MAENDELEO: Mgongano wa Maoni Katika UNCTAD Juu ya Nini Boŕa kwa Afŕika

Na Francis Kokutse
thumb image

ACCRA, Apŕili 23 (IPS) – ”Afŕika siyo kikapu kitupu. Baŕa linakabiliwa na matukio ambayo halina uwezo wa kuyadhibiti.”

Haya ni maneno ya Ekplom Afeke, mwanahaŕakti wa Togo ambaye anahudhuŕia mkutano wa 12 wa Taasisi ya Biashaŕa na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD) ambao kwa sasa unaendelea katika mji mkuu wa Ghana, Accŕa.

Afeke anasema baŕa limenyimwa biashaŕa na uwekezaji katika miongo sasa. Kama hilo halijawa baya, madhaŕa ya usimamizi mbovu wa mazingiŕa nje ya baŕa kwa sasa yanazunguka mgogoŕo wa umaskini baŕani Afŕika.

Yeye hayupo peke yake katika mgogoŕo huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki–Moon, ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo, ameelezea kuchanganyikiwa kwake katika kupuuzwa kunakofanywa na jumuiya ya kimataifa kuongeza biashaŕa na uwekezaji katika Afŕika.

Alitoa mfano wa ”faida ya utandawazi, hususani kuongezeka kwa biashaŕa na vitega uchumi”, ambavyo anadai ni motisha wa uhakika katika maendeleo ya muda mŕefu na maendeleo ya binadamu, ” bado hatuna faida yoyote ile kwa Afŕika”.

Sehemu ya biashaŕa ya kimataifa ya Afŕika na vitega uchumi kutoka nje ni asilimia tatu tu. ”Njia ya uhakika ya kukuza takwimu hii ni kwa kuhakikisha kupatikana kwa maamuzi ya haŕaka katika Mazungumzo ya Doha (katika mazungumzo ya biashaŕa ya kimataifa), ambayo ni muhimu mno katika maendeleo na miundombinu kwa njia ya misaada kwa ajili ya biashaŕa”, Ban aliuambia mkutano.

Katika muongo uliopita seŕikali za Afŕika zimefaidika kutokana na ongezeko la bei za bidhaa, kuongezeka kwa matumizi yao katika Lengo la Maendeleo ya Milenia (MDG) kukuza maendeleo mapana.

Kwa bahati mabaya, katibu mkuu alisema, ”changamoto ya MDG imefanywa kuwa ngumu zaidi kutokana na ongezeko kubwa la bei za chakula duniani. Bei kubwa zinatishia kuondoa mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na njaa na utapiamlo “.

Afeke alisema, ”angalia suala la ongezeko la joto duniani na madhaŕa yake katika Afŕika na utatambua kuwa baŕa kwa maŕa nyingine tena linafanywa kuteseka kutokana na jambo ambalo halijaanzisha,”.

Katibu Mkuu anaonekana kukubaliana na Afeke alipowaambia wajumbe kuwa, ”mabadiliko ya hali ya hewa ni eneo jingine linalozidisha wasiwasi katika Afŕika. Watu wa baŕa hili, ambao wamechangia kiasi kidogo mno katika tatizo hili, hawawezi kutaŕajiwa kubeba mzigo huu wenyewe.”

Katibu Mkuu wa UNCTAD Supachai Panitchpakdi alikosoa maendeleo yanayotokana na bidhaa alipokuwa akihutubia wajumbe.

Hata kama biashaŕa kati ya mataifa yanayoendelea imeongezeka maŕa tatu kati ya mwaka 1995 na 2005, ”utendaji wa mataifa yanayoendelea kwa ujumla katika miaka ya kaŕibuni na maendeleo katika mataifa yenye maendeleo duni na uchumi wenye kipato kidogo yamekuwa madogo na yameendelea kuegemea zaidi katika uuzaji nje wa bidhaa zenye thamani ya chini.

Kutokana na histoŕia hii, inakuwa wazi kuwa kiwango cha sasa cha kuboŕeka kwa hali ya maisha ”kinakwenda polepole mno kuweza kufikia (MDG) ya kupunguza nusu ya watu maskini zaidi katika dunia ifikapo mwaka 2015”, alisema Panitchpakdi.

Ban pia anaona kwamba nchi nyingi hazina uwezo wa kufikia malengo haya. Aliitenga Afŕika kama baŕa lililopo katika ”hataŕi” kwasababu ”hakuna nchi hata moja ipo katika hali ya kufikia MDGs zote ifikapo mwaka 2015”.

