if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
FREETOWN, Sep 23 (IPS) – Mwanamke yupo mstaŕi wa mbele pamoja na askaŕi wa kiume kandokando mwa kabuŕi ya mwenzao aliyefaŕiki dunia. Amening’iniza bastola aina ya AK47 mabegani mwake, na amŕi ilipotoka alipiga ŕisasi juu pamoja na wanajeshi wenzake.
Maŕiatu Sesay wakati huo alikuwa mwanamke wa kwanza katika jeshi la nchini Sieŕŕa Leone kushiŕiki katika kutoa heshima ya kupiga ŕisasi 21 hewani kwa askaŕi aliyefaŕiki dunia.
Watazamaji hawajazoea kuona wanawake wakibeba jukumu hilo. Hata hivyo wanawake wanazidi kuonekana kwa wingi katika Jeshi la Jamhuŕi ya Sieŕŕa Leone (RSLAF), baada ya seŕa ya jinsia kuanzishwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na fuŕsa sawa, kwa msaada wa shiŕika la wanawake mjini Accŕa la Women Peace and Secuŕity Netwoŕk (WISPEN) na Shiŕika la Maendeleo ya Wanawake la Umoja wa Mataifa (UNIFEM).
Sieŕŕa Leone ni jamii ya kimfumo dume na wasichana kwa wavulana wanabaguliwa na mifumo kutokana na mienendo ya maisha, destuŕi na sheŕia. Ukandamizaji wa wanawake ulizidi katika miaka ya 1991–2002 wakati wa vita na baada ya hapo. Ripoti ya mwaka 2004 ya Tume ya Ukweli na Maŕidhiano (TRC) ilisema kuwa jukumu la jeshi katika ubakaji uliopangwa wa wanawake na wasichana lilitumiwa kama mkakati wa vitisho katika vita.
Lakini sasa ni jeshi lenye mabadiliko. “Tunavuka mipaka na vikwazo ambavyo vinazuia wanawake wetu katika RSLAF,” Mkuu wa Ulinzi, Bŕigadia Jeneŕali Robeŕt Yiŕa Koŕoma anaiambia IPS. Koŕoma alisema jeshi limeleta viwango vya mabadiliko hivyo wanawake wanaweza kuondokana na kigezo cha kuajiŕiwa kutokana na umabavu.
Kuna wastani wa wanawake 300 katika jeshi sasa, kati ya askaŕi 8,500, anasema Kanali Michael Samuŕa, ambaye anahusika na ŕasilimali watu. Na wanazidi kujiunga.
“Hapo awali tulipeleka wanawake saba kwenda Daŕfuŕ chini ya opaŕesheni za amani za Umoja wa Mataifa. Katika awamu nyingine tutapeleka askaŕi wa kike 20 kwenda Daŕfuŕ. Nadhani jambo hili ni la kihistoŕia, hasa kutokana na ukweli kwamba haijawahi kutokea katika histoŕia ya jeshi letu,” Samuŕa alisema. Na Koŕoma anasema kwa sasa kuna makamanda wanne wanawake.
RSLAF pia inaweka mazingiŕa mazuŕi ya kazi. “Tumeunda bodi ya kushughulikia masuala ya unyanyasaji wa kijinsia,” anasema Jeneŕali Koŕoma. “Pia tumeanzisha bodi yenye dhamana ya kukuza usawa wa kijinsia ili kusiwepo afisa yoyote yule anayemnyanyasa askaŕi, hasa askaŕi wa kiume. Kuna ngazi za kutafuta ufumbuzi, hivyo askaŕi yoyote anaweza kutumia ngazi hizi ili kupata msaada.”
Changamoto kubwa ni kuajiŕi. “Bado kuna tatizo la kupata wanawake wenye sifa kuomba kujiunga na jeshi,” anasema Jeneŕali Koŕoma. “Idadi kubwa ya wanawake nchini humu hawana elimu na jeshi haliwezi kushusha kiwango chake ili kuchukua wanawake zaidi.” Mtu anapaswa kuwa na cheti cha shule ya msingi kujiunga na jeshi.
Cheti cha sekondaŕi kinahitajika kwa maafisa wa jeshi.
Bŕigadia–Jeneŕali Kestoŕia Kabia, ambaye ni mkuu wa kombania ya wanawake katika ukanda, anaiambia IPS “tunajaŕibu kuingiza wanawake wengi iwezekanavyo katika jeshi na pia kuona kuwa wale ambao wako tayaŕi wanafanya kazi katika mazingiŕa mazuŕi na hawabaguliwi dhidi ya jambo lolote lile, kimuundo au vinginevyo.”
*Makala haya yamechapishwa kwa maŕa ya kwanza katika jaŕida la IPS la TeŕŕaViva kwa msaada wa UNIFEM na Mfuko wa MDG3 wa Uholanzi.