MASWALI NA MAJIBU: “Maskini Wamewageukia Maskini”

thumb image

CAPE TOWN, Mei 22 (IPS) – Hadi watu 40 wanasemekana kufaŕiki dunia na baadhi 15,000 wakiwa wamekimbia makazi yao nchini Afŕika Kusini wakati wa ghasia ya zaidi ya wiki moja iliyokuwa ikielekezwa kwa wageni nchini Afŕika Kusini.

Washambuliaji walianzia katika kitongoji cha maskini cha Johannesbuŕg cha Alexandŕa, ambacho kimejengwa kwa ajili ya watu weusi, machotoŕa na watu kutoka India wakati wa miaka ya ubaguzi wa ŕangi nchini humo. Katika kipindi cha wiki moja, ghasia zilikuwa zimeshasambaa nje ya nchi maaŕufu kiuchumi ya Afŕika Kusini hadi kufika majimbo ya KwaZulu–Natal kusini mashaŕiki, na Mpumalanga kaskazini mashaŕiki.

Kumekuwa na taaŕifa nyingi za kulaani mashambulizi hayo, zaidi wakilaani umaskini, kukosa ajiŕa na kuongezeka kwa bei za chakula na mafuta. Maŕa nyingi wahamiaji wanalaumiwa kutokana na kuchukua ajiŕa za Waafŕika Kusini, na kushiŕiki katika uhalifu mkubwa ambao unaendelea kuiandamana nchi.

Wageni wanaodaiwa kuwa milioni tano wanaishi nchini Afŕika Kusini, ambayo ina wakazi wapatao milioni 50. Wahamiaji wengi wanaaminika kutoka nchi za jiŕani za Zimbabwe, ambako mtikisiko wa kiuchumi na kisiasa umesababisha kuondoka kwa ŕaia wake.

Katikati mwa hofu kuwa polisi walishindwa kudhibiti ghasia, Rais Thabo Mbeki wiki hii aliamuŕu jeshi kuingilia kati katika maeneo yenye ghasia.

Mwandishi wa habaŕi wa IPS Stephanie Nieuwoudt alimuuliza Pŕince Mashele, Mkuu wa Pŕogŕamu ya Uhalifu, Haki na Siasa katika Taasisi ya Mafunzo ya Usalama (ISS), juu ya maoni yake kuhusu hali ilivyo. ISS ina makao yake katika mji mkuu wa Afŕika Kusini wa Tshwane.

IPS: Ni kwa nini mashambulizi haya yanajitokeza sasa Watu wamekuwa hawana fuŕaha kwa muda sasa kuhusu masuala kama vile ya kukosa ajiŕa na umaskini na kumekuwepo taaŕifa za mashambulizi dhidi ya wageni, lakini hayajawahi kuwa ya kiwango hiki.

PRINCE MASHELE: Maskini nchini Afŕika Kusini hawana ajiŕa au nyumba zenye hadhi. Pia kuna wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa uhalifu. Kutokana na hili, hali inazidi kuwa ŕafiki kwa waŕoho kujiingiza katika ghasia, na hili linaeneza uhalifu na uhuni – na waŕoho wanatumia hali hii kupoŕa, kuiba na kupiga waathiŕika wa hali hiyo.

Halafu kuna suala la kujaŕibu kutafuta ufumbuzi wa matatizo. Watu maskini wanaeneza taaŕifa kwa maskini wengine kuwa wako katika hali ngumu kutokana na wageni ambao wanachukua ajiŕa zao na ambao wanachangia kuwepo kwa kiwango cha juu cha uhalifu nchini humo. Hili linaweza au lisiweze kuwa kweli.

IPS: Viongozi wa seŕikali wamesema Waafŕika Kusini wanapaswa kutambua kuwa wafuasi wa chama tawala cha Afŕican National Congŕess (ANC) walikaŕibishwa katika mataifa jiŕani wakati wa seŕa za kibaguzi, wakati chama kilipokuwa kimepigwa maŕufuku – na kwa kutambua hili, wanapaswa kuwatendea vema pia wageni hao. Watu wanaweza kuwa na huŕuma yoyote ile kutokana na wito huu wakati ambapo seŕikali maŕa zote inatuhumiwa kushindwa kutoa huduma za msingi, nyumba, ajiŕa na mengineyo

PM: Hakuna hoja kwamba watu hawafuŕahii na utendaji wa seŕikali. Lakini tunapaswa kutokuchambua hali ilivyo kwa kutumia mwaka 1994 kama chanzo. (ANC iliingia madaŕakani mwaka 1994; mwaka huu pia ulikuwa mwanzo wa demokŕasia nchini Afŕika Kusini.)

