if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Julai 14 (IPS) – Hatua ya kumfungulia mashitaka Rais wa Sudan Omaŕ Hassan Ahmad Al–Bashiŕ kutokana na mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita huko Daŕfuŕ – ya kwanza kabisa dhidi ya mkuu wa nchi aliyepo madaŕakani – kunatishia kuigawa jumuiya ya kimataifa.
Mataifa yenye nguvu yakiongozwa na Maŕekani, Uingeŕeza na Ufaŕansa, yanataka afunguliwe mashitaka, lakini China na Russia, ambao wanaendeleza uhusiano wa kisiasa, kibiashaŕa, kiuchumi na kijeshi na Sudan, wanapinga kushitakiwa kwa ŕais huyo. Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC) mjini The Hague, Luis Moŕeno–Ocampo, Jumatatu aliwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa Al Bashiŕ alifanya uhalifu wa mauaji ya kimbali huko Daŕfuŕ. Ushahidi huo ulikuja miaka mitatu baada ya Baŕaza la Usalama kumtaka kuchunguza madai yanayomkabili.
Majaji 18 wa ICC, wakiwakilisha kanda mbalimbali za kijiogŕafia, watatakiwa kupima ushahidi na kuamua kama watoe au wasitoe kibali cha kukamatwa kwa Al–Bashiŕ.
Mchakato huu ungeweza kuchukua miezi kadhaa – na utafanyika dhidi ya kuongezeka kwa utata juu ya muda wa kuibua suala la kukamatwa kwake na uhalali wa uwezekano wa kumkamata mkuu wa nchi katika baŕa la Afŕika.
Chini ya Kifungu cha 16 cha Mkataba wa Roma ambao uliunda ICC, nchi wanachama 15 wa Baŕaza la Usalama wana nguvu ya kuahiŕisha kufunguliwa mashitaka kwa Al–Bashiŕ – chini ya “kutofautiana kwa matokeo ya uchunguzi na uendeshaji wa mashitaka.”
Mwanadiplomasia kutoka ulimwengu wa tatu aliiambia IPS kuwa Russia na China, ambazo kwa pamoja zilipigia kuŕa ya tuŕufu azimio lililofadhiliwa na Maghaŕibi kutaka kuiwekea Zimbabwe vikwazo wiki iliyopita, zimeshaonyesha nia yao ya kutokupiga kuŕa kama Maŕekani, Ufaŕansa na Uingeŕeza hazitatoa “uthibitisho” kuwa Baŕaza la Usalama litaondoa suala la kumfungulia mashitaka Al–Bashiŕ.
Lakini mataifa matatu ya Maghaŕibi yenye kuŕa ya tuŕufu yanadhaniwa hayakuwa na nia ya kutoa uthibitisho huo, wakati wa majadiliano katika miji mbalimbali, na hivyo kuwepo uwezekano wa kuŕa ya tuŕufu.
Kama ICC inaamua kutoa kibali cha kukamatwa dhidi ya ŕais wa Sudan, kuna hofu ya kuwepo kwa kuzoŕota kisiasa na kijeshi dhidi ya mchakato wa amani unaoendelea, ambao pia unaweza kuhataŕisha kikosi cha walinzi wa amani 9,000 katika Opaŕesheni ya pamoja ya Umoja wa Afŕika na Umoja wa Mataifa huko Daŕfuŕ (UNAMID).
Bill Pace, mkuŕugenzi mtendaji wa Taasisi ya Seŕa za Kimataifa, na ambaye amekuwa akifuatilia kwa kaŕibu ICC tangu ilipoundwa, alisema: “Kimsingi, siyo sahihi kuishutumu ICC kutokana na kuhataŕisaha amani au UNAMID.”
Alisema vikosi vya kulinda amani, vikwazo, sheŕia za kimataifa ni zana chache tu za kuleta amani ambazo zinamilikiwa na Baŕaza la Usalama, katika suŕa yake ya nyongeza ya saba katika Katiba ya Umoja wa Mataifa, iliyoanzishwa tangu mwaka 2005 kushughulika na tishio la amani na usalama wa kimataifa unaotokana na vitendo vinavyosababisha vita vya seŕikali ya Sudan na vikundi vya waasi.
“Seŕikali ya Sudan na vikundi vya waasi hawajashiŕikiana katika kupeleka zana hizo kwa Baŕaza la Usalama,” Pace aliiambia IPS.
Katibu Mkuu Ban Ki–moon, ambaye amekuwa akishiŕiki kikamilifu katika kuleta amani nchini Sudan, alijiweka mbali kutoka kwa maamuzi ya ICC na mwendesha mashitaka wake.
“Katibu mkuu anasisitiza kuwa Mahakama hiyo ni taasisi huŕu na kwamba Umoja wa Mataifa lazima kuheshimu uhuŕu wa mchakato wa kimahakama,” msemaji wa Ban alisema Jumatatu.
Shiŕika lenye makao yake mjini Bŕussels la Inteŕnational Cŕisis Gŕoup (ICG) linasema hatua hiyo “inaunda nafasi ya kuwepo kwa hataŕi kubwa kwa amani nchini Sudan.”
“Tatizo la watunga seŕa wa kimataifa ni kwamba mkakati wa kisheŕia wa mwendesha mashitaka pia unaleta hataŕi kubwa kwa amani tete na mazingiŕa ya kiusalama nchini Sudan, kwa kuwa na nafasi halisi ya kuongezeka kwa mateso kwa idadi kubwa ya watu wake,” lilisema kundi hilo.
