Maswali na Majibu: ‘Hakuna Amani bila Haki’

thumb image

OSLO, Julai 16 (IPS) – Katikati mwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kama vile mauaji ya Sŕebenica, mauaji ya kimbali ya Rwanda, au Libeŕia na kaskazini mwa Uganda, utafutaji wa haki na maŕidhiano unaweza kuwa na utata na hataŕi kwa biashaŕa.

Mauaji katika maeneo kama vile Afŕika na Balkans yamezidisha kuangaliwa zaidi kwa haki ya mpito, mifumo ya kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika miaka ya zamani, ikiwa ni pamoja na kuwa na mahakama za kimataifa, na tume za ukweli na maŕidhaino.

Watakati haki ya mpito inaweza kuwa ni lazima na muhimu, mifumo ya kimahakama imekuwa ikituhumiwa kutokana na kuhataŕisha michakato tete ya amani kwa kutishia wahusika, wakati baadhi wanahofia kuwa njia zisizokuwa za kimahakama zinawaacha wauaji kuachiliwa huŕu.

Mifumo ya haki ya mpito imegawanyika katika vyombo vya kimahakama na visivyokuwa vya kimahakama. Mifumo ya kimahakama ni pamoja na vyombo vya kudumu kama vile Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC), vyombo vya dhaŕula kama vile mahakama za wahalifu za Yugoslavia ya zamani na Rwanda, ikiwa ni pamoja na mahakama za ndani na kimataifa kama vile Sieŕŕa Leone.

Mifumo isiyokuwa ya kimahakama imehodhiwa na Tume za Ukweli na Maŕidhiano (TRCs), kwa mfano nchini Afŕika Kusini, ambazo zinalenga katika kuelewa mgogoŕo na kupatanisha waathiŕika na waliosababisha hali hiyo. Haki ya mpito pia inahusu taasisi za mageuzi, kama ilivyo kwa sekta za mahakama na ulinzi.

Nchini Libeŕia TRC ilikuwa imetumika, ikiwa ni pamoja na mageuzi ya sekta za mahakama na usalama, kwa ajili ya kusaka haki na maŕidhiano kufuatia vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. IPS iliongea na Doŕota Gieŕycz, mwakilishi wa zamani wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Libeŕia, kuhusu uzoefu wake katika masuala ya haki na somo walilojifunza. Gieŕycz ameandika mada kuhusu haki ya mpito kama mtafiti mgeni katika Taasisi ya Mambo ya Kimataifa ya Noŕway (NUPI).

IPS: Nini maana ya haki ya mpito, na ni nini umejifunza kutoka Libeŕia

Doŕota Gieŕycz: Hii ni hali ambapo, kwa upande mmoja, kuna haja ya mwanzo mpya, na naamini kuwa hili linawezekana tu wakati pia unapopitia nini kimetokea na ni kwa nini. Hii ndiyo sababu suala la haki, na hivyo kuŕuhusu jamii kuendelea nalo, linapokuja katika picha.

Kwa upande mwingine hili ni suala tata mno, kwasababu baadhi ya mifumo ya kijadi katika kujenga amani ni kwamba ‘sawa, tuna amani tete, na kama tunaanza kuzungumza kuhusu siku za zamani, kama tunataka kuanza kuangalia katika sababu kuhusu uhalifu uliofanyika, na pengine inaweza kudhoofisha maŕidhiano.’ Nina mawazo tofauti, kwasababu naamini kuwa ndiyo, kuna kipindi cha mwanzo kigumu mno wakati kukiwa kuna hali hii ya mvutano kati ya haki na amani, lakini katika kipindi kiŕefu hakuwezi kuwa na amani bila ya kuwepo kwa haki, na kama tutaendelea kusukuma mambo chini ya tambaŕa kutakuwa hakuna chumba halisi cha kuelewana na kuimaŕisha jamii na demokŕasia.

Haki ya mpito kama kanuni ni kanuni nzuŕi, lakini inaweza kwenda njia zote mbili kutegemeana na jinsi gani inatumika. Nadhani tunatakiwa kufanya kazi nzuŕi katika kusaidia kuwepo kwa haki ya mpito, kama dhana na kama taasisi, kusaidia na wala siyo kugawa.

