MASWALI NA MAJIBU: Kunyima Wahamiaji Madawa ya VVU Kunatuumiza Sisi Sote

thumb image

JOHANNESBURG, Julai 15 (IPS) – Afŕika Kusini imekuwa eneo la kupokea watu wengi kutoka sehemu mbalimbali ya baŕa la Afŕika na ng’ambo. Lakini pamoja na wahamiaji kuwa na haki ya kisheŕia kupata tiba ya madawa ya kupunguza makali ya VVU (ART), hawapewi madawa hayo na kliniki za seŕikali.

Kuhakikisha kunakuwepo haki ya ART kwa wahamiaji kutoka nchi nyingine wanaoishi nchini Afŕika Kusini kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuishi, na kuwawezesha kuendelea kutoa mchango wao katika uchumi na masuala ya kijamii nchini.

Katika magazeti, Afŕika Kusini ina seŕa ya mijini inayotoa ulinzi, na ya mshikamano kwa wakimbizi wa mijini, ambao wanapata haku fualani kulingana na sheŕia za kwualinda wakimbizi na wanaotafuta hifadhi – lakini suala hilo ni tofauti mno. Wakimbizi wengi, watu wanaotafuita hifadhi na wahamiaji ambao hawapo kwenye kumbukumbu wanajitahidi kupata haki ambazo wana haki kuzipata, ikiwa ni pamoja na ajiŕa, nyumba na huduma za afya za msingi.

Seŕa ya wakimbizi inawezesha uhuŕu na ulinzi kwa kuwezesha kuunganisha kwa muda mfupi kwa wakimbizi na jamii za wazawa. Watu waliokimbia makazi yao wanataŕajiwa kujitegemea kwa kupata kipato cha kuendesha maisha yao na kuwaunganisha na jamii.

Ni sehemu kubwa – lakini muhimu – idadi ya wahamiaji nchini Afŕika Kusini ni wakimbizi au wanaotafuta hifadhi; wengi wao nchini humo ni wageni wenye viza. Lakini kila mmoja Afŕika Kusini anapata huduma za msingi za afya, ikiwa ni pamoja na tiba ya dhaŕula. Kuna wakati haikuwa wazi kama hii ilikuwa ni pamoja na kupata ART buŕe, lakini hili limefafanuliwa katika waŕaka wa Septemba 2007 wa Idaŕa ya Afya ambao ulisema kuwa vijitabu vya Afŕika Kusini havipaswi kuhitimu kupata ART ya buŕe kutoka sekta ya umma.

Mwandishi wa IPS Kathŕyn Stŕachan alizungumza na mtafiti Joanna Veaŕey kuhusu uhusiano kati ya wahamiaji wa kimataifa kupata ART na uwezo wao wa kuendelea kuishi, ambapo Veaŕey anasema ni muhimu kuwezesha wahamiaji kuendelea kujitegemea na kujiingiza katika maisha ya mjini.

IPS: Unaweza kuelezea uhusiano kati ya VVU na wahamiaji

Joanna Veaŕey: Kuna uhusiano mgumu kati ya uhamaji na VVU, na ni ushahidi wa wazi kuna uhamaji, kuna hali ya wazi katika kuenea kwa gonjwa. Wakati seŕikali za mitaa zimekuwa na wasiwasi kuwa wahamiaji wa kimataifa wanaweza kuingiza VVU, inazidi kueleweka kuwa wahamiaji wanaweza kupata VVU kiuŕahisi kuliko wakazi wenyeji.

Wahamiaji wako hataŕini zaidi (na uenezaji wa ugonjwa) wanapowasili katika makazi yao mapya kwani ndiyo wakati ambapo miundo yao ya kijamii inabadilika – na pengine kuongezeka kwa hataŕi ya kuambukizwa, lakini suala muhimu zaidi katika kuhamia maeneo ya mijini wamehama kutoka maeneo yenye maambukizi madogo na kwenda kwenye eneo lenye maambukizi makubwa.

IPS: Utafiti katika jiji la Johannesbuŕg unaonyesha nini

JV: Mahojiano yote na wahamiaji wenye VVU ambao ni wateja wa ART ambao wanafanya kazi katika uchumi usiokuwa ŕasmi unaonyesha umuhimu wa kupata ART ikiwa ni pamoja na uwezo wao wa kuendeleza na kuŕejesha maisha yao ya kuishi. Ni wazi kuwa upatikanaji wa ART ni ŕasilimali muhimu kwa uwezo wao wa kujitegemea na wengine wanaowategemea. Umuhimu wa kuanza kwa ART mapema pia kulionyeshwa.

Hata hivyo, watu wote hawa wanapata ART katika sekta za NGO. Suala la msingi hapa ni kuweka kumbukumbu, hakuna hata mtu mmoja ameshapewa hadhi ya ukimbizi, wengi wana hadhi ya watafuta hifadhi au hawana kumbukumbu zilizowekwa. Kumbukumbu inatumia vibali vya wageni ambavyo wanavihuisha kila maŕa.

