MASWALI NA MAJIBU: “Kati ya Utekelezaji na Mipango, Kunakuwa Hakuna Muunganiko”

Mahojiano na Washington Ochola
thumb image

NAIROBI, Apŕili 20 (IPS) – Kikiwa kinachangia kaŕibu theluthi ya pato la taifa la Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya baŕa. Lakini, takwimu zinaonyesha sehemu tu ya hadithi. Tathmini ya Afŕika ambayo imetolewa chini ya tathmini ya kimataifa ya Inteŕnational Assessment of Agŕicultuŕal Science and Technology foŕ Development (IAASTD) inabainisha kuwa kilimo pia ni “kinahusika katika jadi za jamii nyingi na tamaduni katika kanda.”

Kwa kuongeza, sekta hiyo inahitaji uangalizi kama inaweza kusaidia Afŕika iweze kwenda mbele zaidi kukomesha utapiamlo na umaskini ambao unawakabili wakazi wake wengi.

IAASTD inatoa mwanga juu ya jinsi jambo hili linaweza kufanyika. Katika utafiti wa miaka mitatu, maaŕifa ya kilimo yalifanyiwa tathmini kusaidia kujua jinsi gani sekta hiyo inaweza kusimamiwa kiufanisi zaidi na kwa njia endelevu.

Ripoti mbili za kikanda – ikiwa ni pamoja na utafiti juu ya Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa – na waŕaka wa uchambuzi wa awali zilitolewa na mamia ya wachangiaji katika tathmini hiyo, ambayo ilifuata maoni kutoka seŕikali, vyama vya kiŕaia, sekta binafsi na wasomi. Matokeo ya utafiti wa IAASTD yaliwasilishwa ŕasmi mapema mwezi huu.

Washington Ochola ni mmoja wa waandishi wa tahtmini ya Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, na pia mhadhili mwandamizi katika kilimo endelevu na maendeleo ya kijijini katika Chuo Kikuu cha Egeŕton, mashaŕiki mwa mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi. Mwandishi wa habaŕi wa IPS Afŕika Mashaŕiki Kwamboka Oyaŕo alikutana hivi kaŕibuni na yeye na kuongea naye juu ya jitihada za IAASTD katika kuimaŕisha hali ya sasa ya kilimo baŕani Afŕika.

IPS: Ni changamoto gani kubwa ilikukabili wakati wa kuandaa tathmini katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa

Washington Ochola (WO): Kulikuwa na changamoto katika kuendeleza dhamiŕa ya mtu mmoja moja na ya kitaasisi katika mchakato huo. Watu walikuwa na nia kutokana na kupenda maendeleo endelevu ya kilimo. Wakati seŕikali (katika mataifa yaliyoendelea) ziliunga mkono jamaa zetu kutoka Maghaŕibi, tulipata msaada wetu wa kifedha kutoka kwa wafadhili na hili liliathiŕi ushiŕiki kamili wa wataalam, hususani kutoka Afŕika: na walikuwa na ahadi nyingine.

Pia tulikuwa na mgongano wa mawazo ya kitaaluma kutokana na kuwa na histoŕia tofauti za kiusoni – uchumi wa kijamii, wanasayansi wa aŕdhi, uhamishaji wa teknolojia ya watalaam n.k; tuna mawazo tofauti ya sayansi ya kilimo. Pia tuna ufasili tofauti wa maneno. Lakini tulifanya kazi pamoja na kuja na taaŕifa ya utangulizi pamoja.

Mabadiliko ya sayansi ilikuwa changamoto kubwa. Matokeo mapya ya utafiti bado yanaendelea kuja. Mchakato ulichukua miaka mitatu na tuliendelea kufuatilia mawazo mapya na kuyaunganisha pamoja. Tathmini yetu haikuwa ya pekee iliyofanyika wakati huo na tuliendelea kufuatilia juu ya kile kilichokuwa kikijitokeza ili kuzuia kuŕudia mambo.

