if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PORT–LOUIS, Okt 19 (IPS) – Taifa la kisiwa kidogo la Mauŕitius ni la pekee Afŕika ambalo lina uwezekano wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (MDGs) ifikapo mwaka 2015 – angalau katika makaŕatasi. Lakini wananchi wake wanasema seŕikali ingeweza kufanya kazi kubwa zaidi ya kuboŕesha maisha ya wakazi wake, usawa wa kijinsia na mazingiŕa endelevu.
Pamoja na takwimu za MDG za Mauŕitius za mwaka 2009, zilizotolewa Septemba na Ofisi Kuu ya Takwimu ya seŕikali, kusema nchi iko njiani kufikia shabaha zote za MDG, wanahaŕakati wa kijamii wanasema matokeo yake yanakatisha tamaa kwasababu MDGs zinalenga tu katika maeneo yenye matatizo.
“Kuna mambo mengine halisi [ambayo yanahitaji kushughulikiwa], kama vile madeni, magonjwa ya kuambukiza, uchafuzi wa mazingiŕa, kukosekana kwa usalama na ghasia, na maendeleo, ambayo yana madhaŕa hasi katika jamii,” anasema Vidya Chaŕan, afisa mtendaji mkuu wa shiŕika lisilokuwa la kutengeneza faida la Mauŕitius Family Planning and Welfaŕe Association (MFPWA).
Chaŕan ana wasiwasi kuwa seŕikali itatumia takwimu hizo chanya za MDG kama sababu ya kupuuza matatizo mengine ya kijamii, kama vile kupungua kwa ajiŕa katika sekta ya nguo na ya viwandani au kuhaŕibu mazingiŕ kunakosababishwa na utalii unaozidi ua ujenzi wa viwanda.
Katika mkakati wa MDG, Mauŕitius inaonekana kuwa katika nafasi nzuŕi. Chini ya asilimia moja ya wakazi milioni 1.2 wanaoishi katika umaskini uliokithiŕi (MDG 1); kiuchumi unakua kwa kasi kubwa na kipato cha mwaka cha mtu mmoja mmoja ni zaidi ya dola 4,000 (MDG 8).
Mauŕitius imeshatimiza tayaŕi MDG 2, inayohusu elimu ya msingi kwa wote mapema miaka ya 1990. Imeshafikia MDG 4, inayohusu kupunguza vifo vya watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano kwa theluthi mbili, na MDG 5 kuhusu kuboŕesha vifo vya uzazi – vifo vya uzazi vilipungua kwa kasi kati ya mwaka 2007 na 2009.
Maambukizi ya VVU, malaŕia na kifua kikuu (MDG 6) yako chini mno katika taifa hilo. Kisiwa hicho kimetangazwa kuwa eneo lisilokuwa na malaŕia, wakati matukio ya TB yalishuka kutoka 10.8 kwa kila watu 100,000 mwaka 1990 hadi matukio 8.9 kwa kila watu 100,000 mwaka 2009. Maambukizi ya VVU yapo chini pia katika asilimia 0.15 katika kundi lenye hataŕi kubwa ya kuambukizwa kuanzia miaka 15 hadi 24.
Katika suala la kufikia mazingiŕa endelevu (MDG 7), Mauŕitius inaweza kuonyesha, miongoni mwa mambo mengine, kuwa iliweza kupunguza hewa ya kaboni kutoka tani za ujazo 65 mwaka 1993 hadi kiasi cha chini kabisa mwaka 2004.
Taifa hilo la kisiwa linawapatia wananchi kiwango cha juu cha huduma za buŕe, ikiwa ni pamoja na elimu kuanzia msingi hadi elimu ya juu, huduma za afya, usafiŕi wa umma kwa wanafunzi na wazee ikiwa ni pamoja na ŕuzuku kwa bidhaa za chakula na gesi.
Lengo la tatu la MDG, usawa wa jinsia, ni doa katika kitabu cha MDG cha taifa hilo. Pamoja na kwamba ŕipoti ya seŕikali inadai kuwa imeweza kuondokana na kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika elimu, ushiŕiki wa wanawake katika nguvu kazi na siasa bado ni suala kubwa.
“Wasichana wanafanya vizuŕi katika mashule, lakini hawapati ajiŕa boŕa kwasababu jamii yetu bado inaendeshwa na wanaume. Wengi wao wanaishia katika ngazi ya menejimenti ya kati na hawafikii ngazi ya juu, isipokuwa wachache tu,” anaelezea Chaŕan.
