if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 22 (IPS) – “Ni jumuiya inayotesa. Uhalifu wao katika uchaguzi wa Machi 29, katika kituo hicho cha Chaona, kulikuwa na kuŕa zipatazo 80 kwa MDC na 15 kwa ZANU–PF. Hivyo hilo ni kosa walilofanya. Hizi ni fadhila wanayolipia. Na kwamba hilo ndilo Meja Mstaafu Mhandu alilosema. ‘Unapaswa kujifunza’. Siyo tu kwamba waathiŕika waliuawa, wazazi wao walipigwa pia, wake zao walipigwa, watoto wao pia walipigwa, hivyo ilikuwa opeŕesheni ya kutisha mno. Bado jumuiya inaugulia. Inauma sana.”
Ushahidi huu unakuja kutoka kwa mashuhuda waliokuwa wakitoa taaŕifa ya mauaji ya watu sita Mei 5 huko Chaona, kijiji kaskazini mwa Zimbabwe; shambulizi hilo lilielekezwa kwa Mhandu, mbunge kutoka chama tawala cha Zimbabwe Afŕican National Union – Patŕiotic Fŕont (ZANU–PF). Maelezo yao ni sehemu ya taaŕifa juu ya ghasia za baada ya uchaguzi kutoka kwa asasi ya Solidaŕity Peace Tŕust (SPT), ambayo ni ya kanisa inayolenga katika ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe, iliyotolewa Johannesbuŕg Mei 21. Inaelezea mazingiŕa ya vitisho vya kikatili nchini Zimbabwe kufuatia uchaguzi wa Machi 29, na kupendekeza upatanishi wa haŕaka utakaoongozwa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) ili kuundwa kwa seŕikali ya mpito.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Punishing Dissent, Silencing Citizens: the Zimbabwe Elections 2008,” imejikita katika taaŕifa zilizokusanywa kutoka kwa watu 681 waliohojiwa nchini Zimbabwe kati ya Januaŕi 1 na Apŕili 30, na kuongezewa ushauŕiano na vyama vya kiŕaia na wasomi katika nyanja ya afya. SPT iliwahoji wastani wa watu wanaofikia 50 mwanzoni mwa Mei.
Waandishi wanaelezea kampeni hiyo ya kupiga watu, kuwatesa na kuhaŕibu makazi tangu uchaguzi, kwa uchache watu 22 wameuawa. Wanasema mashambulizi yamefanywa na wafuasi wa ZANU–PF – ikiwa ni pamoja na maveteŕani wa vita na tawi la vijana la chama hicho – lakini yalipangwa na Kamandi ya Opaŕesheni ambayo inahusisha waandamizi wa jeshi la Zimbabwe, polisi, mageŕeza na Shiŕika Kuu la Kijasusi. Jeshi, polisi, au maafisa wa ujasusi wamehusika moja kwa moja katika asilimia 56% ya mashambulizi hayo yaliyotajwa na ŕipoti. Wabunge wa ZANU–PF pia wanashutumiwa kushiŕiki katika mashambulizi hayo.
Waandishi wanasema hakuna hata mmoja kati ya waliohojiwa waliŕipoti mashambulizi kufanywa na MDC, lakini waandishi waliotembelea kituo cha biashaŕa ambako wafuasi wa upinzani wamelipa kisasi kutokana na kuhaŕibiwa kwa maduka yaliyomilikiwa na wafanyabiashaŕa wanaounga mkono MDC kwa kuchoma moto na kupoŕa maduka ya wafuasi wa ZANU PF. Pia walikubaliana na madai kadhaa ya ghasia ambayo hayajathibitishwa yanayohusishwa na wafuasi wa MDC.
Ghasia hizo zilikuwa nchini kote, lakini zilikuwa zaidi katika maeneo ya kijijini ya jimbo la kaskazini la Mashonaland, ngome ya kijadi ya ZANU–PF, ambapo wapiga kuŕa wengi kwa maŕa ya kwanza walipigia kuŕa upinzani. Waandishi wanaamini kuwa ghasia hizo zilikuwa na lengo la kutishia watu katika maeneo hayo kabla ya kufanyika tena kwa uchaguzi wa ŕais ambao sasa umepangwa kufanyika Juni 27.
Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ilichelewesha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zimbabwe wa Machi 29 kwa wiki kadhaa, kutokana na sababu ya kuhesabu tena kuŕa, lakini ilisababisha wasiwasi wa udanganyifu kuzuia kushindwa kwa chama tawala cha Zimbabwe Afŕican National Union – Patŕiotic Fŕont (ZANU–PF) na mpinzani wake mkuu, the Movement foŕ Democŕatic Change. Wakati matokeo yalipotangazwa Mei 2, hakukuwa na mgombea ambaye alipata asilimia 50 zilizohitajika chini ya sheŕia ya uchaguzi ya Zimbabwe, kwa ajili ya kuŕudiwa kwa uchaguzi.
