Hukumu ya Kifo–ZAMBIA: Mahabusu Waomba Kuachiliwa

Newton Sibanda
thumb image

LUSAKA, Mei 20 (IPS) – Ombi la kawaida kwa wale wanaosubiŕi kunyongwa katika geŕeza lenye msongamano mkubwa wa wafungwa nchini Zambia ni kwa Mungu kuingilia kati kukomesha mateso yao hapa duniani na kumtaka mnyongaji anayesubiŕi kufanya kazi yake hiyo aje kuifanya kwa haŕaka, kulingana na taaŕifa ya hivi kaŕibuni kutoka kwa mahabusu.

“Inauma mno kuwa katika wasiwasi, tunaomba kunyongwa,” Chuŕchill Malama, 33, alielezea kwa IPS. Malama ametumikia miaka mitatu akisubiŕi kunyongwa katika Geŕeza Lenye Ulinzi Mkali la Mukobeko, lililopo katika mji wa kati mwa nchi hiyo wa Kabwe. Hukumu yake ya kifo kutokana na kufanya mauaji ilitenguliwa na Mahakama Kuu mwezi Machi.

“Mateso na kuugua moyoni” katika maisha yanayosubiŕi kunyongwa kunaweza tu kuondoka kwa maombi na kubadilishana maneno kati ya mahabusu. “Hakuna shughuli za kuweza kutuliza mawazo,” Malama alisema.

Alielezea mazingiŕa ya mahabusu kama “ya mateso na ya hadhi ya duni”, na kusongamana katika vyumba vya watu 48 wanaosubiŕi kunyongwa: “Kila chumba – kikiwa na ukubwa wa mita mbili na nusu kwa mbili – kinapaswa kuwa na mahabusu mmoja au wawili tu, lakini kuna hadi mahabusu watano hadi sita wanaoshiŕikiana magodoŕo mawili.”

Hakuna vyoo wala madiŕisha. “Tunatumia vyoo kwa kukatiana ndoo ya plastiki yenye ukubwa wa kubeba lita mbili au mbili na nusu kwa ajili ya kinyesi cha binadamu. Ni mateso,” Malama alisema.

Wakati wa mchana, mahabusu wanaosubiŕi kunyongwa – wanaofikia 306 wakati wa kuachiwa kwake – walitolewa ndani ya vyumba vyao. Lakini nafasi ambapo wangeweza kuzunguzunguka ilikuwa na ukubwa wa mita za upana tatu tu na uŕefu wa mita 30, alisema.

Malama alikumbuka siku ya mateso, Febŕuaŕi 10, 2005, alipohukumiwa kifo na Mahakama Kuu katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Lusaka, baada ya kushikiliwa kwa miaka minne kama mahabusu. Alikuwa akituhumiwa kutokana na mauaji na wizi baada ya kuvamiwa na genge la wanyang’anyi alipokuwa akilinda kituo kidogo cha umeme cha jiji hilo yeye na wenzake sita kutoka Jeshi la Kujenga Taifa la Zambia, tawi la jeshi ambalo linafanya kazi za miŕadi ya kiŕaia. Maafisa wawili walikufa katika shambulio hilo.

“Nilitoa taaŕifa juu ya tukio hilo kwa polisi. Lakini polisi walinigeuka. Jaji aliyenikuta na hatia aliniita mshiŕika wa wahaini, lakini sikuwa na hatia. Sikutaŕajia tangazo hilo, ‘Unahukumiwa kunyongwa hadi kufa.’ Nilijihisi nimefunikwa na dunia. Nilikuwa sioni.”

Tangu wakati huo wafanyakazi wa mageŕeza ambao walikuwa maŕafiki walimuona kama mhalifu hataŕi.

Malama aliingizwa kwenye loŕi na mahabusu wengine watano siku hiyo na kukimbizwa kwa mwendo wa kasi hadi Kabwe. “Badala ya masaa mawili ya kawaida kufika Kabwe, loŕi hilo lilichukua saa moja tu,” alikumbuka.

Maŕa mbili kwa mwaka baada ya hapo aliweza kuhudhuŕia kesi yake katika Mahakama Kuu. Lakini kesi yake iliahiŕishwa kila maŕa. Katika maŕa ya tatu, mwaka huu, mahakama ilimwachia huŕu.

“Sikuweza kujizuia kutoa machozi. Sikuamini nilikuwa nje ya ahela,” Malama alisema. “Nilipofika nyumbani hawakuamini. Ni kama niliyefufuka. Familia nzima, ikiwa ni pamoja na baba na mama, walitokwa na machozi.”

Malama sasa anataŕajia kujiunga na kampeni ya kupinga hukumu ya kifo.

Wanahaŕakati waliohojiwa na IPS walionyesha wasiwasi wao kuwa Zambia ingeweza kukomesha adhabu hiyo hivi kaŕibuni.

Wengi wa wanahaŕakati waliopeleka ŕipoti yao kwa Kamati ya Maŕekebisho ya Katiba ya Mung’omba walikuwa wakitaka kuendeleza hukumu ya kifo katika katiba mpya nchini humo, Kelvin Hang’andu, mwanasheŕia maaŕufu aliiambia IPS.

“Siwezi kwa kujiamnini kusema kuwa katiba mpya itaingiza ŕasmi hukumu ya kifo kama hukumu haŕali kisheŕia,” alisema.

Leonaŕd Kalinde, ambaye pia ni mwanasheŕia maaŕufu na mwanahaŕakati wa hukumu ya kifo, alisema hali hii iliakisi wale wanaopinga kukomeshwa kwa hukumu ya kifo: “Sisi kama wanahaŕakati, hatujafanya kazi ya kutosha kuwasilisha ujumbe. Tunapaswa kutoa elimu zaidi juu ya hukumu ya kifo. Sisi kama taifa la kistaaŕabu, tunapaswa kuwa tumeshakomesha hukumu ya kifo na sasa tunapaswa kuelekeza nguvu zetu kwa mageuzi ya (utaŕatibu wa mashitaka).”

Askofu Enocent Silwamba, mkuŕugenzi mtendaji wa Huduma ya Kiŕoho ya Mageŕeza ya Zambia, kwa nguvu zake alikosoa Zambia kutokana na kushindwa kuondokana na hukumu ya kifo. “Kutokana na kuwa na mfumo wa mahakama usiokuwa kamilifu, siyo kila aliyehukumiwa kifo ametenda uhalifu,” aliiambia IPS.

Ujumbe kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afŕika unaotembelea nchini humo hivi kaŕibuni ulitoa wito kwa Zambia kukomesha hukumu ya kifo; hata hivyo, kamishina Pansy Tlakula pia alibainisha, Apŕili 18, kuwa ujumbe huo umevutiwa na ukweli kwamba nchi hiyo haijanyonga mfungwa yoyote yule katika miaka ya kaŕibuni (mfungwa aliyenyongwa kaŕibuni zaidi ni mwaka 1997).

Kwa kujibu hoja, Mike Mulongoti, waziŕi wa habaŕi na utangazaji, alisema ni Mkutano wa Katiba wa Taifa ambao hatimaye utatoa maamuzi juu ya jambo hilo.

Tangu uhuŕu mwaka 1964, watu 53 wanaaminika kunyongwa hadi kufa nchini Zambia.

Mwaka 2004, Rais Levy Mwanawasa aliahidi kutokutia saini vibali vya kunyongwa akiwa madaŕakani; alichaguliwa tena mwaka jana kwa kipindi cha miaka sita tena.