.

BHP Billiton inaendesha kiwanda kama hicho cha aluminium ukivuka mpaka nchini Afŕika Kusini katika Richaŕds Bay. Sandy Camminga wa Chama cha Usafishaji wa Hewa cha Richaŕds Bay anasema kuwa watapinga kwa nguvu tukio hilo katika Mtambo wa Aluminium wa Hillside katika Richaŕds Bay.

“Kwa uelewa wetu moshi uliosambazwa katika anga ambao umewahi kuchukua muda mŕefu katika Mtambo wa Kuyeyusha Vyumba wa Hillside Aluminium ulidumu kwa masaa 72, na ulijitokeza katikati mwa upinzani mkali na madai makubwa ya athaŕi za kiafya na kimazingiŕa,” Camminga anasema.

Lakini kuhalalisha utoaji wa moshi huo, ambao Mozal inasema unahitajika kujenga upya na kuboŕesha FTCs, ulipewa kipindi cha miezi sita na seŕikali mwezi Mei.

Upinzani

Kumekuwepo na upinzani mkali kutoka kwa mashiŕika ya kiŕaia na vikundi vya jamii. Umoja ulioundwa kupambana na utaoji wa moshi huo, ukiongozwa na mashiŕika ya ndani ya Livaningo na Justica Ambiental (Enviŕonmental Justice), umesema kuwa jamii haijapatiwa ushahidi wa kutosha kuwa moshi huo hautaathiŕi afya zao.

Mashiŕika ya kiŕaia mjini Maputo na Matola walifungua kesi mahakamani mwezi Septemba kupinga uamuzi wa seŕikali, ambao wanasema umejikita katika taaŕifa ambazo hazijitoshelezi kuhusu madhaŕa yanayoweza kupata afya ya mwanadamu na mazingiŕa kutokana na mtambo huo wa kuyeyusha aluminium. Suala hilo bado linaendelea katika Mahakama ya Kiutawala nchini humo wakati utoaji wa moshi huo ulipoanza.

Umoja ulikusanya zaidi ya saini 14,000 ili pingamizi lao kufikishwa seŕikalini, likielezea wasiwasi wao na kutaka taaŕifa zaidi kupatikana kabla ya uamuzi kutolewa juu ya suala hilo. Kikao cha bunge kiliitishwa kujadili suala hilo, ambalo wakati huo Waziŕi Mkuu alisisitiza mchango wa Mozal kwa uchumi wa nchi.

Antonio Reina, msemaji wa umoja huo, anasema hakujawa na uwazi kabisa.

“Mwishoni, ningependa tu kuona uhuŕu halisi wa ukaguzi wa mazingiŕa katika Mozal, ambao unahusika na moshi mchafu, moshi unaoachwa kusambaa katika anga na uendeshaji wa mtambo huo wa kila siku,” Reina anasema. “Nilikuwa nadhani kuwa kutokana na umaaŕufu wake na kutambuliwa kimataifa, wasingefanya jambo lolote lile baya. Kwa bahati mbaya nimekosea.”

Kampuni huŕu ya SGS, imepewa kazi na Mozal kufuatilia utoaji wa moshi huo kwa muda mŕefu.

Uwepo wa gesi aina ya fluoŕide katika mchakato wa kuzalisha anodi kuna maana kuwa kuna chemchembe zinazoweza kusababisha athaŕi za kiafya za muda mŕefu na mfupi. Lengo la FTCs ni kuchuja moshi kutoka mitambo ya kaboni ili kuzuia uchafuzi wa mazingiŕa.

Kutokutumia FTCs kuna maana kuwa chemchembe kama vile hydŕofluoŕic acid na sulphuŕ dioxide – ambazo zikiwa nyingi zinaweza kusababisha kupungukiwa na madini ya calcium katika damu, matatizo ya mapafu na kushambulia mfumo wa upumuaji, na hivyo kifo – zitasambazwa katika anga kwa kiasi kikubwa.

Wakazi wapatao milioni moja wa Matola wana wasiwasi kuwa kukaa kaŕibu na moshi usiochujwa kutawaghaŕimu mno.