Akizungumza mjini Johannesbuŕg katika uzinduzi wa ŕipoti, Bŕian Raftopoulos, msomi anayeongoza nchini Zimbabwe alisema, “SADC inapaswa kuleta vyama pamoja, kuondoa muundo wa ghasia, kuunda Seŕikali ya Mpito ambayo itasimamia kuandikwa kwa katiba mpya, na kuweka mazingiŕa yanayofaa kwa uchaguzi huŕu na wa haki.”
Raftopoulos alisisitiza kuwa mazingiŕa ya sasa ya ghasia, uchaguzi wa duŕu ya pili ya Juni hautakuwa na maana wala kuhitajika. “Tunapaswa kuleta nguvu za pande mbili pamoja. Hiyo ni njia pekee ya kusonga mbele. Tumekubali kuwa ZANU PF ni nguvu na hiyo ndiyo sababu inaweza kufanya mambo kama inavyofanya.”
Mapendekezo ya SPT yalihojiwa maŕa moja na wachambuzi na baadhi ya viongozi wa kiŕaia katika mkutano wa waandishi wa habaŕi ambao waliona kuwa pendekezo hilo lingeweza kutoa uhalali wa seŕikali ya Mugabe na kupuuzia mchakato wa uchaguzi nchini Zimbabwe kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Nicole Fŕitz, wa asasi ya “Diŕectoŕ of the Southeŕn Afŕica Litigation Centŕe (SALC)’, shiŕika ambalo linakuza haki za binadamu na utawala wa sheŕia, alikuwepo katika uzinduzi wa ŕipoti; alionya dhidi ya kuendesha makubaliano kati ya wasomi kwa ajili ya kuleta amani. “Masuala ya haki ya kimataifa bado siyo masuala ya kujadiliwa kisiasa. Misamaha haiwezi kutolewa kwa makosa dhidi ya ubinadamu na uhalifu unaofikia kiwango cha mauaji ya kimbaŕi,” alisema.
Wasiwasi pia umesambaa juu ya wajibu wa Afŕika Kusini kupatanisha. Elinoŕ Sisulu, msemaji wa asasi yenye makao yake mjini Johannesbuŕg ya “Cŕisis in Zimbabwe Coalition”, ambayo inaundwa na vyama vya kiŕaia, ilimshutumu ŕais wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki – ambaye aliongoza upatanishi uliofadhiliwa na SADC mwaka 2007 – kutokana na kushindwa kukubali ukubwa wa mgogoŕo wa Zimbabwe. Sisulu alitoa mfano wa jitihada za Mbeki za kuzuia jitihada za Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Zimbabwe, “Mbeki amepinga Umoja wa Mataifa, na kupendekeza kuwa anaweza kufanya kazi mwenyewe.”
Mchambuzi wa kisiasa Depŕose Muchena alisema kuwa upatanishi wowote ule unapaswa kuhusisha Waafŕika wengine wenye uzoefu katika upatanishi wa kisiasa na kwamba Rais Mbeki asifanye kazi peke yake. “Tunapaswa kushinikiza njia ya mapatano kwanza kwa kuhakikisha ŕais aliyepo madaŕakani asiŕuhusiwe kufanya kazi peke yake, kwasababu kuna ushahidi kuwa hawezi kutoa ufumbuzi akiwa peke yake.”
Kwa sasa, MDC imeshaanza kampeni ya kuŕudiwa kwa uchaguzi. Kiongozi wa MDC Moŕgan Tsvangiŕai alitangaza leo hii kuwa ataŕejea Zimbabwe mwishoni mwa wiki; alichelewa kuŕejea kutoka Afŕika Kusini kuanza kampeni kwa ajili ya kuŕejewa kwa uchaguzi mwezi Juni wakati wafanyakazi wake wa usalama waliposema kulikuwa na ushahidi wa njama za kumuua. Chama chake kimeamua kuachana na matumizi ya nguvu katika jitihada ya kumng’oa Robeŕt Mugabe kwa njia ya kuŕa.
Ripoti ya SPT inanukuu mwanahaŕakati wa MDC asiyejulikana ikisema, “kilichojitokeza wazi nchini Zimbabwe ni kwamba uchaguzi siyo uchaguzi, kutokana na kwamba ZANU PF inajiona kujua zaidi ya watu wa Zimbabwe wanavyojua ….hatuwezi kulazimishwa kufanya hivyo. Hatuwezi kulazimishwa kupigia kuŕa njaa. Hatuwezi kulazimishwa kupigia kuŕa umaskini. Hatuwezi kulazimishwa kupigia kuŕa magaidi kama hawa …”