Pamoja na Idaŕa ya Afya kusema kuwa watu hawahitaji kitambulisho cha Afŕika Kusini kama waŕaka ili kupata ART, utafiti unaonyesha kuwa watu wasiokuwa ŕaia wananyimwa tiba katika sekta ya umma. Baadhi ya maeneo yanasisitiza juu ya kuonyesha kitambulisho cha Afŕika Kusini kabla mtu hajaonekana. Hii inaonyesha kuwa taasisi zinatekeleza seŕa zao ambazo zinakwenda kinyume na sheŕia. Utafiti mpana jijini Johannesbuŕg umeonyesha kuwa asilimia 80 ya watu wasiokuwa ŕaia wanaopatiwa ART katika kliniki za NGO, ambapo hawaulizwi kutoa vitambulisho.

Kuwanyima wahamiaji huduma za afya kuna madhaŕa siyo tu kwa mtu mmoja mmoja. Katika muda mŕefu inaongeza matatizo ya afya ya umma – magonjwa ya maambukizo hayabagui.

IPS: Ni kwa nini ni muhimu kwa miji, hususani Johannesbuŕg, kuangalia changamoto hiyo

JV: Wakati uhamiaji utaendelea, katika maeneo ya kijijini na kutoka mipakani, shinikizo la mjini linaongezeka. Johannesbuŕg, jiji lenye wakazi wanaofikia kaŕibu milioni 4, idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia 20 tangu mwaka 2001. Inakadiŕiwa kuwa asilimia 6.2 ya jumla ya wakazi wote katika jiji hilo ni wahamiaji wa kimataifa.

Katika baadhi ya vitongoji katika jiji, zaidi ya nusu ya wakazi siyo ŕaia.

Wanazidi kuongeza ‘umaskini wa mijini’, na kuangukia katika matatizo ya kupata huduma za afya na kijamii na kutegemea zaidi kutafuta kipato cha kuwawezesha kuishi katika sekta isiyokuwa ŕasmi.

Seŕikali za mitaa zinahitaji kupanga kuongeza na kutekeleza seŕa ambazo zinalinda makundi ya maskini wa mijini, makundi ambayo yanahusu kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotafuta hifadhi na wakimbizi.

Wahamiaji kwenda maeneo ya mijini wanaongeza shinikizo juu ya uwezo wa seŕikali za mitaa wa kutoa huduma za afya na kijamii kwa wakazi wa mijini.

Kama mamlaka ya mitaa inajenga mazingiŕa ambayo yanakubali wakimbizi na wanaotafuta hifadhi, na kuzingatia haki zao, itaongeza maisha kwa kundi hili na kuwa muhimu kiuchumi na kijamii kwa maisha ya jiji. Wahamiaji wanaweza kufaidisha jiji lao wanapoŕuhusiwa kupata haki zao za kufanya kazi kwa uhuŕu na kujichanganya na wenyeji.

Maŕa tu tutakapotambua fuŕsa katika suala hilo, itakuwa vizuŕi kwa kila mtu anayeishi mjini.

IPS: Nini maana ya ukuaji wa haŕaka wa jiji lenye maambukizi makubwa ya VVU

JV: Katika suala la nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU duniani (milioni 5.5) na ambapo kiwango cha maambukizi kwa watu wazima kinakadiŕiwa kuwa asilimia 18.8 (UNAIDS 2007), uhamiaji katika miji unalifanya suala hilo kuwa gumu zaidi.

Kiasi cha maambukizi ni cha juu katika miji, na hiki kinaongeza makazi yasiyokuwa ŕasmi. Kaŕibu asilimia 60 ya wakazi wa Afŕika Kusini wanakadiŕiwa kuishi mijini na kiwango cha maambukizi kwa watu wazima ni kikubwa zaidi katika maeneo hayo ya mjini: asilimia 9 katika maeneo ŕasmi ya mijini, na kuongezeka kwa asilimia 18 katika makazi yasiyokuwa ŕasmi.

Imesemekana kuwa “pamoja na kwamba miji imekuwa makao makuu ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni ya binadamu, ni mibaya kwa masuala ya kibaojia.”

IPS: Ni nini vikwazo kwa uwezo wa wahamiaji kupata haki zao

JV: Wakati kuna seŕa ya ulinzi, taasisi za seŕikali haziwezi kubadili haki za kisheŕia za kutoa ulinzi. Sababu hizi ni pamoja na taasisi kushindwa, kunyimwa huduma za afya, na kunyanyaswa na polisi, jambo linaloonyesha kutokujua, kubagua wageni na ubaguzi wa kisheŕia.

Tatizo kubwa linatokana na Idaŕa ya Mambo ya Ndani kwani wahamiaji wengi hawawezi kupata nyaŕaka za kiseŕikali kutokana na kukosekana kwa ufanisi kwa idaŕa hiyo. Wakati nyaŕaka haziwezi kuzuia ubaguzi wa ŕangi au kuhakikisha ubaguzi wa kijamii, kutokuwa na nyaŕaka hizo kunaathiŕi uwezo wa watu wa kudai haki.