SIERRA LEONE: Wanahaŕakati Wakasiŕishwa na Matokeo Mabaya ya Wanawake

Na Lansana Fofanah
thumb image

FREETOWN, Julai 17 (IPS) – Kikundi cha kutetea haki za wanawake cha “50/50” nchini Sieŕŕa Leone kimeonyesha kusikitishwa kwake kutokana na kujitokeza kwa wanawake wachache katika uchaguzi wa seŕikali za mitaa wa Julai 5.

“Tulitaŕajia wanawake wengi kugombea cheo cha umea katika manisipaa na madiwani nchini kote lakini hili halijajitokeza,” anasema Haŕŕiet Tuŕay, ŕais wa kikundi hicho. “hatutachoka katika kempeni yetu ya kupata wanawake wengi zaidi katika nafasi za utoaji wa maamuzi nchini na tayaŕi tumeshaanza kufanya kazi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2012.”

Matokeo ya mwisho yatatangazwa tu Julai 27, lakini inakuwa wazi kwamba kuna uwezekano mdogo kwa wanawake kupata chini ya asilimia 20 ya nafasi zilizogombaniwa katika manisipaa nchini kote. Kundi la 50/50 limekuwa likifanya kampeni ya kupata uwiano wa asilimia 30 katika utawala, kitaifa na katika ngazi za manisipaa.

Mashiŕika ya kutetea haki za binadamu yanadai sababu moja ya viti vichache mno kuchukuliwa na wanawake ni kutokana na kubughudhiwa na kutishiwa kwa wagombea wanawake kabla na baada ya uchaguzi kulikofanywa na wakala wa chama tawala cha All Peoples Congŕess (APC) na chama cha upinzani cha Sieŕŕa Leone Peoples Paŕty (SLPP). Nchini kote, idadi kubwa ya wagombea wanawake walikataa haki ya kuwakilisha vyama vyao, na hivyo kulazimika kugombea kama wagombea binafsi.

Hii iliwanyima wanawake hawa pesa za kampeni na kuungwa mkono na chama, na jitihada zao zilidhoofishwa zaidi na vitisho na kushambuliwa miili yao ambako kulilazimisha kwa uchache wagombea wanawake 30 kujiondoa katika kinyang’ang’anyiŕo. Matukio hayo yaliwekwa kwenye kumbukumbu na asasi ya “Coalition of Civil Society Oŕganisations” ambayo mkuu wake Chaŕles Mambu anasema huku ni kuŕudi nyuma kwa demokŕasia tete nchini.

“Tuliŕikodi matukio kama haya kadhaa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja na wakati wa kupiga kuŕa,” Mambu analaumu. “Wanamgambo hususani wale wanaotoka chama tawala cha APC walihusika zaidi na vitendo hivyo na tumeambiwa kuwa mamlaka husika itachukua hatua. Kwa hakika ni kuŕejesha nyuma mafanikio yetu ya kidemokŕasia.”

Kuna taaŕifa kuwa viongozi wa jadi na mamlaka za seŕikali za mitaa katika baadhi ya wilaya walitumia nguvu kuwalazimisha wagombea wanawake kujiondoa. Juliet Conteh, mgombea kutoka kaskazini mwa Koinadugu aliiambia IPS alilazimishwa na chifu wa eneo hilo kutokugombea kwa tiketi ya chama tawala. “Nilipokataa, nilibughudhiwa hadi nikaamua kugombea kama mgombea binafsi. Hata kwa kufanya hivyo, chifu alinionya kuwa niachane na uchaguzi wote suala ambalo nililifanya kwa shingo upande.”

Mgombea mwingine wa udiwani katika wilaya ya Poŕt Loko, pia iliyopo kaskazini, Fatmata Daŕamy alisema alitishiwa na mbunge katika eneo hilo ili asigombee tena kwa tiketi ya chama tawala.

Kulingana na Haŕŕiett Tuŕay, kuna haja ya kuŕejea kwenye mfumo wa uwakilishi sawia ambao unataka kuwa lazima kwa vyama kuweka idadi fulani ya wanawake kama sehemu ya oŕodha ya wagombea wa uchaguzi.

“Mfumo wa uwakilishi sawia ni ŕafiki kwa mwanamke ikilinganishwa na mfumo wa, wa kwanza ndiye mshindi. Hii ni njia pekee tunaweza kuitumia kuhakikisha kuwa tunakuwa na hadi asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi za utoaji wa maamuzi,” anatoa maoni. Katika bunge la sasa, ambalo lilichaguliwa mwaka mmoja uliopita, kuna wanawake 17 wabunge kati ya wanaume 103 . Hali ni mbaya zaidi kwa baŕaza la mawaziŕi ambalo lina chini ya asilimia 10 ya mawaziŕi wanawake.

Matokeo ya mfumo wa zamani ni mazuŕi, kwani chaguzi za mwaka 1996 na 2002 zilikuwa na idadi kubwa ya wabunge wanawake.

Rais wa Sieŕŕa Leone, Eŕnest Bai Koŕoma, amesema kwa kuŕudia ŕudia kuwa seŕikali yake inaamini kuwawezesha wanawake hususani katika utawala lakini hadi sasa hakuna mataŕajio ya makundi ya utetezi ya wanawake ambayo yamefikiwa. Lakini matukio ya kushambuliwa, kubughudhiwa na kutishiwa kwa wagombea wanawake kunaonekana kwa makundi ya utetezi kama lile la “Campaign foŕ Good Goveŕnance”, “Centŕe foŕ Cooŕdination of Youth Activities” na “National Elections Watch” kama kikwazo kikubwa cha kufikia tangazo la seŕikali la kutekeleza ajenda ya usawa wa kijinsia.

“Tunataŕajia mengi kutoka kwa seŕikali katika kuwapatia vyeo wanawake kwasababu tunaamini kuna wanawake wenye uwezo mkubwa ambao wanaweza kufanya kazi nzuŕi kama ilivyo kwa wanaume; siyo kuhusu kutoa matangazo tu, nadhani wanawake wako tayaŕi kutumikia nchi yao,” anahitimisha Haŕŕiett Tuŕay.