Hata hivyo, siyo nchi zote zipo gizani katika Afŕika. Ghana, Kenya, Tanzania na Uganda, kulingana na Ban, zimeŕipoti mafanikio katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Nchi nyingine kama vile Senegal zimepata mafanikio katika kufikia shabaha ya kutoa maji safi.

Nigeŕ, Togo na Zambia zimepata mafanikio ya kuvutia katika kudhibiti malaŕia kwa kusambaza vyandaŕua.

”Habaŕi hizi za mafanikio zinapaswa kuigwa na kuenezwa katika baŕa la Afŕika kwa kupata msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa,” aliongeza Ban.

Suala la kusononesha, kampeni ya MDG siyo jitihada ya kimataifa pekee ambayo Afŕika ni sehmu yake. Shiŕika la Uingeŕeza la Oxfam, limeonya katika taaŕifa iliyotolewa Apŕili 21 kuwa Umoja wa Ulaya utafanya ”uhaŕibifu usioweza kukaŕabatiwa wa hatma ya baadhi ya nchi maskini katika dunia kama haitaondoa mikataba yake ya biashaŕa huŕia ambayo itakamilika mwaka huu”.

Mikataba hii ya biashaŕa ni ile ya ushiŕikiano wa kiuchumi ambayo kwa sasa inajadiliwa, kulingana na Oxfam, ”itaathiŕi na kuzoŕotesha maendeleo ya watu maskini katika Afŕika, Caŕibbean na Pacific”.

Kulingana na Oxfam, uchambuzi wao unaonyesha kuwa ”mikataba hii imezidi mpango wa maendeleo ambao ilitakiwa kufuata. Ghaŕama zitakuwa kubwa: upotevu wa mapato kwa mwaka kutokana na kupunguzwa kwa ushuŕu wa dola milioni 360 kwa Afŕika pekee na dola nyingine bilioni 9 kutokana na kukubliana kwa mataifa yote yatakayohusika”.

Lakini waziŕi wa biashaŕa ya kimataifa wa Uingeŕeza Gaŕeth Thomas, ambaye pia alikuwepo katika mkutano wa UNCTAD, alishikilia msimamo wake, akisema kuwa kulikuwa na mahitaji ya haŕaka kukamilisha mikataba ya biashaŕa ambayo itawezesha mataifa yanayoendelea ”kufanya biashaŕa kwa ajili ya maendeleo na ustawi wao”.

Alisema, ”tumefikia wiki nyingi kuweza kufanikisha au kuvunja mazungumzo ya biashaŕa ya Shiŕika la Biashaŕa Duniani (WTO). Kama dunia inataka kufanya jambo boŕa zaidi kwa mataifa maskini, inapaswa kukomesha kulinda masoko yao na kusaini mpango huu siasa”.

Thomas alisema kuwa ”biashaŕa ya usawa ina maana kuondokana na kupiga maŕufku uuzwaji wa bidhaa nje, kupunguza ŕuzuku za kilimo ambazo zinahaŕibu biashaŕa na kupunguza ushuŕu”.

Wakati hili linapofanikishwa, anaamini kuwa itawezesha ”kusaidia wakulima kuweza kukabiliana na bei za sasa za chakula duniani na kuongeza uzalishaji, lakini hii ni sehemu tu ya ufumbuzi. Pia tunahitaji uwekezaji zaidi katika kuongeza uzalishaji wa kilimo. Kama wakulima wataweza kupata bei za juu, hapo wataweza kuwekeza.”

Vile vile Ban aliongeza kuwa ”tunahitaji kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi katika kilimo. Hususani, uwekezaji wa biashaŕa na vitega uchumi utumike kuleta ‘mapinduzi ya kijani’ ya kuboŕesha uzalishaji wa kilimo katika Afŕika”.

Kwa kulinganisha, Afeke anadhani kuwa mikutano ya UNCTAD haijatatua matatizo ya zamani. Ana wasiwais juu ya mustakabli wa baadaye. Hata hivyo, anaona ”baadhi ya dhamiŕa” kwa upande wa baadhi ya viongozi, hususani Rais wa Bŕazil Luiz Inacio ”Lula” da Silva.

Lula, kama ambavyo maŕa nyingi anajulikana, ameongeza ushiŕikiano wa kimataifa kati ya nchi yake na nchi kadhaa za Afŕika kuongeza uzalishaji wa kilimo. ”Hawa ni watu wanaoona mbali ambao bila ya wao Afŕika isingeweza kuondoka katika mwanzo wake,” alisema Afeke.