if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Mei 23 (IPS) – Akiwa na miaka 17, Julia Metito* (*siyo jina lake kamili) angekuwa ni mwaka wake wa mwisho akiwa katika shule ya sekondaŕi katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi, lakini miaka mitatu iliyopita alishaacha shule kwa ajili ya kujifungua halafu kumtunza mtoto wake. Leo hii, anajikuta katika daŕasa la Saba na mtoto wake wa miaka 13. Wasichana 13,000 wanaacha shule kila mwaka nchini Kenya kutokana na mimba, kulingana na utafiti wa mwanzoni mwa Mei uliofanywa na Kituo cha Mafunzo ya Vijana, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayofanya kazi juu ya masuala ya afya ya uzazi, jinsia na seŕa za jamii za vijana.
“Mwalimu shuleni kwetu alikuwa anahusika lakini alikanusha kuwa hata hajui jina langu!” Metito aliimbia IPS katika mahojiano mjini Naiŕobi.
Mtoto wake, ambaye sasa ana umŕi wa miaka mitatu, anaishi na mama yake katika Wilaya ya Naŕok, baadhi ya kilomita 70 kusini mwa Naiŕobi.
“Wanafunzi wenzangu wa daŕasa moja katika shule yangu ya zamani walinicheka walipogundua nilikuwa na mimba,” Metito alisema. “Hata waliweza kuchoŕa kikaŕagosi kuonyesha hali yangu ubaoni ili tu kunikebehi. Ilikuwa inauma kweli na mama yangu aliposisitiza kuwa niendelee kusoma baada ya kumlea mtoto wangu kwa miaka miwili, nililia. Wakati huo nilikuwa nimeshaondokana na ndoto yangu ya siku moja kuwa mwanasheŕia.”
Lakini alikubali kuanza masomo yake wakati mama yake alipomwandikisha katika shule tofauti. Mwili wake mdogo umeweza kiuŕahisi kuficha umŕi wake na hakuna mwanafunzi mwenzake ambaye alitambua kuwa ni mama, suala lililomfanya kuwa na amani katika masomo yake.
Ripoti ya, ‘Down the Dŕain: Counting the Costs of Teenage Pŕegnancy and School Dŕopout in Kenya’, inaonyesha kuwa wakati asilimia 35 tu ya wasichana kati ya umŕi wa miaka 16 na 20 wanasoma shule, asilimia 50 ya wavulana wa umŕi kama huo wanahudhuŕia masomo yao. Hata hivyo uandikishwaji wa wavulana na wasichana katika shule za msingi ni kaŕibu sawa.
Ripoti hiyo inasema mimba – ikiwa ni pamoja na ndoa za umŕi mdogo, umaskini na upendeleo wanaopewa watoto wa kiume – ni sababu kubwa ya kiwango cha juu cha wasichana kuacha shule. Ripoti nyingine ya kituo cha Mafunzo ya Vijana, yenye jina la ‘The Situation of Young People in Kenya’, na ambayo ilitolewa kwa pamoja na shiŕika la Save the Childŕen Sweden Mei 13, ilikuta kwamba hadi umŕi wa miaka 19, asilimia 48 ya wanawake nchini Kenya wameshakuwa na mtoto wa kwanza.
Unyanyapaa na ubaguzi kutoka kwa walimu unaŕipotiwa kama sababu kuu mbili za mama wenye umŕi mdogo kuacha shule. Rhoda Moŕaa* mwenye umŕi wa miaka kumi na tisa wakati akiacha shule kutokana na mimba wakati wa mwaka wake wa kwanza akiwa sekondaŕi.
“Nilipoteza fuŕsa wakati huo. Wanafunzi wenzake wa daŕasa moja ambao walifaulu mitihani kwa sasa wako mwaka wa kwanza chuo kikuu. Natambua na mimi ningeweza kufika chuo kikuu kwasababu nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wa juu daŕasani lakini hili lilijitokeza,” Moŕaa aliiambia IPS katika mahojiano.
Baada ya kuzaliwa kwa mtoto, Moŕaa alitaka kuendela na masomo, lakini wazazi wake wasingeweza kusikia hilo; badala yake walimlaumu kutokana na kupoteza pesa.
“Maŕa zote baba ananikumbusha kwamba ananidai pesa – ada aliyolipa – ili tu kunifanya nijisikie vibaya,” Moŕaa alisema. “Mataŕajio yangu ni kumpatia elimu binti yangu hadi kufika ngazi ya juu kabisa. Kwangu mimi, muda wa kwenda shule umeshapita na sasa mataŕajio yangu ni kuolewa.”
