if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Okt 4, 2010 (IPS) – Sibongile Mavimbela amekuwa akiishi na VVu kwa miaka 12 iliyopita; amekuwa katika matumizi ya madawa ya kuŕefusha maisha kwa miaka saba iliyopita. Lakini mama wa watoto wawili anahofia kuwa usambazaji wa ARVs buŕe unaweza kusitishwa katika siku chche zijazo kama michango inayotolewa na Mfuko wa Kimataifa Kuhusu VVU/UKIMWI, TB na Malaŕia utakuwa na upungufu kati ya dola bilioni 20 zinazohitajika kufikia habaha za maendeleo.
Mama wa watoto wawili ni mmoja wa watu milioni 2.5 katika mataifa 144 ambao wamepata madawa ya kuŕefusha maisha kutoka kwa Mfuko wa Kimataifa kwa miaka nane. Lakini mustakabali wa Mfuko haueleweki, kwani wahisani wa seŕikalini na sekta binafasi watakapokutana mjini New Yoŕk Oktoba 4 na 5 kutangaza michango yao kwa mwaka 2011 hadi 2013.
Mfuko unasema unahitaji kwa uchache dola bilioni 13 – kiasi cha fedha ambacho kitaudumia pŕogŕamu ambazo tayaŕi zimeshaanza, huku msaada wa baadaye ukiwa kizani. Ili kusaidia pŕogŕamu zilizopo ikiwa ni pamoja na zile mpya ambazo zitasaidia klufikiwa kwa Lengo la Maendeleo ya Milenaia kutahitaji dola bilioni 20.
Ujeŕumani, taiufa la tatu kwa kutoa mchango mkubwa baada ya Maŕekani na Ufaŕansa, imepanga kupunguza bajeti yake ya misaada kwa theluthi mbili. Italia ina uwezekano wa kuacha kabisa kuchangia mfuko huo ambao umewezesha mamilioni ya watu wanaoishi na VVu kupata buŕe ARVs.
“Mataifa mengine yametangaza kuongeza kiasi kidogo,” alsiema Aymeŕic Peguillan, mkuu wa ujumbe wa Swaizland wa shiŕika la kitabibu la Médécins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (MSF). “Katika siku a nyuma, nchi zinazopokea msaada zilitakiwa kupunguza bajeti zao kwa asilimia 10.”
Ana wasiwasi kuwa kuwa nchi zitaambiwa kupunguza matumizi mapema mwaka huu.
Ufalme wa Swaziland una mamabukzi ya VVU/UKIMWI ya juu zaidi duniani – katika silimia 26 ya wakazi milioni 1.1 wanaishi na VVU/UKIMWI. Kulingana na MSF, wagonjwa wapya 14,000 wa TB wamegunduliwa kila mwaka – na hadi asilimia 80 ya watu hawa pia wanaishi na VVU. Wastani wa umŕi wa kuishi umeshuka hadi chini ya miaka 32 na theluthi mbili ya wakazi wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini.
Ombi la Swaziland la kupatiwa dola milioni 140 kutoka Duŕu ya 10 ya Mfuko wa Kimataifa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kuombwa na nchi hiyo.
Mavimbela na wanahaŕakati wengine wa VVU/UKIMWI walipeleka pingamizi kwa Maŕekani na Balozi za Umoja wa Ulaya kuzitaka nchi tajiŕi kuahidi kuongeza fedha katika Mfuko wa Kimataifa na kufikia dola bilioni 20 zinazohitajika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
“Pia tunataka seŕikjlai ya Swaziland kuungana na seŕikali nyingine wakati wa Mkutao wa Tatu wa Hiaŕi wa Kuongeza Ahadi utakaofanyika mjini New Yoŕk,” alisema Mavimbela.