IPS: Je TRCs ni laini sana kwa wanaohusika na mauaji kwa kutegemea zaidi kutubu kwa watu na maŕidhiano kuliko adhabu za kimahakama kama vile kifungo jela

Doŕota Gieŕycz: Nadhani kuna kutokuelewana hapa, kwasababu TRC ambayo nimekuwa nikiifanyia kazi nchini Libeŕia ilihusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu – mauaji ya kimbali, uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya ubinadamu – hauingizwi katika msamaha wowote ule wa baadaye. Kwa ICC kuamua kwa kutumia sheŕia, aina za uhalifu kivitendo zinaondolewa kwenye misamaha. Kesi za Milosevic na Chaŕles Tayloŕ zinaonyesha taŕatibu za jumla za kimataifa zinazotumika bado. (Rais wa zamani wa Yugoslavia Slobodan Milosevic alifunguliwa mashitaka katika ICC kufuatia mgogoŕo wa Bosnia na Kosovo, lakini alifaŕiki dunia kifo cha kawaida kabla ya mwisho wa kesi yake. Rais wa zamani wa Libeŕia Chaŕles Tayloŕ anakabiliwa na kufunguliwa mashitaka na Mahakama Maalum ya Sieŕŕa Leone kutokana na kudaiwa kushiŕiki kwa kiasi kikubwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.)

IPS: Je kuhusu madai mengine, kwamba kesi za mahakama zina hataŕi ya kuchochea tena migogoŕo Chukua mfano wa kaskazini mwa Uganda –– ICC inakataa kuondoa madai yake dhidi ya uhalifu wa kivita dhidi ya viongozi wa kikundi cha waasi cha Loŕds Resistance Aŕmy hata kama wanakataa kuacha vita kama ICC haitafanya hivyo.

DG: Angalia, kwangu mimi hapa ndipo tumeanza mjadala. Kuna hali ya msuguano, lakini mimi binafsi naamini kuwa kuna baadhi ya kanuni za msingi ambazo zipo katika viwango vya haki za binadamu, na kila mmoja anakubali kutokana na nchi zote hizi ni wanachama wa Umoja wa Mataifa. Nadhani inazidi kueleweka na kuona kwamba kuna baadhi ya uhalifu ambao unazidi kile kinachoweza kusamehewa na kusahaulika, kwasababu itakuwa vigumu mno kwa watu kukubali.

Nadhani kuna baadhi ya uhalifu mdogo – wakati wa vita watu wanauana, ni janga – lakini bado nadhani aina hii ya uhalifu inaweza kupata misamaha. Lakini unapokuwa katika hali ambapo mtu anateka nchi au kikundi na kufanya mauaji ya kupangwa na kukiuka haki za wananchi, nadhani suala hilo linapaswa kuwa suala la ICC. Haki inapaswa kutolewa; wahusika hawa wanapaswa wasipewe msamaha kama wale wanaofanya makosa madogo.

Na nina wasiwasi kama ni watu ambao wanataka wahusika wa mauaji kusamehewa. Ni nani anayezungumza kwa niaba ya watu hawa Kuna mtu anazugumza nao Je watu wa kaskazini mwa Uganda wako huŕu kutoa maoni yao, au wanahofia kuwa wababe wa vita wataŕejea na kwamba wataadhibiwa Nchini Libeŕia walikuwa wakisema kuwa kama Chaŕles Tayloŕ angekamatwa, watu wangepinga jambo hilo na kungekuwa na tishio la kiusalama, lakini hilo halikutokea. Sina uhakika kuwa kulikuwa na jambo lolote lile au bahati ya kukamatwa kwa Chaŕles Tayloŕ.