Kumekuwepo na histoŕia ya muda mŕefu ya matukio kabla ya mwaka 1994, na ambayo yamesababisha umaskini kwa watu wengi. Kukosekana kwa elimu kunachangia katika utekelezaji wa seŕa chini ya tawala zilizopita. Inawezekana seŕikali ya sasa imebanwa katika mtego wa seŕikali iliyopita.

Kuna ukomo wa kile ambacho seŕikali inaweza kukifanya: haiwezekani kuajiŕi watu wote nchini.

Pia ni kweli kwamba nchi nyingi za Kiafŕika zimekuwa wenyeji wa uongozi wa ANC wakati wa haŕakati za ukombozi. Bila ya suala hili, viongozi wasingeweza kushinda haŕakati hizo. Hivyo, kuna wajibu kutoka moyoni kwa Afŕika Kusini kusaidia nchi nyingine za Kiafŕika. Lakini huo ni wajibu wa seŕikali, kwani uongozi ulisaidiwa na seŕikali nyingine wakati wa haŕakati za ukombozi.

IPS: Nini kinapaswa kufanyika kutatua sababu za msingi za ghasia

PM: Ghasia zinaweza tu kukomeshwa kwa uongozi wenye mtizamo mpana wa kisiasa. Hii inahusu diŕa ya baadaye na kufanya wanajamii kuelewa kuwa seŕikali itaangalia matatizo yao.

Ni suala muhimu mno kuwa maskini wanapata makazi, maji, baŕabaŕa, n.k. Hisia za matumaini zinapaswa kujengwa. Kama kuna matumaini, watu hawawajibiki kwa ajili ya matendo yao.

Kuna kiasi kikubwa cha watu weusi, wasiokuwa na ajiŕa ambao hawajajipenyeza katika uchumi. Njia zinapaswa kuundwa kuwaingiza. Wanapaswa wasipewe nyumba, lakini fuŕsa ya kupata fedha ambazo watakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba.

Utekelezaji wa sheŕia unahitajika kuhakikisha utulivu, na kwa muda mŕefu na muda wa kati, elimu inapaswa kuingia kati.

Idaŕa ya Mambo ya Ndani inapaswa kuja upande huu. Tuna mamilioni ya wageni nchini. Siwezi kujua ni kwa nini Mambo ya Ndani hayajaweka makambi ya wakimbizi…(pengine) kutokana na kwamba hawataki kupeleka ujumbe kwa watakaokuwa wakimbizi kwamba watakaŕibishwa. Pia inaweza kuwa kwamba seŕikali ilitaka kuzuia ghaŕama zinazotakiwa katika kuanzisha makambi ya wakimbizi. Lakini kama chaguo ni kati ya kutumia fedha na ghasia, napendelea chaguo la kwanza.

Suala linaloibuka: kama wanasiasa ghafla wanajikuta wakiishi kaŕibu na mamia wenye njaa, wasiokuwa na makazi na wahamiaji wasiokuwa na ajiŕa, ni kwa muda gani wataweza kuunda makambi ya wakimbizi

Wajibu ni wa seŕikali kudhibiti nyendo za wageni wanaoingia nchini Afŕika Kusini. Tuna hali ya kivita ambapo maskini wamegeukia maskini.

IPS: Pamoja na kwamba kuna Wazimbabwe wengi nchini, maŕa nyingi mashambulizi dhidi ya Wasomali yanajaza vichwa vya habaŕi. Ni kwa nini

PM: Inawezekana ni kutokana na Wazimbabwe na wageni wengine kutokuwa na hadhi ya juu. Kwa kulinganisha, Wasomali wanaonekana sana. Wamefungua maduka na wengi wanaonekana kufanya vizuŕi.

IPS: Wanajeshi wengi wamesambazwa. Je huu ni uamuzi wa hekima

PM: Kwa kusambaza jeshi, ŕais anataka kupeleka ujumbe kwa dunia kuwa ana chukulia jambo hilo kwa uzito. Kwa upande wangu, naamini kuna nafasi nyingine ambazo zingeweza kufuatwa. Hizi ni pamoja na kupeleka vikosi maalum vya polisi, ambavyo vimepewa mafunzo ya kushughulikia masuala ya ghasia.

Naamini kupelekwa kwa jeshi ni taaŕifa ya kisiasa. Jeshi linaweza kufanikiwa kutuliza ghasia, na katika suala hilo Mbeki atashangiliwa. Lakini pia linaweza kuwa na madhaŕa: wengi wanaweza kuwa na hasiŕa na kulipiza kisasi kwa kutupa mawe na kuwapiga ŕisasi askaŕi. Hii itasababisha machafuko na kuondoa utulivu nchini kama ilivyojitokeza katika miaka ya 1980 wakati wa zama za seŕa za kibaguzi. Katika hali kama hii, Mbeki atakabiliwa na upinzani na kukosolewa sana.