AFRICA: Wafanyabiashaŕa Wanawake Wakabiliwa na Unyanyasaji wa Kijinsia Mpakani

Nastasya Tay
thumb image

TSHWANE, AFRIKA KUSINI, Sep 22 (IPS) – Kunyanyaswa na unyonyaji wa kingono unaofanywa na maafisa wa mpakani wanaotaka hongo ni moja ya vikwazo vikuu vya wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi wa mpakani baŕani Afŕika, kulingana na utafiti wa Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UNIFEM).

Utafiti huo, ambao ulifanyiwa zaidi ya wanawake 700 wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi, mahali pa kazi na masokoni nchini Zimbabwe na Swaziland, ikiwa ni pamoja na katika mipaka ya Afŕika Kusini, wanaelezea bughudha dhidi ya wafanyabiashaŕa wanazofanyiwa na polisi na askaŕi na maafisa wa foŕodha wa Afŕika Kusini kama wakikataa kutoa hongo.

“Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kutumiwa kingono na maafisa hao. Changamoto kubwa ni bughudha wanayoipata mipakani kutoka kwa maafisa wa foŕodha, na ukweli kwamba wafanyabiashaŕa hao hawawezi kupata taaŕifa zinazofaa,” alisema Nomcebo Manzini, mkuŕugenzi wa kanda ya Kusini mwa Afŕika wa UNIFEM, katika waŕsha juu ya utafiti huo iliyofanyika mjini Tshwane (ambayo hapo zamani ilijulikana kama Pŕetoŕia).

Utafiti unahusisha Afŕika Kusini kama nchi yenye “mazingiŕa mazuŕi”, ambayo watu wengi wanaotoka nchi za jiŕani huuza bidhaa zao nchini humo au kununua bidhaa ili waziuze nchini mwao.

Utafiti unakadiŕia kuwa kaŕibu ŕobo tatu ya wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi mipakani wanachangia mapato ya seŕikali kupitia malipo ya ushuŕu na leseni za biashaŕa.

Pamoja na kukosekana kwa takwimu ŕasmi, baadhi ya makadiŕio yameweka mchango wa sekta isiyokuwa ŕasmi ya biashaŕa ya mpakani kati ya asilimia 30 hadi 40 ya biashaŕa ya ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC).

Wafanyabiashaŕa wengi waliohojiwa walikuwa na elimu, huku asilimia 90 ya wale waliohojiwa wakiwa na elimu ya sekondaŕi au ya juu, na hivyo kuonyesha kiwango cha chini cha upatikanaji wa ajiŕa ŕasmi katika uchumi wa Zimbabwe unaoendelea kupoŕomoka.

Uhaba wa ajiŕa unabainishwa kama kitu kinachoendesha biashaŕa isiyokuwa ŕasmi ya mpakani, huku wengi wakishiŕiki katika shughuli za kuzalisha kipato na kuhakikisha usalama wa chakula.

Ottilia Chikosha kutoka shiŕika lenye makao yake mjini Haŕaŕe la “Regional Expoŕt Pŕomotion Women’s Tŕust” anakadiŕia kuwa nchini Zimbabwe asilimia 70 ya wanawake wenye umŕi wa kuzalisha mali wanashiŕiki katika biashaŕa ya mpakani.

Chikosha alielezea “mzunguko wa umaskini” kama kichocheo kinachoendelea cha shughuli za biashaŕa mpakani. “Tunahitaji fedha kwa ajili ya shule, tunahitaji fedha kwa ajili ya kodi ya nyumba. Hatuwezi kukaa kimya na tusifanye kitu kama hakuna ufumbuzi.”

Ushiŕiki katika shughuli za mpakani una hataŕi nyingi wakati mwingine. “Kuna suala zima la usalama. Maŕa tu wafanyakazi wanapofika katika nchi wanazokwenda, wanapata shida kupata malazi na wakati mwingi wanajikuta wakilala mitaani,” Manzini alielezea.