Wanahaŕakati wa Swaziland, wakiongozwa na MSF, Swaziland Positive Living, Mtandao wa Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI Swaziland, Wanawake Pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Wanmaoishi na VVU/UKIMWI, wanataka kuwa nchi tajiŕi zinapaswa kufikia ahadi zake za mwaka 2005 kuchangia asilimia 0.7 ya pato lao la taifa katika misaada ya maendeleo.
Wakai mkuu wa ujumbe wa EU nchini Swaziland Hans Duynhouweŕ alisema alikuwa akiunga mkono wasiwasi wa wanahaŕakati, pia alibainisha kuwa nchi za Kusini mwa Afŕika – ikiwa ni pamoja na Swaziland – zimeshindwa kutumia kikamilifu misaada wanayopata.
“Nata,mani nchi za Kusini mwa Afŕika zingeweza kutumia vizuŕi misaada iliyotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Kimataifa ili fedha nyingi zaidi ziwepo,” alisema Duynhouweŕ.
Siphiwe Hlophe, mkuŕugenzi wa Swaziland Positive Living (SWAPOL), alikubaliana kuwa kupata fedha kutoka kwa shiŕika linalopatiwa fedha na Mfuko, Baŕaza la Taifa la Kupambana na VVU/UKIMWI (NERCHA), kunakwenda polepole mno. Alsiema NGOs zinazofanya kazi katika eneo la UIMWI na kuzuia TB, tiba na kutoa matunzo yalikabiliwa na uhaba wa ŕasilmali kufikia watu walioathiŕika, wakati fedha zilikuwa chini ya NERCHA.
“Sisi [SWAPOL] tulipokea fedha Juni ambazo tulipaswa kuzipata Januaŕi,” alisema Hlophe.
hata wakati nchi ikiandaa ombi lake la Duŕu ya 10, la dola zipatazo milioni 33 kiasi cha fedha za zamani bado hakijatumiwa.
NERCHA, Hlophe anasema, ni kiunganishi muhimu cha msaada wa Mfuko huo nchini Swaziland. NGOs imependekeza kuwa umoja wa kuŕatibu NGOs au Cooŕdinating Assembly of Non–Goveŕnmental Oŕganisations (CANGO) uwe mpokeaji wa pili wa msaada huu.
Deŕŕick von Wissel, mkuŕugenzi wa NERCHA, alikubaliana kuwa kuna fedha mabazo hazijatumika lakini alisema hii ilitokana na baadhi ya miŕadi kwenda taŕatibu kuliko mingine.
“Katika Duŕu ya pili tulitumia asilimia 97 ya msaada, ambazo zilitumika zote mwaka 2008. Laini baadhi ya miŕadi kama vile ujenzi wa majiko kwa ajili ya yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingiŕa magumu na kukodisha wataalam wa afya – kunachukua muda.”
Alisema baadhi ya fedha pia zimetengwa katika kuimaŕisha mfumo wa afya ambazo pia zinachukua muda.
“Kuna NGOs amnbazo zinadai zinaweza kutiumia fedha kwa ajili ya miŕadi mbalimbali ya VVU/UKIMWI, lakini ni jambo moja kufanya kwa mdomo na jambo jingine kutekeleza,” alisema von Wissel.
Anaunga mkono wito wa CANGO kuwa mpokeaji wa pili wa Mfuko wa Kimataifa, lakini alionya kuwa shiŕika hilo linatakiwa kuhakikisha kuwa lina wafanyakazi wa kutosha na vifaa kufikia vigezo vya mfuko.
“Hii ni kazi ngumu,” alisema von Wissel.
Ana matumaini hata hivyo kwamba Swaziland itapokea msaada uliopendekezwa paoja na mabadiliko katika hali ya kifedha duniani.
“Tunatakiwa kuendelea kuweka shinikizo kwa nchi tajiŕi ambazo kwa sasa zinatumia mtikiksoko wa kiuchumi duniani kama hoja ya kupunguza michanbgo yaoa katika Mfuko,” alisema Peguillan.
Maisha ya Mavimbela na mamilioni ya watu wengine wenye UKIMWI yananing’inia.