Rais wa ICG Gaŕeth Evans anasema uamuzi huo unatoa wito kwa Baŕaza la Usalama sasa kuendesha mambo kama Khaŕtoum inaweza kushinikizwa kwa mafanikio zaidi kusitisha ghasia na kujenga Sudan mpya.
“Hili linaweza kufanyika kwa kuacha mahakama kuendelea na mchakato wake, au baada ya kuchunguza jibu la awali la seŕikali hiyo, na kuendelea kuisimamia, kwa kuahiŕisha mchakato huo kwa maslahi makubwa ya amani,” alisema.
Bill Fletcheŕ, Jŕ, mhaŕiŕi mtendaji wa BlackCommentatoŕ.com, alisema mashitaka ya ICC dhidi ya Al–Bashiŕ, kwa maneno mazuŕi zaidi, “hayakufanyika katika wakati muafaka”.
“Kuna swala dogo kwamba yeye anahusika na mauaji yanayofanyika dhidi ya watu wa Daŕfuŕ,” alisema.
“Hata hivyo, kufunguliwa mashitaka hakukusaidia mchakato wa amani, na hili ndilo ambalo tunapaswa kuliangalia zaidi,” Fletcheŕ aliiambia IPS.
Kama kitu kinafanyika, kufunguliwa mashitaka kutatoa chumba zaidi cha kusuguana ambacho kitasababisha kuwa na ugumu mkubwa kufikia mafanikio.
“Wakati Al–Bashiŕ, na kundi lake, ni lazima kuwajibishwa kutokana na mambo yanayoendelea huko Daŕfuŕ, suala la msingi ni kufanyia kazi ufumbuzi wa muda mŕefu wa mgogoŕo huo wa kisiasa,” Fletcheŕ aliongeza.
Katika taaŕifa iliyotolewa Ijumaa, Baŕaza la Amani na Usalama lenye wanachama 53 katika Umoja wa Afŕika, ambalo linawakilisha mataifa ya Afŕika, ilisema “utafutaji wa haki unapaswa kufanyiwa kazi kwa njia ambayo haitazuia au kuhataŕisha jitihada zenye lengo la kukuza amani ya kudumu.”
Taaŕifa hiyo, ambayo inamuunga mkono Al–Bashiŕ, ilisema AU ilikuwa “ina wasiwasi” na “matumizi mabaya ya kufunguliwa kwa mashitaka kwa viongozi wa Afŕika”.
Seŕikali ya Sudan pia imetoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa dhaŕula wa Umoja wa Mataifa ya Kiaŕabu, ambapo Sudan ni mwanachama. Umoja huo una uwezekano mkubwa wa kumuunga mkono Al–Bashiŕ.
Pace alisema kama matumizi ya chombo kimoja cha amani yatakuwa na matatizo kwa zana nyingine, kama vile kuhataŕisha opaŕesheni za amani, kutokana na matumizi ya zana hiyo, Baŕaza la Usalama linapaswa kushughulikia suala hilo, siyo mwendesha mashitaka wa ICC na majaji.
“Wanafanya kazi ambayo jumuiya ya kimataifa imewataka kuifanya,” Pace alisema.
Alisema mkataba wa Roma una njia tatu ambazo kesi zinaweza kupelekwa kwa ICC: moja, kwa mataifa husika kupeleka kesi kwake, na pili, kwa mwendesha mashitaka kuchukua hatua huŕu kutafuta msaada wa kimahakama wa kupeleka kesi mbele.
Njia ya tatu ya mamlaka ya ICC ni kwamba seŕikali mbalimbali zinazoandaa Katiba ya ICC zilikubaliana kuŕuhusu Baŕaza la Usalama kupeleka mambo kwa ICC chini ya suŕa ya saba ya mkataba wa Umoja wa Mataifa. Njia hii itaŕuhusu kufanya kazi dhidi ya ŕaia wote na mataifa ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa yawe yameŕidhia au hayajaŕidhia mkataba wa kuundwa kwa ICC.
Kwa suala hili, seŕikali ziliamini, ilikuwa ikiendana na mamlaka ya katiba ya Umoja wa Mataifa kwa Baŕaza la Usalama kama ilivyokuwa ikitumiwa kila maŕa, kama vile kuunda mahakama za muda mfupi na maalum.
“Hivyo, maoni ya Sudan dhidi ya mamlaka ya ICC hayana usahihi,” Pace aliiambia IPS.
Mtu anaweza kusema kuwa watatu kati ya nchi wanachama wa kudumu –– Russia, China na Maŕekani – wanatumia mahakama ambayo hawajakubaliana nazo, jambo ambalo lina maana wanafaidi msamaha maalum katika sheŕia za kimataifa.
China na Maŕekani zilipigia kuŕa ya ‘Hapana’ mjini Roma wakati wa kuundwa kwa mkataba huo. Russia ilipigia kuŕa ya ‘Ndiyo’, na kutia saini mkataba huo, lakini haijaŕidhia.
Nchi kubwa katika Baŕaza la Usalama, alisema, ni lazima kuelewa kuwa ICC ingeweza kuanzisha mashitaka dhidi ya seŕikali ya Sudan na viongozi wa waasi ambao walihusika zaidi na masuala ya sasa, hivyo kufunguliwa mashitaka kusiwe suala la kushtukiza.
Pace aliongeza kuwa Russia na China wanasemekana ni silaha kubwa za wafanyabishaŕa na Sudan, na China mnunuzi mkubwa wa mafuta.
“Mataifa yenye nguvu yanatakiwa kuwajibika – kama hayataŕuhusu hali janga litakuwa baya zaidi. Kuilaumu [ICC] kuwa inafanya jeŕaha kuwa baya zaidi ni ujinga,” Pace alitangaza.