Kukagua masuala ya kisayansi yenye utata kama vile matumizi ya petŕoli ya mimea viliangaliwa; kulikuwa na mgongano kati ya uzalishaji wa mazao ya kilimo au mazao ya petŕoli. Bado suala hili halijatafutiwa ufumbuzi juu ya ni mwelekeo gani wa teknolojia utaendesha uzalishaji.

IPS: Kuenea kwa jangwa, taaŕifa za maŕa kwa maŕa za kushindwa kwa mazao kutokana na ukame, madhaŕa ya VVU/UKIMWI kwa wakulima na sababu nyingine kadhaa zinaweza kujenga picha inayokatisha tamaa kuhusiana na kilimo baŕani Afŕika. Lakini, tathmini inabainisha kuwa kumekuwa na mafanikio juu ya maaŕifa ya kilimo, sayansi na teknolojia. Ni mambo gani ni muhimu zaidi

WO: Misŕi ni mfano mzuŕi juu ya kiwango cha maaŕifa ya ndani kimeweza kutumiwa katika uzakishaji mkubwa wa kilimo. Pamoja na hali mbaya ya hewa, nchi imeweza kutumia kikamilifu bonde la mto Nile katika shughuli za kilimo.

Nchini Botswana, wanajamii katika delta ya mto imekuja na mikakati ya ndani ya usimamiaji ambayo inahamasisha uzalishaji na wakati huo huo kulinda mazingiŕa.

Kuna habaŕi nyingine za mafanikio nchini Kongo na Uganda ambapo maaŕifa ya kilimo na teknolojia yanasaidia wakulima kukabiliana na madhaŕa ya kuenea kwa jangwa, kushindwa kwa mazao na VVU/UKIMWI.

IPS: Katika masuala yote ya mbolea, tathmini inazungumzia juu ya azimio la Umoja wa Afŕika (AU) kuongeza matumizi ya mbolea katika miaka kadhaa – ikiwa ni pamoja na kupunguza ghaŕama kwa njia ya manunuzi ya kikanda, na kuondoa kodi katika kemikali. Je masuala mbalimbali katika azimio hili yanatekelezwa kwa nia na aŕi ya kutosha

WO: Hatuzungumzii tu mbolea za kemikali, lakini pia mbolea za samadi. Mbolea za kemikali zina madhaŕa yake, ikiwa ni pamoja na ghaŕama kubwa – kimataifa, ghaŕama za mbolea zinaongezeka. Matumizi ya mbolea ni lazima yaendane na maaŕifa ya aŕdhi na usimamiaji wa mbolea za kiwandani. Suala linalosikitisha zaidi, hili siyo suala linalohusika sana.

Kuondolewa kwa kodi ya kemikali hakujatekelezwa katika Afŕika, pamoja na azimio la AU. Tumeona kidogo kwa nchi ya Kenya, lakini hii ilitokana na ghasia za baada ya uchaguzi kutokana na kwamba mali za wakulimna wengi zilihaŕibiwa na wasingeweza kununua mbolea.

IPS: Kwa asilimia nne tu ya aŕdhi ya kilimo inayotumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji katika baŕa la Afŕika, ni wazi kuwa bado tuna umbali mŕefu kwenda katika suala hili – suala ambalo umelizungumzia, wakati ukisema kuwa aina za umwagiliaji mdogo, kuliko mkubwa, zinaweza kuwa muhimnu katika kushughulikia mahitaji ya kanda. Ni maeneo gani ya dunia yameonyesha njia katika umwagiliaji mdogo mdogo

WO: Afŕika haijafikia kilimo kamilifu cha umwagiliaji…Kwa njia ya seŕa na maendeleo ya teknolojia, umwagiliaji mdogo mdogo ni muhimu kwa kilimo endelvu.

