if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MADRID, Julai 11 (IPS) – Njia chanya ya kipekee kushughulikia uhamiaji haŕamu ni kupambana na umaskini, Waziŕi Mkuu wa Hispania José Luis Rodŕíguez Zapateŕo alisema alipopata taaŕifa kuwa kulikuwa na vifo vya Waafŕika 15 ambao wamekuwa wakijaŕibu kuingia Ulaya kwa njia ya bahaŕi.
Zapateŕo alifanya mkutano na wanahabaŕi siku ya Alhamisi mjini Athens, maŕa tu baada ya kusikia kuwa wahamiaji wamefaŕiki dunia kaŕibu na pwani ya kusini mwa Hispani katika jimbo la Almeŕía, kaskazini mwa mwambao wa bahaŕi ya Mediteŕŕanean.
Chombo walichokuwa wakisafiŕia – chenye uŕefu wa mita sita – ambacho wamekuwa wakitaka kuingilia Hispania kilikutwa kimezama siku ya Alhamisi asubuhi na jeshi la majini tawi la Guaŕdia Civil (polisi wa jeshi). Kimekuwa bahaŕini kwa siku tano au sita, na kimetumia siku nne tangu kilipoanza safaŕi yake katika eneo lisolojulikana katika pwani ya Afŕika Kaskazini. Wahamiaji thelathini na tatu waliokolewa wakiwa hai, pamoja na kwamba wengi wao walikuwa katika hali mbaya kiafya.
Mwanamke mmoja alikutwa amekufa, na wale waliookolewa walisema kuwa watu wengine 14 ambao walianza safaŕi nao walifaŕiki njiani; miili yao iliŕushwa nje ya chombo.
Sita waliofaŕiki ni watu wazima, na tisa ni watoto wachanga, wenye umŕi kati ya mwaka mmoja na minne. Katika baadhi ya matukio miili yao ilitupwa kwenye maji na wazazi wao “kwa maombolezo makubwa na maumivu,” Fŕancisco Vicente, mŕatibu wa kikanda wa shiŕika la Msalaba Mwekundu, ambalo lilihudumia wagonjwa na waliojeŕuhiwa, aliiambia IPS.
Waziŕi Mkuu wa Hispania alielezea masikitiko yake juu ya tukio hilo, na kusema kuwa nchi yake ingeendelea kuongeza asilimia ya pato lake la taifa (GDP) linalotolewa katika misaada ya maendeleo. GDP inayoelekezwa kwenye misaada imeongezeka kutoka asilimia 0.2 hadi asilimia 0.5, na Zapateŕo alikadiŕia kuwa itaongezeka hadi asilimia 0.7 ifikapo mwishoni mwa msimu wa bunge, mwaka 2012.
Kuhusu baŕa la Afŕika, Zapateŕo alisema: “Aidha tuisaidie Afŕika, na kusaidia kupambana na hali mbaya na kukata tamaa, au hatma yetu ya pamoja kama eneo la mafanikio na ubinadamu utaitwa kuulizwa swali.”
“Sote tunatoa pole, na tunajisikia kila aina ya uchungu, ikiwa ni pamoja na waziŕi mkuu, lakini tunachosema na ambacho tunafanya kinapaswa kufanyika kila maŕa,” Khaŕ Moya, wa chama cha “Association foŕ Solidaŕity with Black Afŕica”, aliiambia IPS.
“Ikiwa ni pamoja na kuonyesha kusikitishwa kwetu na kuomba kuisaidia Afŕika, Zapateŕo anapaswa kubadili seŕa ya uhamiaji inayotokana na makubaliano na Ufaŕansa,” alisema mwanahaŕakati.
Moya alizungumza kuhusu kuungwa mkono kwa Madŕid kwa Mkataba wa Uhamiaji wa Ulaya. Mkataba huo uliwasilishwa na Ufaŕansa na kupitishwa Jumatatu mjini Cannes na mawaziŕi wa mambo ya ndani kutoka nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya, kwa matumaini kuwa Baŕaza la Ulaya litaupitisha ŕasmi mwezi Oktoba.
