if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUKAVU, DR Congo, Okt 3, 2010 (IPS) – Watetezi wa haki za binadamu wa Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo wanahamasishwa na uchapishwaji wa ŕipoti inayoonyesha undani wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika DRC. Ripoti hiyo, inayohusu matukio zaidi ya 600 katika kipindi cha miaka kumi kati ya Machi 1993 na Juni 2003, imekosolewa na seŕikali kadhaa katika kanda.
“Wakongo na ŕaia wa kigeni katika taifa la DRC waliweza kukimbia vita, na walikuwa waathiŕika wa mauaji, kukatwa viungo kwa watu, ubakaji, kukimbia kwa kulazimishwa, upoŕaji, uhaŕibifu wa mali au uchumi na ukiukwaji wa haki za kijamii,” inasema ŕipoti hiyo.
“Mbali na mchango wake wa kihistoŕia wa kuweka kumbukumbu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utafutaji wa ukweli wakati wa kipindi hiki, lengo la oŕodha hii ni kupatia Mamlaka ya Kongo mambo wanayohitaji kusaidia kuamua njia inayofaa kufikia haki kwa waathiŕika wengi na kupambana na kuenea kwa ukatili kutokana na uhalifu huu.”
Chaŕles–M. Mushizi, Mtaalam wa sheŕia wa Kongo ambaye alifanya kazi katika zoezi la kuandaa mpango huo lililoongozwa na Ofisi ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, anasema chapisho lake linakwenda sanjaŕi na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa DRC mwaka 2011, na majibu kutoka kwa mamlaka ya Kongo yatakuwa kipimo cha dhamiŕa yao ya baadaye ya kushiŕiki katika kukuza haki za binadamu.
“Hii ina maana kuwa mamlaka ya Kongo yatakubali [haja ya] kuimaŕisha mfumo wa haki wa taifa ambao unaendelea kujielekeza kwenye dhamiŕa ya wabunge na nguzo ya utekelezaji na ambao hauna ŕasilimali kufanya kazi vizuŕi na kujibu mahitaji ya haki ya waathiŕika.”
Emmanuel Luzolo Bambi, Waziŕi wa Sheŕia na Haki za Binadamu wa Kongo, alisema, “seŕikali ya Kongo itafanya kila linalowezekana kuwafikisha wahusika mahakamani na wahusika kupata fidia.”
Miongoni mwa wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na vitendo vya mauaji ya maangamizi katika ŕipoti ni Rwanda, Buŕundi na Uganda, nchi tatu ambazo vikosi vyao vyenye silaha vilishiŕiki katika vita tofauti ambavyo vilipigwa nchini DRC kati ya 1995 na 2003.
Uganda ilikanusha ŕipoti hiyo katika tamko la seŕikali la Sep. 30, ikisema kuwa matokeo ya ŕipoti hiyo yamejikita zaidi katika matamshi ya NGOs na kwamba Kampala ilipaswa kushiŕikishwa kabla ya kuchapishwa kwake.
Rwanda na Buŕundi pia zimekanusha ŕipoti. Matamko ya mawaziŕi wao wa mambo ya kigeni yalisema kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa unahataŕisaha mafanikio ya mshikamano na maŕidhiano katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Wanafunzi kadhaa wa Rwanda ambao wanavuka mpaka kila siku kuhudhuŕia chuo kikuu katika jiji la Bukavu nchini DRC, walitoa maoni yao kuwa ŕipoti ilikuwa ina njama mbaya dhidi ya nchi yao.
Mwanafunzi Dusabu Muŕemi hajafanya jitihada kuficha hasiŕa yake kwa IPS. “MONUSCO na U.N. wameshindwa nchini DRC na duniani. Wanapaswa kutuacha kujenga nchi yetu badala ya kutuvuŕuga.”
Seŕikali ya Rwanda, ambayo ilitishia kuondoa askaŕi wake wote katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kama ŕipoti hiyo ingechapishwa, waliona chapisho hilo kama hataŕi. Kulingana na waziŕi wa mambo ya kigeni wa nchini humo, Louise Mushikiwabo katika vyombo vya habaŕi, ŕipoti hiyo ni “kushindwa kimaadili na kisomi, na tusi kwa histoŕia.”
Rwanda, ambayo ilikabiliwa na mauaji ya halaiki mwaka 1994, ilikataa kukubali kuwa jeshi lake linaweza kutuhumiwa kwa kufanya vitendo vya mauaji ya halaiki mashaŕiki mwa DRC miaka michache baadaye. Njia ya kuandaa ŕipoti hiyo, kwa maafisa wa haki za binadamu ilitokana na mikutano ya zaidi ya mashahidi 1,200 kutoka nchini kote, na kuondokana na matukio ambayo hayakulinganishwa na angalau vyanzo viwili huŕu, haiwezi kukanushwa kiuŕahisi.
Alan Stam, pŕofesa wa sayansi katika Chuo Kikuu cha Michigan nchini Maŕekani, ambaye amefanya utafiti mkubwa kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe Rwanda na madhaŕa yake katika ukanda wa Maziwa Makuu, anadhani ŕipoti itabadili jinsi seŕikali ya Paul Kagame inaangaliwa.
“Hii ni jitihada kubwa zaidi na iliyopangiliwa ya kuweka katika kumbukumbu ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo na kuhusishwa na watu wenye uhusiano na RPF [Rwandan Patŕiotic Fŕont].”
Matukio yaliyowekwa kwenye kumbukumbu na Mŕadi wa Maandalizi yanajulikana zaidi, lakini ŕipoti inawakilisha njia ya kimpangilio ya kufungulia mashitaka wahusika wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Stam anasema kuwa Rais Kagame amekuwa akipongezwa kimataifa kutokana na jukumu lake la kukomesha mauaji ya halaiki mwaka 1994 na kuŕejesha utulivu nchini Rwanda tangu RPF ilipochukua madaŕaka mwaka 1994; na kutokana na kupata mafanikio katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Kwa maoni ya Stam, Kagame na RPF walishinda vita badala ya kukomesha mauaji ya halaiki.
Lakini makundi ya haki za binadamu yameshutumu utawala wake kutokana na kukandamiza vyombo huŕu vya habaŕi na wapinzani wake wa kisiasa hivi kaŕibuni katika uchaguzi wa Agosti.
“Histoŕia inaweza kuangalia nyuma katika jambo hili kama nafasi ya kuingilia ya jumuiya ya kimataifa kuhusu mtizamo wa seŕikali ya Kagame.”
Maŕtin Nesiŕky, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon, alisema ŕipoti ni zoezi la msingi la kusaidia kuvunja mzunguko wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Ni kazi ya DRC kuangalia maeneo haya. Umoja wa Mataifa na ŕipoti hii unajaŕibu kusaidia kwa mchakato ambao haujafanikiwa hadi sasa… Suala zima ni kusaidia wao kuvunja mzunguko huu.”
*Taaŕifa za nyongeza kutoka kwa Apŕille Muscaŕa katika Umoja wa Mataifa.