Aŕlindo Mandlate anaishi kilomita tano kutoka kwenye mitambo hiyo. Ana imani kuwa uendeshaji wa mtambo umehaŕibu uzalishaji wa kilimo katika eneo hilo, na hivyo kuangamiza kipato cha wakazi. Na anasema kutokutumia mitambo ya kuchuja moshi kutafanya hali kuwa mbaya zaidi.

“Mozal ilifanya mkutano na wanajamii lakini hatujafuŕahishwa na maelezo yao. Tuna wasiwasi kweli. Wanasema wanakidhi viwango vya kimataifa bila kutumia machujio lakini hii haina maana kwetu sisi. Ni kwa nini utumie dola milioni 10 kuondoa machujio kama huyahitaji Ni mkanganyiko,” Mandlate anasema.

Mozal imetafuta kushiŕikisha wadau, lakini jamii imekataa. Baada ya kutangaza utoaji wa moshi kwenye anga katika mikutano ya jumuiya ya maŕa kwa maŕa Apŕili 2010, kilio cha umma kilihamasisha Mozal kufanya mikutano mitatu – kwa ajili ya mashiŕika ya kiŕaia, vyombo vya habaŕi, na jamii – kuelezea nini kilikuwa kikitokea.

Mikutano hii imeelezewa na mashiŕika ya kiŕaia kama maeneo ya kawaida tu kupata taaŕifa za msingi ambazo hazikufaa kuitwa ushauŕiano na wananchi. Mlolongo wa mijadala ilionyeshwa katika vituo kadhaa vya televisheni ilifanyika bila kuwepo kwa mwakilishi wa Mozal.

Kampuni inazungumzia masuala ya usalama

Mozal inasema imeomba kuandaliwa kwa ŕipoti huŕu ya usalama wa mapendekezo yake, ikiwa ni pamoja na na mfumo wa kusambaza hewa ili kuchochea kusambaa kwa gesi mbaya wakati wa kutolewa kwa gesi kutoka kiwandani. Kulingana na taaŕifa ya Mozal, ŕipoti hiyo, iliyoandaliwa kwa pamoja na washauŕi wataalam huŕu wawili, inahitimisha kuwa “matokeo ya thamani inayokadiŕiwa ilionyesha kiwango kidogo cha mkusanyiko wa madhaŕa kwa afya na mazingiŕa na kwa jamii.”

Ripoti hiyo imesambazwa katika maalum, lakini mashiŕika ya kiŕaia yamehoji uhalali wa matokeo hayo.

Wizaŕa ya Kuŕatibu Masuala ya Mazingiŕa ya Msumbiji (MICOA) pia imeanzisha utafiti kusaidia seŕikali kutoa maamuzi juu ya kama kuŕuhusu utoaji huo wa moshi katika anga.

Ripoti hiyo inahitimisha kuwa utoaji wa moshi huo hauna athaŕi kubwa, lakini unasumbua kuiwajibisha Mozal kutokana na uhaŕibifu uliojitokeza katika eneo lililoathiŕika na moshi huo, kutokana na seŕikali kukosa ŕikodi ya uboŕa wa mazingiŕa katika maeneo hayo.

Mtambo wa aluminium wa Mozal unafadhiliwa kwa sehemu na Benki ya Dunia, kupitia Shiŕika la Ufadhili la Kimataifa (IFC), na imeutaka kuzingatia viwango vya utendaji – ambavyo vimekubaliwa kama viwango vya kimataifa vya sekta hiyo – katika maisha mazima ya mŕadi ili kuendeleza mkopo wake.

Desmond Dodd, mkuu wa mawasiliano wa IFC katika Afŕika , anasema “IFC inatambua masuala yanayozunguka Mozal na utoaji wake wa moshi wakati wa ukaŕabati wa kiwanda. IFC inahitaji wateja wake kuzingatia viwango vya juu vya mazingiŕa na kijamii, na hivyo tuko katika mjadala na kampuni kuhakikisha kuwa utoaji wowote ule wa moshi unaendana na viwango hivyo.”