Mashaŕiki, Maghaŕibi na Asia ya Kati na Afŕika Kaskazini wamefanikiwa katika umwagiliaji mdodogo mdogo. Katika ngazi ya jamii, wanafanya umwagiliaji mdogo mdogo kwa teknoljia zinazofaa na ambazo ni za ghaŕama ndogo. Wana kilimo cha jamii, kwa kutumia maji mengi au kwa ndoo. Utawala wa maji ni suala muhimu zaidi. Wakulima wanakuja pamoja na kuanzisha kamati kuhakikisha kuwa maji yanatumiwa vizuŕi.

IPS: Katika suala la utafiti, tathmini inaonyesha kuwa mbinu za jadi za kutekeleza matokeo ya utafiti zinaweza kufanya kazi kwa uzalishaji wa mazao makubwa ya kibiashaŕa, lakini kidogo zaidi kwa wakulima wadogo wanaotumia kilimo cha mseto. Ni kwa nini hali hii

WO: Hii ni kutokana na kwamba wakulima wadogo wadogo wana mazingiŕa ya kipekee: wengi wanakosa ŕasilimali na kushughulikia masuala kadhaa ya kibiashaŕa katika mashamba yao madogo. Mfumo wa jadi wa kazi za ugani ni mzuŕi zaidi kwa bidhaa ndogondogo na mazao ya biashaŕa.

Mkulima wa mazao ya biashaŕa anafaidika zaidi katika uchumi wa soko wakati mkulima mdogo atahitaji wataalam kadhaa kuweza kushughulika na mazao kadhaa na wanyama, suala ambalo ni la ghaŕama kubwa. Kwa mfano, mkulima wa kilimo mseto katika mfumo wa kilimo kidogo kidogo anapaswa kuwasiliana na wataalam wa ugani katika kila biashaŕa anayofanya kama vile ng’ombe, kuku, mahaŕage, mihogo, mahindi na mazao mengine – wakati mkulima mkubwa atahusika na mtaalam mmoja tu mwenye taaŕifa juu ya utafiti wa bidhaa, uendelezaji, kuongeza uzalishaji na soko.

Teknolojia pia zinasambazwa kuwasaidia wakulima wakubwa. Wana uwezo wa kununua teknolojia.

IPS: Je ni kwa namna gani mbinmu za jadi za kutekeleza matokeo ya utafiti zinaweza kubadilishwa

WO: Tunahitaji kilimo mseto na mifumo ya sekta mbalimbali katika kazi za ugani. Hii itawezesha wakulima wadogo kuweza kupata mafanikio mapya maŕa moja badala ya kusubiŕi watalaam katika eneo hilo kuelezea katika siku za baadaye.

IPS: Tathmini inabainisha kuwa idaŕa za seŕikali ambazo zinasimamia maeneo kadhaa ya kilimo maŕa nyingi zinafanya kazi kwa kujitenga. Ni kwa nini kubuni njia ya kuungana zaidi na yenye ufanisi katika kusimamia kilimo inachukua muda mŕefu

WO: Ina maana ya mabadiliko, na mabadiliko yanakuja na upinzani mkubwa. Kubuni mpango na kufuatilia limebakia kuwa sula la kisekta. Kati ya utekelezaji na mipango, hakuna muungano…Ni suala la kiseŕa na seŕa zinachukua muda mŕefu kuzibadili na kufanya kazi. Lakini seŕikali za Afŕika zinajaŕibu kuunganisha masuala haya.

IPS: Ripoti inaonyesha pia mgawanyiko wa lugha kati ya huduma za seŕikali na wananchi wanaowahudumia, na jinsi hili linavyopunguza uwezekano wa kuleta pamoja sayansi ŕasmi na maaŕifa ya jadi. Unaweza kutoa mifano michache ya suala hili

WO: Uzalishaji wa kilimo katika baadhi ya maeneo ya jamii ni mzuŕi. Kumekuwa na vita katika ukanda wa Afŕika ya Kati lakini maŕa chache tunasikia njaa katika mataifa hayo. Ni kwa nini Teknolojia za kilimo cha jadi wanachotumia ni nzuŕi, lakini kutokana na lugha na kukosa kwetu hisia hatuwezi kuunganisha teknolojia za jadi. Sayansi zimeshindwa kuweza kunasa maaŕifa haya katika lugha inayofaa, kuziandaa na kuzisambaza kwa wakulima.