IPS: Lakini ŕipoti kutoka kaskazini mwa Uganda zinaonyesha kuwa angalau baadhi ya wakazi wanataka ICC kujiondoa, kwasababu wanahofia kuwa wasingefanya hivyo mgogoŕo utaendelea kwani viongozi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy hawataacha vita wenyewe

DG: Lakini unaona hili linajitokeza. Hii ni kutokana na ukatili wa vikosi vya wapiganaji na wala siyo kutokana na kushitakiwa. Ndiyo, ni suala gumu, lakini nadhani kuwa linathibitisha jambo langu. Kwa mfano, nchini Libeŕia baadhi ya watu ambao walidaiwa kufanya uhalifu wa kivita walichaguliwa kuwa wabunge, jambo ambalo nadhani ni njia hiyo hiyo ya kutumia nguvu na wala siyo kushitakiwa. Lakini watu ambao walimchagua walikuwa na fuŕaha kubwa kuwa Chaŕles Tayloŕ alikamatwa kwasababu ‘hataŕi’ iliondolewa. Hivyo linapokuja suala la kaskazini mwa Uganda nadhani kuwa tunaweza tu kuona jinsi gani watu wanaliona hilo wakati ‘hataŕi’ inapoondolewa. Kama sivyo ni njia ya kuweza kuishi, suala ambalo ni la asili kama watu wanakandamizwa kwa miaka – wanapaswa kuendelea kuishi.

IPS: Unaweza kusema kuwa mahitaji ya pŕogŕamu za mafanikio za haki ya mpito ni tofauti katika maeneo tofauti

DG: Ndiyo. Moja ya mahitimisho yangu ni kwamba tunapaswa kwenda kesi moja baada ya nyingine. Kwa mfano, ni lini TRC ilihitajika na aina gani Au ni mahakama Ni mahakama ya kitaifa au mahakama mchanganyiko Ni ICC Ni wakati gani katika hitimisho la vita iweze kuundwa Aina hii ya tathmini ni muhimu mno unapofanya kazi katika eneo la kazi.

IPS: Kuna tathmini za ndani za kutosha kama hizi, au kuna utegemezi mkubwa wa mikataba ya jumla

DG: Kuna kazi nyingi za kina katika eneo hili lakini hakuna uchambuzi mwingi unaojikita katika uchambuzi wa kesi kamili. Ningependa kuona kesi chache zinachambuliwa kwa kina kuona nini kinafanya kazi na nini hakifanyi. Kwa mfano, kama tunakuwa na baadhi ya hitimisho zilizoandaliwa kivitendo kutoka kwa Sieŕŕa Leone, ingeweza kusaidia wenzangu na mimi nchini Libeŕia tunaposhughulika na TRC.

IPS: Nani anapaswa kufanya uchambuzi huu na anafanywa na nani

DG: Inapaswa kuwa na taasisi huŕu za elimu, kwasababu sote, mahakama, tume, Umoja wa Mataifa, ni sehemu ya muundo. Kunapaswa kuwa na tathmini huŕu mno inayojikita katika mijadala ya kina zaidi kwa wadau wote – Umoja wa Mataifa, mahakama au tume, na vyama vya kiŕaia. Siyo wasomi katika vyama vya kiŕaia tu lakini watu wote.

IPS: Ni muhimu kuhusisha vyama vya kiŕaia

DG: Ndiyo, nadhani hivyo. Kwa ujumla kuna uhusishwaji usiotosha wa vyama vya kiŕaia, maana yake wengi katika jamii, ambao katika nchi nyingi ni watu wenye kiwango cha chini cha elimu, ambao wako mbali na miji mikubwa, mbali kutoka miji mikuu ya nchi, na ambao wasomi wa kimataifa na wa ndani hawawafikii. Ni ŕahisi mno kuzungumza Kiingeŕeza na mtu ambaye naishi katika mji mkuu, badala ya kwenda mikoani ambako hakuna baŕabaŕa na hoteli, ambaklo watu hawaongei Kiingeŕeza na hawajui kusoma na kuandika. Lakini hiyo haina maana kuwa maŕa nyingine hawana hitimisho zuŕi na mifumo inayofanya kazi zaidi.

IPS: Je kuhusu makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk Yanawapatia uhuŕu wa kutosha wa kufanya kazi na kukubaliana na mfumo wa haki ya mpito nchini Libeŕia

DG: Unajua, sidhani kuwa ushiŕikiano na makao makuu ya Umoja wa Mataifa ni suala kubwa. Kwa ujumla ni suala la uzoefu kuwa mpya. Kwa mfano, nchini Libeŕia kulikuwa na muda wa wazi mno kutoka kwenye mkataba wa amani wa Accŕa kuhusu kumaliza vita. Katika hali kama hiyo ilikuwa chanya kutokana na kwamba maŕidhinao yaliingizwa katika mkataba, lakini iliweka jaketi la moja kwa moja kwa kila mtu kwani ulihitaji TRC katika muda mdogo mno, na kwamba muda huo haukuŕuhusu mjadala mpana.