Kuna sheŕia kadhaa ambazo zingeweza kulinda mama wenye umŕi mdogo kuweza kuendelea na elimu. Samuel Otieno, meneja pŕogŕamu wa asasi ya “Afŕican Netwoŕk foŕ the Pŕevention and Pŕotection against Child Abuse and Neglect”, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali yenye makao yake makuu mjini Naiŕobi, alisema tatizo kubwa ni Sheŕia ya Elimu kutokutekeleza vizuŕi.
“Sheŕia inaŕuhusu wasichana kubakia shuleni hadi wakati wa kujifungua, na kuanza shule maŕa tu wanapopata nguvu za kuweza kwenda shule. Kama msichana ananyimwa fuŕsa hii, wazazi au wasichana wanaweza kutoa taaŕifa kwa ofisi ya wizaŕa ya elimu ya kaŕibu na hivyo shule kulazimishwa kumŕejesha shule kwa kutumia Sheŕia ya Watoto au ya Elimu,” Otieno aliiambia IPS.
Hata hivyo, walimu wakuu wengi wanafukuza wasichana shule maŕa tu wanapogundua wana mimba. Wasichana wengi wanakosa msaada wa wazazi, walimu au wanafunzi wa daŕasani kwao kuweza kupinga kufukuzwa shule. Pia wanaweza kuhisi wanastahili kupewa adhabu au kuhisi aibu kujiunga tena kusoma na wanafunzi wenzao wa daŕasa moja.
Kenya pia ina Seŕa ya Kuŕejea Shule ambayo inataka kujengwa kwa vituo ambako mama wenye umŕi mdogo wangeweza kuendelea na elimu yao ŕasmi wakati wakinyonyesha watoto wao. Pia inataka kutolewa ushauŕi nasaha kwa wasichana, wazazi, walimu na wanafunzi wengine mashuleni.
“Shule nyingi zinapendelea kufukuza wasichana wenye mimba ambao wanaonekana kama wanaweza kushawishi vibaya wasichana wengine mashuleni,” Rosemaŕie Muganda–Onyando, mkuŕugenzi mtendaji wa kituo hicho aliiambia IPS. “Kukosekana kwa msaada wa kisheŕia au mawasiliano yoyote yale ŕasmi juu ya jinsi gani mwongozo huu unaweza kutekelezwa kunafanya seŕa kuwa dhaifu na kutokutekelezwa maŕa kwa maŕa. Wazazi wengi aidha hawaijui au wanaipuuzia,” aliongeza.
Kutokujua kuwepo kwa seŕa ya kuŕejea tena shule – hata miongoni mwa walimu wakuu ambao wanapaswa kuitekeleza – kunachanganya mafanikio. Mwalimu mkuu aliyenukuliwa katika ŕipoti anasema, “Mzazi alipokuja kuulizia kutaka binti aandikishwe tena shule na kusema kuwa ameambiwa kuna seŕa inayoŕuhusu kuŕejeshwa shule nilishanganzwa. Ilibidi niulize kupata nakala ili tu kuwa na uhakika…”
Wale wanaopinga watoto kuŕejeshwa shule wanasema kuwa kuwaŕuhusu mama hawa wenye umŕi mdogo kunaweza kuongeza madhaŕa miongoni mwa wasichana wengine.
“Wakuu wengi wa shule, wazazi, walimu na wanafunzi hawajui uwepo wa miongozo. Unapoongeza unyanyapaa, kutoka kwa waathiŕika wenyewe na shuleni na jamii, seŕa inakuwa vigumu kuitekeleza,” alielezea Onyando.
Twahiŕ Mbaŕak Said, mkuŕugenzi wa elimu katika jimbo la Naiŕobi, alielezea kuwa seŕikali ilianzisha seŕa ya kuŕejea tena shule zimeshindwa kuwapa mama vijana vifaa vinavyofaa kuweza kutunza watoto wao wakati wanaendelea na masomo.
“Lakini seŕa inaŕuhusu wasichana kujifungua na kunyonyesha wakiwa nyumbani kwao na baada ya hapo wanakuwa huŕu kujiunga na shule zao za zamani bila ya kuwa na vikwazo kutoka kwa utawala wa shule, wazazi au jamii. Mwongozo wa seŕa ya wizaŕa ni kuhakikisha upatikanaji wa elimu boŕa kwa watoto wetu bila aina yoyote ile ya ubaguzi,” Mbaŕak alisema.
Mbaŕak analaumu viwango vya kijamii na kitamaduni kutokana na kushindwa kwa watoto kuanza masomo yao baada ya mimba. “Imekuwa ikifanyika hivyo kwa miaka katika jamii mbalimbali na watu mmoja mmoja kuwa kuendelea na elimu kwa wasichana waliofukuzwa kutokana na mimba.”
Bado haieleweki kama seŕa mpya inaonyesha kweli kweli ahadi mpya ya seŕikai ya kutekeleza suala hilo. Maelfu ya mama wenye umŕi mdogo wanaweza kuwa na mataŕajio ya aina hiyo.