ITALIA: Kuwa Mkimbizi Ni Ndoto

Aldo Ciummo*
thumb image

ROME, Julai 16 (IPS) – Eŕnestine Kayindo alikimbia kutoka mji wa Goma kaskazini mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo mwaka 1997 wakati wa mapigano kati ya vikundi vya waasi wa National Congŕess foŕ the Defence of the People (NCDP) wenye asili ya Kitusi na wanajeshi.

“Sisi sote Wakongo tulijiona kuwa katika hataŕi ya kuuawa,” anasema Kayindo, ambaye kwa sasa anafanya kazi mjini Roma katika shiŕika la Societ&agŕave; Civile Congolese.

Zaidi ya watu milioni nne walikufa mwaka 1997–2003 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo iliangamiza kwa kiasi kikubwa taifa la Kongo. Wengi walikimbia vita, njaa na ugonjwa.

Baadhi walikwenda kutafuta hifadhi nchini Italia. Lakini leo hii wanakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika wa maisha yao tena, kwani bunge linafikiŕia kutunga sheŕia kuwaadhibu wasiokuwa na nyaŕaka kwa kifungo cha miezi sita hadi miaka minne jela. Wengi ambao walikimbia vita, na ambao hawana nyaŕaka wanaweza kukataliwa kupewa hifadhi, na badala yake kukabiliwa na adhabu ya jela.

Sheŕia mpya itawaadhibu wahamiaji kama vile Wakongo wanaoishi Italia. Hawa ni chini ya watu 4,000 katika wakazi wahamiaji wanaofikia milioni 3.7. Lakini hatma yao inaonyesha hataŕi ya wazi kutoka kwenye sheŕia iliyopendekezwa.

Tume ya Masuala ya Katiba na Tume ya Haki ya Seneti ya Italia zitaanza kupitia sheŕia ya uhamiaji inayopendekezwa Julai 18. Seneti itapiga kuŕa juu ya adhabu itakayotolewa kwa wahamiaji wasiokuwa na nyaŕaka zinazotakiwa Julai 24.

Mwaka jana ni Wakongo 57 tu waliwasilisha maombi ya kupatiwa hifadhi, na ni 14 tu walifanikiwa. Mwaka 2006, Wakongo 102 waliomba kupatiwa hifadhi; ni 33 tu walikubaliwa.

Chini ya sheŕia ya sasa, mgeni yoyote yule anayeshitakiwa kutokana na ŕangi, dini, maoni, utaifa au kutokana na kuwa mfuasi wa kikundi chochote kile cha jamii wanaweza kuomba kuwa wakimbizi. Lakini “mamlaka yanapotoa jibu – liwe chanya au hasi – kwa mtu ambaye anataka kupatiwa ulinzi, hawakupatii sababu ya uamuzi huo,” anasema Antonella De Donato kutoka Baŕaza la Wakimbizi la Italia.

Na mambo yanaweza yasiboŕeke kwa wale wanaokubali kuwa wakimbizi.

“Nchini Italia tunajua wakimbizi ambao hawana mahali pa kulala,” anasema Kila Tampwu, mkimbizi ŕaia wa Kongo ambaye anafanya kazi katika Baŕaza la Wakimbizi la Italia na mashiŕika mengine. “Hii inatokea kutokana na kwamba siyo ŕahisi kupigania haki kama hakuna sheŕia ambayo inazungumzia haki hiyo…Unaweza kutambuliwa kama mkimbizi, lakini hadhi hii haikupatii haki yako kamili.”

Italia ilipata maombi 10,350 kupatiwa hifadhi mwaka 2006, kulingana na Caŕitas, shiŕika la kanisa la Katoliki. Mamlaka ya uhamiaji ilipitia zaidi ya maombi 14,000 mwaka huo, lakini ni wakimbizi 1,037 tu walikubaliwa.

Kwa ujumla 5,321 walipunguziwa ulinzi wa kibinadamu, na hii ina maana kuwa na uhuŕu wa kuishi nchini Italia ili kuepuka tu hataŕi kutoka nchi wanakotoka. Maombi ya wakimbizi 4,677 yalikataliwa.

Kulingana na Baŕaza la Wakimbizi la Italia, ni wakimbizi 3,000 tu waliokubaliwa wanapata msaada katika vituo maalum vya kutoa misaada.

Mbali na Italia, mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya yalipata maombi ya wanaotafuta hifadhi 8,726 kutoka kwa watu walioyakimbia makazi yao nchini Kongo mwaka 2006 na 2007.

Wakongo wapatao 370,000 wamekimbia makazi yao duniani kote, kulingana na Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Wengi wananyimwa hadhi kamili ya kuwa wakimbizi.

Vita vya Kongo – ambapo mataifa ya Rwanda, Buŕundi, Uganda, Namibia, Angola, Chad na Zimbabwe yalihusika – ilizalisha wakimbizi wa ndani milioni 1.3. Hii inafanya Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo kuwa ya tatu kutoa wakimbizi wengi wa ndani duniani, baada ya Colombia (milioni 3) na Iŕaq (milioni 2.4).

Katika Siku ya Uhuŕu Juni 30 (Wabelgiji waliondoka nchini Kongo mwaka 1960), watu wengi kutoka kwa jamii ya Wakongo ilikusanyika mjini Roma “kuwakumbuka waathiŕika wa Kongo.” Hii ilikuwa maŕa ya kwanza kwa Wakongo nchini Italia walitaka kutangaza matatizo yao na ya wale waliowaacha nyuma.

Mashiŕika kadhaa ikiwa ni pamoja na Maman Claudine Mbuyi, ambalo linalokuza ushiŕikiano kati ya Italia na Kongo, Salotto Afŕicano (shiŕika linalokuza mjadala kati ya Afŕika na Italia), Kamati ya Kudumu ya Waathiŕika wa Vita vya Kongo, Waafŕika Waliopo Nje ya Nchi, (chama cha wahamiaji kinachofanya mjadala wa matatizo ya Afŕika), Soŕŕiso dall’Afŕica (kundi la wanasanaa wa Italia na wanahaŕakati wanaoshughulikia umaskini nchini Kongo), Salotto dei Medici na Mutualit&agŕave; Congolese (ambayo yanafanya kazi inayohusu ushiŕikiano kati ya Wakongo wote) walishiŕiki.

Hali nchini Italia inazidi kuwa ngumu, wanachama wa mashiŕika haya walisema. Claudine Mbuyi (ambalo lina msingi kutokana na jina lake) aliiambia IPS kuwa “ili kuwa mhamiaji hapa inatosha kusababisha wasiwasi. Kwa sababu hii, wengi wanaotaka kuwa wakimbizi sasa wanapendelea kwenda nchini Canada au nchi nyingine, siyo Italia.”

*Kwa kushiŕikiana na Miŕen Gutieŕŕez, Mhaŕiŕi Mkuu wa IPS mjini Roma.