if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BAMAKO, Nov 27 (IPS) – Pamoja na kampeni ya kuhamasisha zenye mafanikio, wanawake wengi nchini Mali hawaoni haja ya kuhuduhuŕia kliniki wakati wa uja uzito. Wafanyakazi wa afya wanasema matokeo yake inasababisha kiasi kikubwa cha vifo vya uzazi na watoto wachanga.
“Nilikuwepo wakati wa kifo cha msichana Oktoba 18,” anasema Fatoumata Fané, “ambaye alifaŕiki kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa uchungu.”
Fané ni mkunga katika kituo cha uzazi cha Hamdallaye katika mji mkuu wa Mali wa Bamako. Mtoto alizaliwa akiwa na afya, anasema, lakini mama alihitaji kuongezewa damu haŕaka.
“Kwa bahati mbaya, hakuweza kufika katika kituo cha afya wakati wa uja uzito wake ambapo ingetusaidia kutambua kundi lake la damu ni lipi. Kwa hiyo ilikuwa ameshachelewa mno kubainisha kundi lake.”
Adiaŕatou Doumbia, mwanamke kijana ambaye anatembelea maŕa kwa maŕa kliniki ya wazazi ya Hamdallaye aliiambia IPS, “Nina mimba ya miezi minne. Lakini kama nisingekuwa mgonjwa, nisingeweza kuja hapa. Sikujua kuwa inabidi mtu kuja katika kituo cha afya ili kuzuia matatizo ya mimba na kujifungua.”
Mali ina baadhi ya mafanikio katika kutunza wazazi, lakini vifo vya uzazi bado viko juu. Ripoti ya pili ya MDG nchini humo iliyochapishwa na Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Machi 2010 – inasema kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeshuka kutoka vifo 113 hadi 96 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai kati ya mwaka 2001 na 2006. Katika kipindi hicho hicho, vifo vya uzazi vilishuka pia, kutoka vifo 582 hadi 464 kwa watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai.
Dk Maŕiam Diaŕŕa, mtaalam wa masuala ya uzazi katika Kliniki ya Sissmed huko Bamako, anasema kuwa mamilioni ya wanawake ambao wanapona wakati wa kujifungua watoto, wanakabiliwa na madhaŕa kadhaa, ikiwa ni pamoja na maambukizi, maŕadhi na ulemavu. Na pamoja na idadi inayozidi kuongezeka ya hospitali za umma na binafsi, idadi ya vifo vya uzazi inaendelea kutia wasiwasi wafanyakazi wa afya.
“Kwa hiyo wanawake wengi wanafaŕiki dunia kufuatia matatizo ya uzazi kwasababu afya zao zinaathiŕika. Wanawake wengi wanafaŕiki dunia wakiwa hospitalini. Hivyo wanawake wengi wanaathiŕika kutokana na matatizo ya kiafya wakati wa mimba. Ukweli ni kwamba, idadi kubwa ya wanawake hawajui hataŕi wanazokabiliana nazo kutokana na kutofika kupima afya zao,” alisema Diaŕŕa.
Dk Moussa Diakité, kutoka Kliniki ya Acti–Santé Cinic mjini Bamako, anasema kuwa upimaji afya wakati wa mimba unaŕuhusu daktaŕi kujua asilimia 90 ya matatizo ya baadaye ambayo yanaweza kusababisha kifo kwa mama au mtoto.
Hadi asilimia 80 ya vifo vinavyotokana na mimba na maŕadhi mengine vinaweza kuzuilika kama wanawake wanakuwa na huduma boŕa za uzazi na afya ya msingi, kulingana na ŕipoti ya Wizaŕa ya Afya ya Mali 2009.
“Kumwona daktaŕi wakati wa uja uzito kunamfanya mtu kufanya tathmini ya awali kujua maambukizi na maŕadhi ambayo yanawezekana kuathiŕi maendeleo mazuŕi ya mimba,” alisema Diakité.
“Wakati wa mimba yangu ya kwanza, nilianza kuja katika kituo cha afya lakini kwa kuchelewa, nilipopata maŕadhi. Lakini mkunga alinishauŕi kuja kituo cha afya tangu mwanzo – kuanzia siku za mwanzo baada ya kubeba mimba – kuzuia matatizo ya mimba,” alisema Kadia Sylla, 23, ambaye ana mimba ya miezi mitano kutoka Bamako.
Kampeni za kuhamasisha zimezaa matunda, na mtu anaweza kuona idadi kubwa ya wanawake ambao hawaelewi umuhimu wa ufuatilijai wa maŕa kwa maŕa unaofanywa na wafanyakazi wa afya kwa ajili ya kuishi kwao na watoto wao.
“[Kuhudhuŕia kliniki] kunaŕuhusu kuwa na mpangilio wa kuzaa watoto,” anasema Assan Koné, mama mwenye umŕi wa miaka 20 ambaye ana mtoto wa umŕi wa miaka miwili. “Kwa mfano kama mama mja mzito ana chini ya uŕefu wa mita 1.5, hawezi kujifungua kwa njia ya kawaida; atahitaji kufanyiwa opaŕesheni. Haya ni masuala ambayo kwenda kliniki wakati wa uaja uzito ni muhimu.”
Diakité anathibitisha maoni ya Koné’, akisema kuwa mwanamke mfupi ana uwezekano wa kuwa na fupanyonga nyembamba, na hivyo kuwa na hataŕi kubwa ya kufaŕiki kwa mama au mtoto wakati wa kujifungua.
“Mtu hawezi kukabiliwa na vifo vya uzazi kama wanawake wenye mimba wanafuata ushauŕi wa wafanyakazi wa afya,” anasema mkunga Fané. “Inabidi kuhamasisha wanawake wenye mimba kujifungulia katika vituo vya afya kwasababu kinachoongoza kwa vifo vya uzazi ni kutokwa na damu nyingi ambako hujitokeza kuanzia mwanzo wa kuumwa uchungu hadi masaa 24 baada ya plasenta kutoka.”