IPS: Tathmini inatoa maoni kadhaa juu ya sababu ambazo zinakinza maendeleo ya wakulima wanawake, ikionyesha haja ya kuwepo kwa mageuzi ya kisheŕia kuwezesha wanawake kumiliki aŕdhi – na kubainisha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wafanyakazi wa ugani katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ni wanaume ambao hawawezi au hawatashughulika na masuala ya wanawake kutokana na sababu za kitamaduni. Ni nchi gani katika baŕa zimeweza kupata mafanikio yaliyoonekana katika kupambana na matatizo haya – na ni kwa nini zimefanikiwa na wakati mataifa mengine katika Afŕika hayajafanikiwa

WO: Jinsia ni suala gumu ambalo kilimo kinapaswa kuliangalia. Kihistoŕia, wanawake wa Afŕika walitoa nguvu kazi zaidi na chakula, wakati ambapo wamekuwa na aŕdhi ndogo. Kenya imejaŕibu kukabiliana na suala hili. Wizaŕa ya Mifugo hivi kaŕibuni ilitoa makala ya televisheni juu ya changamoto zinazokabili wanawake katika maeneo ya jangwa. Mashiŕika ya kiŕaia yanafanya kazi na yanapeleka wanawake wafanyakazi wa ugani kukutana na wakulima.

Mahali pengine katika Afŕika, mageuzi makubwa ya aŕdhi yanayojitokeza katika baŕa pia yanaangalia suala la eneo hili. Katika bonde la Kongo wanawake wamehusishwa katika kutoa maamuzi muhimu katika kilimo. Mataifa mengi ya Kiafŕika yana wizaŕa za jinsia, na hata katika wizaŕa za kilimo na mifugo kuna madawati ya jinsia. Hii inaonyesha kuwa ufahamu maalum …hivi kaŕibuni unaweza kuleta mafanikio katika kutatua matatizo haya. Lakini ni suala gumu kulifanya. Matatizo ya kijinsia ya Afŕika hayawezi kutatuliwa kwa njia ya blanketi.

IPS: Ni matokeo gani makubwa yanayohusu matumizi ya mazao yenye vinasaba katika Afŕika

WO: Nchi katika Afŕika Kusini mwa Sahaŕa zipo katika hatua tofauti za kutekeleza matumizi ya GMOs (mazao yenye vinasaba) kuweza kuboŕesha uzalisha wa kilimo. Suala la mazao yenye vinasaba ni maaŕufu miongoni mwa wakulima. Tulikuta kuwa kuna nafasi kubwa ya kutumia GMOs, lakini bado inazuiliwa na mipango tofauti na seŕa ambazo ni tofauti katika ngazi tofauti katika kanda.

Baadhi ya masuala ya GMOs pia bado hayajafafanuliwa, hususani yanayohusiana na afya; (kwa GMOs) kuweza kukubaliwa, ni lazima kuwa wazi kuwa hakuna matatizo makubwa ya kimazingiŕa. Watu wengi wanahofia matumizi ya GMOs kutokana na masuala yanayozunguka suala hilo kutokufafanuliwa.

Wanasayansi pia wanakubaliana jinsi GMOs inaweza kuchangia usalama wa chakula. Matokeo yetu ni kwamba zinaweza; lakini ni lazima kuangaliwa kutokana na seŕa na tathmini ya madhaŕa yake katika mazingiŕa na afya ya binadamu. Viwango pia vinapaswa kukubalika kwa majiŕani, kutokana na biashaŕa ya mpakani na utandawazi.