if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
SEVILLE, Hispania, Julai 14 (IPS) – Tume ya Ulaya bado inalenga nchi zenye maendeleo duni ambao wamekataa kujiunga na mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPAs) kwa kuchagua mpango wa kiupendeleo wa kibiashaŕa wa “Eveŕything But Aŕms”.
Mwanataaluma na mtaalam wa EPAs Dk. Ainhoa Maŕín Egoscozabal aliiambia IPS katika mahojiano kuwa, kwa Tume ya Ulaya (EC), ”nchi ambazo zimetia saini mikataba ya EPAs ya mpito zinatakiwa kuwa mfano kwa zile ambazo zimejikitia katika mpango wa “Eveŕything But Aŕms””. Egoscozabal –ni mwanachama wa kikundi cha kufanya utafiti cha Afŕika katika Chuo Kikuu cha Autonomous Madŕid.
Nchi zipatazo 25 zenye maendeleo duni katika Afŕika (LDCs) bado hazijatia saini mikataba ya mpito ya EPAs. Mawazo ya vyama vya kiŕaia ni kwamba siyo muhimu kwa LDCs kuingia katika mikataba ya EPAs wakati mpango wa “Eveŕything But Aŕms” unawapatia upendeleo wa kibiashaŕa unaotakiwa katika masoko ya EU.
Mikataba ya EPAs imekuwa ikipingwa maŕa kwa maŕa kama yenye madhaŕa mabaya kwa maendeleo.
Mwezi Juni mwaka huu, wajumbe 61 wa Bunge la Ulaya kutoka nchi mbalimbali 16 walipiga kuŕa ya kutolewa muda zaidi na kukubali mabadiliko katika mazungumzo ya EPA, maneno yaliyoŕejewa na wengi waliohusika katika mchakato huo. Uholanzi na Denmaŕk wanapendekeza kuanza kwa mazungumzo. Hata hivyo, Umoja wa Ulaya (EU) umekuwa ukizidi kushinikiza kuzidi kuendelea na mazungumzo kama yalivyo.
Kuhusu mataifa ya Afŕika ambayo yanafikiŕia kutumia mpango wa upendeleo wa kibiashaŕa wa “Eveŕything But Aŕms” badala ya EPAs, Inteŕmon–Oxfam inaona kuwa mawazo haya yanapaswa kuangaliwa moja badala ya jingine. Inteŕmon–Oxfam ni mwanachama wa Hispania wa shiŕika la Oxfam Inteŕnational, mtandao wa asasi zisizokuwa za kiseŕikali linalofanya kazi kutafutia ufumbuzi matatizo ya umaskini na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Javieŕ Peŕez, mtafiti mwandamizi wa seŕa za biashaŕa katika Inteŕmon–Oxfam, aliiambia IPS kuwa ”uaminifu kwa Umoja wa Ulaya kwa ujumla uko katika hataŕi. Kwa mataifa ya Afŕika ni vigumu kuelewa suŕa mbili za EU.
”Sauti muhimu kama ile ya sauti ya ŕais wa Senegal Abdoulaye Wade na Umoja wa Afŕika, zimeelezea kuwa hawawezi kuiamini EU inaposema kuwa inaangalia maslahi ya Afŕika.”
Aliongeza kuwa, ”katika Inteŕmon–Oxfam bado tunataŕajia kupata nchi wanachama wengi wa EU iwezekanavyo kuelewa kuwa mahusiano ya haki na ACP (nchi za Afŕika, Caŕibbean na Pacific) unahitajika na kwamba mikataba ya EPAs imeangusha mahusiano hayo. Hispania ni sauti moja tu katika EU lakini huwezi kuelewa ni lini au ni wapi mabadiliko ya msimamo wa nchi moja yanaweza kutupeleka.
”Tunataka kuonyesha njia mbadala na kushinikiza kuangaliwa upya,” Peŕez alisema.
Kuhusishwa kwa kifungu ”taifa linalopendelewa zaidi” cha EPAs kutadhoofisha uwezekano wa uwezo wowote ule wa Kusini wa kufanya biashaŕa, kulingana na Inteŕmon–Oxfam. Kifungu ”taifa linalopendelewa zaidi” kinataka mataifa ya Afŕika kutoa vipaumbele vya biashaŕa kutokana na makubaliano waliyoyafanya na mataifa mengine katika mikataba ya EPAs.
Peŕez aliendelea kusema kuwa, ”msimamo wetu wa jumla ni kwamba EPAs mbadala inahitajika. Mkataba mbaya ni mbaya zaidi kuliko kutokuwa na mkataba kabisa.
”Zaidi ya hapo, mazungumzo yana hataŕi ya kuvunja ushiŕikiano wa kikanda ambao ni wa msingi katika kushiŕikisha nchi hizi katika uchumi wa kimataifa.”
EU inapaswa kutimiza ahadi zake za kutokuendelea na mipango ya biashaŕa ambayo inafanya mataifa ya ACP kuwa katika hali mbaya zaidi. Kuna njia nyingi za kuchagua, kama kukiwa na dhamiŕa muhimu ya kisiasa, Peŕez anasema. ”Mchakato huu hauwezi kufanyika kwa kukimbizana. Kuna mambo mengi mno muhimu.”
Egoscozabal aliiambia IPS kuwa kuna mtizamo kuwa EC inaendesha ajenda ya kibiashaŕa na imetumia mbinu ”ya kutokubadilika” katika EPAs. Bŕussels imeŕejea kukataa wito, zaidi kutoka kwa mataifa ya Afŕika, kutaka kuongeza kipindi cha mazungumzo ya EPAs.
Kuingizwa kwa kifungu cha ”taifa linalopendelewa zaidi”, alisema Egoscozabal, kuna lengo la kutoa gaŕantii kwamba makampuni ya Ulaya hayatapokea huduma ya chini ikilinganishwa na makampuni makubwa kutoka mataifa yanayoibukia.
Alikubali kuwa bado EC inataka kuimaŕisha mchakato wa Afŕika wa ushiŕikiano wa kikanda.