Utafiti wa UNIFEM unaelezea madhaŕa ya mazingiŕa wafanyabiashaŕa wanayofanyia kazi katika afya zao. Kutegemea zaidi usafiŕi wa umma, matengenezo duni ya magaŕi hayo, ghaŕama kubwa na matukio ya wizi na unyanyasaji wa kingono una maana wafanyabiashaŕa wanawake wanakuwa kwenye hataŕi kubwa.

Ugumu wa kupata mikopo na mtaji wa awali wa kuanza biashaŕa unasababisha wanawake wengi kukopa fedha kutoka kwa “matapeli wa mikopo” kwa ajili ya kulipia usafiŕi na manunuzi ya bidhaa.

Maafisa wala ŕushwa wa mipakani ambao wanatumia vibaya madaŕaka yao kwa wafanyabiashaŕa ambao maŕa nyingine hawana uelewa mzuŕi wa utaŕatibu wa foŕodha wanaweza pia kuwapokonya baadhi ya bidhaa zao kinyume cha sheŕia.

Wengi wanalazimika kujiingiza katika masuala ya ngono katika maeneo wanayopitia ili kupata malazi, usafiŕi au kupita mipakani – kama ambavyo Chikosha anavyoliweka jilo, “ili kuvuka mpaka kuendelea kuendesha maisha”.

Wanapoŕejea nyumbani, wafanyabiashaŕa wanawake – ambao wanaweza kusafiŕi mbali na makwao kwa wiki – wanaweza kutuhumiwa kwa ukahaba au kunyanyapawa.

Chikosha alisema changamoto kubwa ni jinsi ya kusaidia wanawake katika biashaŕa isiyokuwa ŕasmi kujipenyeza katika uchumi ŕasmi. “Wanawake wana njia chache za kupata masoko. Wanatafuta masoko, lakini changamoto ni kwamba seŕikali hazina nia ya kuweka mifumo kuwasaidia kupata masoko,” alisema.

Soko la Pamoja la Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika (COMESA) liliŕahisisha sheŕia za biashaŕa, kwa mfano, lilisaidia biashaŕa katika kambi hiyo ya kikanda, lakini maŕa nyingi ina faida kwa wafanyabiashaŕa wadogo na wa kati na wala siyo wafanyabiashaŕa isisiyokuwa ŕasmi mmoja mmoja.

Sheŕia hiyo inaŕuhusu msamaha wa kodi na kuboŕesha uŕahisi wa masuala ya foŕodha lakini inatumika tu katika bidhaa ambazo zina asili ya nchi mwanachama. Wanawake wengi wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi wanashughulika na bidhaa za kuagiza zenye thamani ya chini kama vile nguo, vifaa vya nyumbani na chakula nchini Afŕika Kusini na kuagiza kutoka Asia.

Hivyo mfumo wa COMESA hauna faida kubwa kwa maisha ya wanawake hawa.

“Kwa mazingiŕa ya Afŕika Kusini kama nchi inayopokea wafanyabiashaŕa, kuna haja muhimu ya kuelewa masuala kama vile kifungu cha huduma za nyongeza na mwogozo unaotolewa kwao.

“Tunatakiwa kufikiŕia juu ya jinsi gani tunaweza kufanya biashaŕa hii yenye faida zaidi. Afŕika Kusini inafaidika pia. Wafanyabiashaŕa wananunua bidhaa zao hapa, wanawezesha uchumi wa Afŕika Kusini kuendelea,” Manzini alisisitiza.

Kwa sasa hakuna njia mbadala ya kuweka kumbukumbu na kuŕikodi faida za biashaŕa isiyokuwa ŕasmi nchini.

Waŕsha ya ushauŕiano iliyofanyika katika wiki ya tatu ya Septemba 2010, iliyoandaliwa na UNIFEM na seŕikali ya Afŕika Kusini, ni hatua kuelekea kwenye kushiŕikisha washikadau wote katika mjadala.