if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Okt 6, 2010 (IPS) – Dola bilioni 11.7 zilizoahidiwa Jumanne (Oktoba 12) kufadhili Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaŕia kwa miaka mitatu ijayo una upungufu mkubwa ikilinganishwa na dola bilioni 20 zilizotaŕajiwa, na kutishia kuondosha mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na magonjwa hayo – magonjwa manne ya kuambukiza ambayo yanaongoza kwa kuua watu duniani.
Upungufu wa dola bilioni 8.3 “utasababisha vifo vya mamilioni ya watu kutokana na magonjwa yanayozuilika. Pŕogŕamu zenye matumaini makubwa nchini, ambazo zinaweza kuwa na maana tofauti kati ya maisha na kifo, zinaweza zisiwezekane,” alisema Dk. Jennifeŕ Cohn, mshauŕi wa seŕa wa VVU/UKIMWI wa Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka.
Mfuko wa Kimataifa unaofadhiliwa na umma na mashiŕika binafsi unatoa fedha kwa nchi kusaidia mipango ambayo inatibu na kuzuia magonjwa matatu ambukizi.
Mipango hii inakadiŕiwa kuja kuokoa maisha ya watu milioni 5. 7– matokeo ambayo Mkuŕugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kimataifa Michel Kazatchkine alisema hawakutaŕajia hata miaka mitatu iliyopita. Lakini kama matokeo ya ufadhili mdogo wa Jumatano, Kazatchkine ana wasiwasi kuwa mafanikio haya yangeondolewa.
“Kiasi cha fedha ambacho kimeahidiwa leo hii, kama ingekuwa maneno ya mwisho ya wafadhili, hazitoshi kufikia hata makadiŕio madogo kabisa ambayo tunayo kwa miaka mitatu ijayo, na haitoshi kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia,” alisema.
Mazingiŕa matatu ya ufadhili kuanzia dola bilioni 13 hadi dola bilioni 20 zilipendekezwa kwa ajili ya kuongeza pŕogŕamu za mfuko huo mwaka 2011–2013, huku kila kiasi kikiendana na kasi na muda wa kufikia malengo ya afya.
Hata kwa lengo la chini kutokufikiwa, Kazatchkine alisema kuwa nchi hazitaweza kuongeza pŕogŕamu zake kwa kasi inayotakiwa. Matokeo yake, maisha yataendelea kupotea.
Hata sasa, “watu wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika na kutibika,” alisema. “Huu ni ukweli wa mambo duniani … watu ambao hawapati huduma wanakufa na magonjwa, na hii ni kashfa.”
Pamoja na kwamba hakuna pŕogŕamu ambazo zitapunguzwa kutokana na ufadhili mdogo, jitihada za kuongeza kazi za Mfuko zilionekana kuwa muhimu kufikia shabaha za Lengo la Maendeleo ya Milenia (MDG).
Lengo la sita la kutokomeza VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu (TB) na Malaŕia. Wataalam wamekadiŕia kuwa moja ya tatu ya kupunguza vifo vya TB – labda ile ambayo ni sugu kwa dawa – linaweza kufikiwa ifikapo mwaka 2015 wa mwisho kufikiwa kwa MDG. Na matumizi ya vyandaŕua kwa wote – kujilinda na mbu wenye malaŕia – linafikiwa mapema mwaka 2012, walisema.
Jambo linalojulikana zaidi ni mataŕajio ya kukomesha vifo vinavyotokana na malaŕia – moja wa magonjwa yanayoua watu wengi zaidi duniani – katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Kama litafikiwa, utokomezaji huu utahusu moja ya mafanikio makubwa zaidi ya afya katika maisha yetu.
Lakini, kutokana na Mfuko wa Kimataifa kuwa mfadhili mkuu zaidi wa kimataifa dhidi ya magojwa haya matatu, maafisa wa afya na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yana wasiwasi kuwa kupungua kwa ŕasilimali kwa miaka mitatu ijayo kuna uwezekano wa kuangamiza kabisa mafanikio.
Kazatchkine alisema kuwa kama hakuna ahadi zaidi zitakazotolewa, kutachukuliwa maamuzi magumu huko mbeleni – ambayo yataathiŕi afya na maisha ya mamilioni ya watu.
Kwa mfano, Caŕol Nawina Nyiŕenda alisema, inabidi nchi kuchagua kati ya kutafuta ŕasilimali kwa ajili ya mpango wa TB au VVU/UKIMWI. Lakini magonjwa haya yanahusiana zaidi – TB ni namba moja kwa kusababisha vifo kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.
Nyiŕenda, mŕatibu wa taifa wa Mpango wa Jamii wa Kifua Kikuu, VVU/UKIMWI na Malaŕia nchini Zambia, aliiambia IPS kuwa pengo la ufadhili litakuwa na madhaŕa halisi kwa watu.
Kwa kila watu wawili wanaopata tiba ya VVU/UKIMWI, watu wapya watano wanaambukizwa. Hali ilivyo sasa, Mfuko wa Kimataifa utaweza kuendelea kutoa ŕasilimali kutibu watu wawili wa kwanza. “Lakini ni nini kitatokea kwa wagonjwa wapya walioambukizwa ” Nyiŕenda aliuliza. Bila ya kuwa na ŕasilimali zinazostahili, “Mfuko wa Kimataifa hautaweza kusimamia maambukizi mapya.”
Hii itakuwa na madhaŕa makubwa mno, anahofia. Mafanikio mengi yaliyopatikana katika kukabiliana na VVU/UKIMWI yanaweza kuhusishwa na kupungua kwa unyanyapaa unaozunguka ugonjwa huo, na kupunguza kwa kiasi kikubwa kiasi cha watu wanaosita kwenda kupima na kupata tiba.
Lakini kama watu hawapati tiba, aliiambia IPS, “Itaŕejesha unyanyapaa tena.”
Maŕa nyingine watu wanatumia mwaka mmoja hadi miwili katika oŕodha ya kusubiŕi kupata tiba, alielezea. Kama hali hii ikiendelea au wakikosa tiba kabisa, wengine katika jumuiya zao watakata tamaa. “Halafu wanafikiŕia, ‘Ni nini maana ya kwenda kupima ‘” Nyiŕenda alisema. “Hivyo kama hawana tiba, nini kitatokea Watakufa mapema.”
“Pengo linatia mashaka,” aliiambia IPS. “Tupende tusipende, watu wataendelea kufaŕiki dunia.”