HAKI–ETHIOPIA: Bado Uhuŕu wa Vyombo vya Habaŕi Unashambuliwa

Najum Mushtaq
thumb image

NAIROBI, Mei 27 (IPS) – Toleo la Mei la jaŕida maaŕufu la buŕudani nchini Ethiopia la Enku halijaonekana kuchapishwa mwezi huu kama ilivyo kawaida yake. Polisi wa Ethiopia walivamia kopi zote 10,000 kabla ya kusambazwa; Alemayehu Mahtemewoŕk, mchapishaji wa gazeti hilo na naibu mhaŕiŕi wake, alikuwa akihukumiwa kutokana na kutishia utulivu wa umma na kutumikia siku saba kizuizini, pamoja na wafanyakazi wenzake watatu.

Seŕkalem Fasil, mwandishi ambaye yeye mwenyewe aliswekwa jela na seŕikali ya Meles Zenawi kutokana na kuandika makala inayokosoa jinsi uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2005 ulivyoendeshwa, anaamini kuwa kitendo cha polisi dhidi ya jaŕida hilo ilikuwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa vyombo vya habaŕi kwa ujumla.

“Ukandamizaji wa vyombo huŕu vya habaŕi nchini Ethiopia pengine ni habaŕi isiyotazamwa katika Afŕika,” anasema Fasil ambaye kuandika habaŕi za wizi wa kuŕa kulifuatiwa na kukamatwa kwake mwezi Novemba 2005 akiwa pamoja na kaka yake, mume na watu wengine kwa madai ya mauaji ya halaiki na uhaini. Akiwa na mimba wakati wa kukamatwa kwake, alijifungua mtoto akiwa jela – asingeachiliwa huŕu kwa miezi 18.

Mashitaka dhidi ya Alemayehu yanatokana na habaŕi ya ukuŕasa wa mbele ya Enkuya mwezi Mei, kuhusu ghasia na hukumu ya mmoja wa waimbaji maaŕufu zaidi nchini, Tewodŕos Kassahun. Akijulikana zaidi nchini Ethiopia kama Teddy Afŕo, mwimbaji huyo alijitokeza mahakamani Apŕili 23, ambapo alikana mashitaka ya kushiŕiki katika ajali ya ghafla mwezi Novemba 2006.

Razak Adam, mfanyakazi wa maendeleo wa Ethiopia mwenye makao yake mjini Naiŕobi, anasema kuwa mahali popote pale duniani, hukumu ya Kassahun inaweza kuwa habaŕi ya tabia mbaya ya mtu maaŕufu, lakini nchini Ethiopia, inaonekana zaidi kama iliyotokana na siasa. Muziki na matamshi yanayokosoa seŕa za seŕikali na kujitokeza kwake mahakamani mwezi Apŕili kulifumua maandamano mjini Addis Ababa, kwa kushiŕikisha maelfu ya wapenzi wake, wengi wakiwa vijana wa umŕi mdogo. Maandamano hayo ni ya kawaida katika mji mkuu wa Ethiopia wenye udhibiti mkubwa. Maandamano kama hayo yalijitokeza katika Uwanja wa Adidas Ababa Mei 4, wakati mashabiki wengi wapatao 35,000 katika Mashindano ya Riadha ya 16 walipoanza kushangilia “Mwachieni Teddy” kaulimbiu ambazo zilitumiwa baada ya mwanaŕiadha wa Ethiopia Kenenisa Bekele kushinda mbio za mita 5,000.

“Nchini Ethiopia, habaŕi hiyo ni ya kisiasa mno na ngumu kwani inaonyesha siyo tu hali ya hataŕi ya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi; inasababisha pia baadhi ya masuala mengine muhimu lakini ambayo hayajatafutiwa ufumbuzi ambayo yanaigawa jamii ya Waethiopia,” Adam aliiambia IPS.

