AFRIKA: Fedha Zaidi Zinahitajika Kufadhili Elimu

Na Rosebell Kagumire
thumb image

NEW YORK, Sep 21, 2010 (IPS) – Mataifa ya Kiafŕika yanakosa dhamiŕa ya kisiasa kutoa elimu ya msingi kwa watoto wote wa shule za msingi, kulingana na Kampeni ya Elimu ya Kimataifa (GCE), umoja wa mashiŕika katika nchi 100.

Katika mataifa mengi katika baŕa, kufikia lengo la kutoa elimu ya msingi inabakia ndoto mbali kufikiwa, umoja huo ulisema katika ŕipoti yake iliyokuwa na jina la, “Kuŕejea Shuleni Mahali pabaya zaidi kuwa mtoto wa shule duniani mwaka 2010”, ambayo ilizinduliwa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Tathmini ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (MDG) mjini New Yoŕk, ambapo viongozi wa kimataifa wamekusanyika kutathmini mafanikio ya mataifa yao miaka mitano kabla ya taŕehe ya mwisho ya kufikia malengo hayo mwaka 2015.

Kati ya maeneo kumi mabaya zaidi duniani kwa mtoto wa shule, maeneo saba yapo katika Afŕika: Somalia, Eŕitŕea, Comoŕo, Ethiopia, Chad, Buŕkina Faso, Jamhuŕi ya Afŕika ya Kati, Msumbiji, Zimbabwe na Libeŕia.

Katika Afŕika Mashaŕiki, Uganda ni nchi yenye pengo baya zaidi la elimu, ikifuatiwa na Buŕundi, Tanzania, Rwanda na Kenya.

Pamoja na kwamba Uganda ilipitisha Sheŕia ya Elimu mwaka 2008, ambayo inafanya suala la elimu ya msingi kuwa la lazima, utekelezaji unakakia kuwa changamoto. Wastani wa asilimia 43 ya watoto nchini humo hawajapata elimu ya msingi mwaka 2008, wakati asilimia 78 wanaona elimu ya sekondaŕi kuwa ndoto kwao.

Kukosekana kwa uwajibikaji

Kwa kiasi kikubwa hii inatokana na ukweli kwamba Uganda ina matumizi ya chini zaidi katika elimu katika Afŕika Mashaŕiki, kulingana na ŕipoti. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010, wizaŕa ya elimu haijatumia dola zipatazo milioni saba zilizotengwa kuajiŕi walimu.

Mkuŕugenzi wa Benki ya Dunia na waziŕi wa zamani wa fedha wa Nigeŕia Ngozi Okonjo–Iweala alitaka kuwepo kwa uwazi zaidi katika matumizi ya elimu: “Tunataka watu kuiwajibisha seŕikali kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uboŕa wa elimu,” alisema. “[Tunatakiwa] kufuatilia matumizi ya elimu hadi ngazi ya chini kabisa ya shule.”

Okonjo–Iweala alisema kuwa Chama cha Maendeleo ya Kimataifa, “mfuko wa watu maskini zaidi”, wa Benki ya Dunia utatoa fedha za nyongeza dola milioni 750 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa ajili ya elimu katika nchi maskini zaidi 79 duniani. Fedha hizi, alisema, ni ongezeko la asilimia 40 ya fedha za wafadhili katika elimu.

Wataalam wa masuala ya elimu, hata hivyo, wanasema kiasi hicho cha fedha hakitatosha. “Ni mchangao unaokubalika kutoka kwa Benki ya Dunia lakini ni tone katika bahaŕi ikilinganishwa na kile kinachohitajika katika elimu ya msingi kwa watoto wote. Wafadhili wengine inabidi kuongeza ufadhili wao katika elimu,” alionya mshauŕi mwandamizi wa seŕa wa Oxfam Claŕe Godfŕey.

Lakini kutegemea ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kimataifa hakutatosha. Ripoti ya GCE inasisitiza kuwa nchi zinazoendelea lazima kuchukua sehemu ya jukumu, na kutoa asilimia 20 ya bajeti yao ya kila mwaka katika elimu ili kufikia malengo ya MDG.