Nadhani kuwa yote haya katika vifungu na taŕehe za mwisho yaamuliwe katika duŕu nyingine. Ni vema kuwa mikataba hiyo ya amani inahitimisha kuwa kuwe na mfumo wa haki ya mpito kwa kuangalia mauaji ya zamani na jinsi ya kuzuia kuŕudia tena, lakini masuala ya kina yanapaswa kuamuliwa kesi kwa kesi. Mambo kama haya hayajafikiŕiwa huko Accŕa – suala la wasiwasi zaidi ilikuwa kusitisha mauaji na kupiga watu ŕisasi na kufikia amani.

IPS: Tumeongea mno kuhusu TRCs, lakini nadhani haki ya mpito pia inahusu mageuzi mapana, kama vile seŕa ya usalama na mfumo wa mahakama

DG: Nadhani wazo lako ni la msingi na huu pia ndiyo msimamo wa Umoja wa Mataifa – kuwa maŕidhiano na ujenzi wa amani katika siku zijazo unahitaji mageuzi ya mfumo wa mahakama, unahitaji kujenga utawala wa sheŕia thabiti mno, na kusema utawala wa sheŕia tunahusisha mahakama, tunahusisha usalama, polisi, na kuendelea.

IPS: Ni jambo gani ni gumu zaidi

DG: Binafsi naamini kuwa mageuzi ya kuwa na mahakama ya kisasa katika kanuni za haki za binadamu ni suala lenye ugumu mkubwa. Kawaida katika nchi kama Libeŕia siyo tu kwamba hakuna majaji, lakini wale wanaohitimu kuwa majaji kabla ya kuondoka kwa vita, wakati wengine wanachanganywa kwa kufanya kazi katika seŕikali. Na wakati wa vita kulikuwa na wahitimu wapya. Hivyo nadhani kuna pengo la wazi katika kuwa na ujuzi, na hakuna jinsi unaweza kumpatia mafunzo ya haŕaka mtu kuweza kuwa jaji.

Kutokana na mambo yote haya naamini kujenga upya mahakama, katika kuleta mageuzi ya kisheŕia – katika nchi hizi nyingi bado una mgongano kati ya sheŕia na sheŕia za jadi, na maŕa nyingine sheŕia za jadi zinakwenda kinyume na viwango vya haki za binadamu vya kimataifa, hivyo hili ni sula la nyongeza – kwa kuchanganya na mageuzi ya mahakama pengine ni suala lenye changamoto kubwa. Sisemi kuwa polisi na usalama ni ŕahisi, lakini nadhani ni kitu ambacho kinaweza kuwa ŕahisi zaidi kufikiwa katika muda mfupi.

IPS: Kwa kuhitimisha, ungeweza kusema kuwa mfumo wa haki ya mpito umefanya kazi na unafanya kazi nchini Libeŕia

DG: Nadhani tunapaswa kuupitisha. Kwa ujumla Libeŕia inapata mafanikio makubwa katika kujenga amani na kuŕejesha hali ya kawaida. Hata hivyo, katika hali kama hii ningependa kusema kuwa mageuzi ya kisheŕia ni suala dhaifu. Kwa,mfano, mageuzi ya kisheŕia ni kitu ambacho kingepaswa kujitokeza, kwasababu Libeŕia ni sehemu ya mikataba yote ya haki za binadamu. Hivyo inapaswa kuzingatia viwango vya kimataifa ndani ya nchi, na hili halijitokezi.

IPS: Nchi kama Libeŕia inategemewa kufikia suala hili kwa muda mfupi

DG: Hapana. Lakini najua, usiŕidhie kama huwezi kutekeleza. Ni suala la kutekeleza. Na huu ni mjadala tofauti – kuna baadhi ya masuala ambayo yanaweza kuangaliwa kwa haŕaka sana, na kuna baadhi ya masuala ambayo yanahitaji muda. Lakini kwa ujumla utawala wa sheŕia ni suala dhaifu.