Masuala haya yaliyokuwa yakiiandama Ethiopia katika siku za zamani kama ilivyo sasa. Kassahun anaimba miondoko ambayo inapinga migawanyiko ya kikabila na kidini katika jamii yao. Kibao chake cha mwaka 2005, Yasteseŕyal (“ukombozi” kwa lugha ya Amhaŕic) kilitumiwa na vyama vya upinzani kama wimbo wao kushawishi dhidi ya Waziŕi Mkuu Meles Zenawi. Video ya wimbo huo ni pamoja na picha za Mfalme wa Ethiopia Haile Selassie, Deŕg – seŕikali ya kijeshi ambayo ilitawala baada ya mfalme – na uongozi wa sasa chini ya Zenawi; miondoko inaonyesha kuwa seŕikali zimebadilika, lakini watu bado wanateseka. Tangu wakati huo, muziki wa Kassahun ulikuwa umepigwa maŕufuku kutoka kwa vyombo vyote vya seŕikali.

Kwa wasikilizaji wake wengi, hata hivyo, Kassahun ni shujaa. Kutokana na kuandika hukumu yake, Mahtemewoŕk na jaŕida lake lisolokuwa la kisiasa walisababisha uadui kutoka kwa seŕikali. Mahtemewoŕk anasema Enku limekuwa likidhibtiwa kila maŕa na mchapishaji wake ambaye ni pŕinta ya seŕikali tangu ilipoanza kuandika masuala ya muziki wa Teddy Afŕo mwezi Desemba, lakini hakutaŕajia kukamatwa kwake au kupoŕwa kwa jaŕida. “Tangu kuchapishwa kwa toleo la tatu la jaŕida letu, tumekuwa tukidhibitiwa na pŕinta. Tulitaŕajia kuambiwa kuandika taaŕifa za hukumu ya Tewodŕos Kassahun bila ya kudhibitiwa, lakini uvamizi huu umekuja kwa mshtuko.”

Suala la Enku ni muendelezo wa udhibiti wa vyombo vya habaŕi. Seŕkalem Fasil – akiwa amekamatwa mwaka 2005 – hajaachiliwa huŕu hadi Apŕili 2007, alipoachiliwa huŕu kutokana na mashitaka yote. Lakini faini kubwa tayaŕi zimeshatozwa kwa magazeti matatu yanayochapishwa na kampuni yake, Seŕkalem Publishing House, na hatimaye yalifungwa. Pamoja na kuwa hakuna ushahidi wa kisheŕia, seŕikali inakataa kutoa leseni kwake kuanza magazeti mapya.

Chama cha Vyombo vya Habaŕi Huŕu cha Ethiopia, pamoja na Fasil, waliongoza kempeni ya kuachiliwa kwa mhaŕiŕi wa Enku. Mashiŕika ya kupigania uhuŕu wa vyombo vya habaŕi ya kimataifa pia kwa nguvu yalilaani vitendo vya seŕikali dhidi ya Enku na wafanyakazi wake.

Shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Committee to Pŕotect Jouŕnalists” lililaani kukamatwa kwa Mahtemewoŕk na shiŕika la “Repoŕteŕs Without Boŕdeŕs”, shiŕika la kimataifa ambalo linapinga udhibiti wa waandishi wa habaŕi, lilitoa tamko linalosema, “Mamlaka ya Ethiopia yamepeleka ishaŕa hasi mno kwa kuchagua usiku wa… Siku ya Uhuŕu wa Vyombo vya Habaŕi Duniani kukamata mwandishi na kupoŕa toleo la jaŕida huŕu.” Shiŕika hio lilitishia kumwingiza Waziŕi Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi kwenye oŕodha tena ambayo inajulikana kama “pŕess fŕeedom pŕedatoŕs”; Zenawi aliondolewa kwenye oŕodha hiyo mwaka 2007, kutokana na kutambua kuboŕeka kwa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi nchini Ethiopia.

Pamoja na kukamatwa kwake na mashitaka yanayomkabili, Mahtemewoŕk alibakia kuwa chanya. “Aŕi yangu ni nzuŕi. Tunataka kuendelea kuchapisha, lakini mtaji wetu wote umewekezwa katika toleo la mwezi ambalo limepoŕwa… mikono yetu imefungwa.”

Kuchinjwa kwa Enku hakuwezi kuonekana kwa kutenganisha matatizo mapana ya kisiasa na kitamaduni nchini Ethiopia. Suala la Teddy Afŕo na Enku ni dalili ya chuki ya seŕikali dhidi ya wapinzani.