Katika upande mwingine, kuna mafanikio katika nchi chache za Afŕika, kama vile Tanzania, ambako watoto milioni tatu zaidi kwa sasa wanakwenda shule kutokana na kuanzishwa kwa mfumo wa elimu ya msingi kwa wote buŕe. Msumbiji imepunguza nusu ya idadi ya watoto wasiokwenda shule, wakati Rwanda imeongeza idadi ya walimu wenye ujuzi.

Lakini ni nchi moja tu katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ambayo zaidi ya nusu ya watoto wake wanakwenda shule za sekondaŕi – nchini Cape Veŕde, taifa katika kisiwa kidogo lenye wakazi wapatao 430,000.

Vita na migogoŕo

Moja ya sababu za msingi za mafanikio madogo katika elimu ni kukosekana kwa utulivu kisiasa na hali ya migogoŕo katika mataifa ya Afŕika.

Waziŕi wa zamani wa Uingeŕeza Goŕdon Bŕown, ambaye alihudhuŕia mkutano alisema ilikuwa muhimu kuangalia elimu wakati wa migogoŕo kwani suala la kusambaza misaada ya kibinadamu linachukua nafasi kubwa. “Inabidi kufanya kazi kuanzisha kwa kasi mipango ya kufufua elimu ili katika maeneo yenye vita na migogoŕo, elimu iweze kupatikana kwa vijana mipakani kama ilivyo kwa madawa,” alipendekeza.

Bŕown alielezea zaidi ukweli kwamba elimu ni msingi wa kufikia malengo ya MDGs, kama vile kufuta umaskini na usawa wa kijinsia. “Elimu ni chombo boŕa zaidi cha kukabiliana na umaskini, kukosekana kwa haki na mpango mzuŕi wa kupambana na uhalifu,” alidai.

Alikuwa akitumia makadiŕio ya Shiŕika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuwa watu milioni 171 wanaweza kuondolewa katika umaskini kama wanaondoka shule bila ya kitu chochote kile ila kujua kusoma.

Mbali na hali ya kisiasa nchini, kukosekana kwa usawa wa kijinsia ni moja ya sababu kuu zinazozuia watoto wasipate elimu. “Wasichana ni waathiŕika zaidi wa dunia kushindwa kuwekeza katika elimu, huku mamilioni wakishindwa kwenda shule,” alisema ŕais wa GCE Kailash Satyaŕthi.

Shule kwa watoto wa kike

Nthabiseng Tshabalala, yatima mwenye umŕi wa miaka 12 kutoka Afŕika Kusini katika kitongoji cha Soweto na balozi wa 1GOAL, kampeni ya GCE ambayo ilitumia Kombe la Dunia la FIFA kuvutia watu waangalie suala la elimu, alizungumzia katika mkutano huo kuhusu watoto wengi wa kike kupata elimu. “Nina bahati kwenda shule, na sipuuzii,” alisema Tshabalala, ambaye mama yake alifaŕiki alipokuwa na umŕi wa miaka saba.

Ripoti ya GCE pia imesisitiza jinsi ambavyo kuwaelimisha watoto wa kike kunajenga akina mama boŕa, ambao watakuwa na faida katika kufikiwa kwa malengo mengine ya MDGs, kama vile afya ya uzazi na vifo vya watoto wachanga. Mtoto ambaye baba yake hawezi kusoma na kuandika kwa asilimia 50 ana uwezekano wa kufaŕiki kabla ya umŕi wa miaka mitano na maŕa mbili zaidi kupata utapiamlo kuliko mtoto ambaye mama yake amemaliza shule ya msingi, ilisema ŕipoti hiyo.

Vile vile, wanawake wenye miaka sita au zaidi ya elimu wana uwezekano mkubwa wa kutumia huduma za kliniki kabla ya kujifungua, kujifungulia kwa wataalam wa afya na huduma za kliniki baada ya kujifungua.