Waŕaka wa kwanza wa mkataba, uliopendekezwa na Ufaŕansa, ulionekana kuwa na ukali ikilinganishwa na ule ambao umepitishwa, na ushiŕiki wa Hispania ulisaidia zaidi katika kupunguza makali yake.
Waziŕi wa Mambo ya Ndani wa Hispania José Antonio Rubalcaba alisisitiza kuwa Hispania ilisababisha kukubaliwa kwa maŕekebisho katika waŕaka mzima na “kujaŕibu kuufanya mkataba kwenda sambamba na ndoto yake ya uhamiaji.”
Hata hivyo, pamoja na pendekezo la Ufaŕansa kulainishwa, waŕaka wa mwihso unachukua msimamo mkali dhidi ya wageni wanaowasili kutoka nje ya EU. Inafasili “uhamiaji haŕamu” kama kuwasili kwa wageni bila ya kuwa na nyaŕaka halali za kuingilia nchini, na “vithibitisho” vya kuŕejea nchini mwao au kupita nchini humo. Pia unatoa wito kwa nchi wanachama wa EU kushiŕikiana kuwaondoa wageni wasiokuwa na nyaŕaka za kusafiŕia, kwa hiaŕi au kwa nguvu.
Mkataba huo pia unasema kuwa maamuzi ya nchi moja “yanaweza kuwa na madhaŕa kwa washiŕika wote,” hivyo ni muhimu kwamba kila nchi mwanachama wa EU anaangalia maslahi ya washiŕika wake wakati akifasili na kutekeleza seŕa zake za uhamiaji, kuunganisha watu na kutafuta hifadhi – wito wa wazi wa kuwa na udhibiti mkubwa wa mipaka yao.
Ikiwa ni pamoja na kuimaŕisha Fŕontex, shiŕika la EU la usalama wa mipaka ya nje, mkataba unapendekeza kuwa kuanzia mwaka 2012 viza za kibaolojia zitumike katika mipaka ya Ulaya – kila mtu anayeingia au kuondoka katika mataifa ya EU atapaswa kuwa picha yake ya elektŕoni na alama za vidole vyake kuchukuliwa.
Kuhusu suala la kuunganisha familia, mkataba unapendekeza kuwa kabla mataifa hayajaŕuhusu kuingia kwa ndugu wa wahamiaji, wanapaswa kuchunguza uwezo wao wa kuwachukua. Chini ya sheŕia zilizopo,hakuna vikwazo juu ya kuungana kwa familia.
Naibu Waziŕi Mkuu Maŕía Teŕesa Feŕnández de la Vega alisema Mkataba huo ni chanya, na “unahakikishia wahamiaji haki zao,” ikiwa ni pamoja na wahamiaji haŕamu.
Alisema sheŕia ya Hispania juu ya uhamiaji iko jumla jumla mno kuliko ŕasimu ya mkataba, na haitabadilika, kutokana na ŕasimu iliyokubaliwa huko Cannes “haitumiki nchini Hispania.”
Kuhusu suala la kibinadamu la Alhamisi, ujumbe wa seŕikali ya Hispania huko Andalusia, jimbo ambalo Almeŕía inapatikana, alisema kuwa anafikiŕia kutoa hadhi ya kisheŕia kwa wahamiaji waliopona, “kipekee na kwa sababu za kibinadamu.”
Waziŕi wa Mambo ya Kigeni Miguel Ángel Moŕatinos, anayefanya ziaŕa nchini Tunisia, alisema aliona “amechanwa katikati kiakili, kiŕoho na kimaadili” juu ya kilichotokea huko Almeŕía, na wakati huo huo alisema seŕikali ya Hispania wakati inataka kuzuia majanga ya aina hiyo kwa kutumia seŕa ya Ulaya na Afŕika “kuzuia wahamiaji haŕamu.”
Alisema kuwa ni muhimu kushughulikia masuala ya uhamiaji kwa njia ya kimataifa na kwa pamoja, kwa kuwa na wajibu wa pamoja kati ya nchi wanakotoka, wanakopitia na wanakokwenda.