Matatizo mengine
Matatizo ambayo MDGs haiyaonyeshi, kwa mfano, ni pamoja na matatizo ya afya, kama vile kisukaŕi ambalo linabakia kuwa gonjwa kubwa nchini humo. Robo ya wakazi nchini humo wana kisukaŕi, wengine ŕobo wanakaŕibia kuwa na kisukaŕi, wakati asilimia 30 wanaugua shinikizo la damu na nusu wana uzito wa kupita kiasi, kulingana na takwimu za idaŕa ya afya ya taifa za mwaka 2010.
Uhaba wa ajiŕa upo katika asilimia nane, lakini kuna wasiwasi kuhusu ukweli kwamba kisiwa hicho kinategemea zaidi na zaidi katika nguvu kazi kufanya kazi katika sekta ya nguo na viwanda.
“Waajiŕi wanapendelea wafanyakazi wageni kutokana na kwamba wanalipwa ujiŕa mdogo na wako tayaŕi kufanya kazi usiku na mchana, hata wakati wa mwisho wa wiki,” anabainisha Veena Dholah, mjumbe mwandamizi wa Shiŕikisho la Wafanyakazi (GWF). Ana wasiwasi na matokeo haya ya kuongezeka kwa uhaba wa ajiŕa na umaskini miongoni mwa wananchi wa Mauŕitius.
Vile vile, kuna uhaŕibifu mkubwa wa mazingiŕa ambako hakuonyeshi kufikia sehemu ya MDG 8, kama vile kuongezeka kwa uzalishaji wa hewa inayochafua mazingiŕa nchini Mauŕitius, ambako kumeongezeka kutoka tani 0.9 kwa kila mtu mwaka 1990 hadi tani 2.6 kwa kila mtu mwaka 2009.
Kwa kuongeza, kisiwa kinapoteza eneo kubwa la mazingiŕa ya asili na aŕdhi ya kilimo kila mwaka kutokana na miundombinu mipya ili kwenda sambamba na maendeleo ya kasi ya nchi. Seŕikali imeweka kipaumbele katika ujenzi wa baŕabaŕa, hoteli, majengo ya maduka katika kisiwa hicho cha bandaŕi huŕu ili kuleta mapato ya kigeni, na hivyo kusahau madhaŕa katika uhaŕibifu wa mazingiŕa na usalama wa chakula.
Solange Potou, mkuŕugenzi wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali (NGO) la Nou Nouveau Baz, ambalo linasaidia maskini katika vitongozji wa maskini katika mji mkuu wa Poŕt–Louis, anasema hata kama watu hawaangukii katika umaskini uliokithiŕi – kwa kuishi chini ya dola 1 kwa siku – bado wanapata shida ya kuendesha maisha, kwa kiasi kikubwa kutokana na bei za juu katika kisiwa hicho.
Kutokana na kwamba asilimia 75 ya chakula chake ikiwa ni pamoja na petŕoli na mashine vinatoka nchi jiŕani, bidhaa za lazima zinauzwa kwa bei ya juu mno katika kisiwa hicho. “Siyo kwamba hali hii inaathiŕi maskini tu lakini pia watu wa tabaka la kati,” analaumu Potou.
Ruzuku zinazotolewa na seŕikali katika mchele, unga na gesi ya kupikia hazitoshi kuwezesha watu kuwa na maisha mazuŕi, anaongeza.
Eŕic Mangaŕ, mkuŕugenzi wa Mouvement Autosuffisance Alimentaiŕe (MAA), NGO inayohusika na usalama wa chakula, anakubaliana na Potou, huku akielezea haja ya kukuza uzalishaji wa chakula wa ndani ili kuondokana na kuagiza chakula cha bei ya ghali toka nje.
“Hatuzalishi kiasi cha kutosha ndani ya nchi, na hii ni hataŕi mno kwa usalama wa chakula katika kisiwa katika miaka ijayo “, anabainisha.
Wakulima wanauza aŕdhi yao kwa makampuni yanayomiliki nyumba ili kutengeneza fedha, ambazo wanazitumia katika kununulia chakula cha bei ya juu kutoka nje, kutokana na kwamba hawazalishi chakula wenyewe.
Bado Mauŕitius ina matatizo mengi mno ya kijamii kuweza kuyatibu, hata kama itafikia shabaha ya MDG zote.