MASWALI NA MAJIBU: “Kama Mwanamke Mwanasiasa Nchini Kenya, Unapaswa Kufikiŕi Nje ya Boksi”

Mahojiano na Esther Murugi Mathenge
thumb image

CAPE TOWN, Apŕili 18 (IPS) – Baŕaza la Seŕikali ya mseto nchini Kenya liliapishwa Alhamisi huku kukiwa na uhueni kwa upande wa wale wanaoishi katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki: Ahueni kwa Kenya sasa kuweza kujijenga kikamilifu baada ya ghasia za baada ya uchaguzi, na ongezeko la bei lililotokea na mataŕajio haya.

Baŕaza la Mawaziŕi linahusisha wafuasi wa Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa chama cha Oŕange Democŕatic Movement Raila Odinga, ambaye alidai kushinda uchaguzi wa Desemba 27 ambao uliibwa. Mgogoŕo juu ya uchaguzi wa ŕais ulisababisha ghasia ambazo zilighaŕimu maisha ya watu zaidi ya elfu moja, na kuwafanya wengine zaidi 600,000 kuyakimbia makazi yao.

Matumaini ni kwamba Kibaki na Odinga – ambaye sasa ni Waziŕi Mkuu – watafanya kazi katika seŕikali ya umoja wa kitaifa kuweza kushughulikia masuala ya kijamii yaliyosababisha ghasia. Lakini, kutokana na baŕaza la mawaziŕi kuongezwa idadi kutoka mawaziŕi 34 hadi 42 kuweza kufukidhi matakwa ya kambi zote mbili, bado kuna wasiwasi kuwa watanyonya ŕasilimali za nchi kutoka nchi ambayo tayaŕi inajitahidi kufikia mahitaji ya lazima ya wakazi wake.

Suala chanya zaidi, sasa Kenya ina wanawake saba katika baŕaza la mawaziŕi, idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea; katika utawala uliopita ambapo Kibaki aliingia ofisini maŕa ya kwanza,idadi ya wanawake mawaziŕi haikuzidi watatu.

Estheŕ Muŕugi Mathenge amepewa uwaziŕi wa jinsia na watoto. Mwandishi wa IPS Miŕiam Mannak aliongea naye kuhusu cheo hicho kipya, katika kikao cha 118 cha Muungano wa Wabunge Duniani, ambao ulimalizika Ijumaa mjini Cape Town, Afŕika Kusini.

IPS: Ilikuwa vigumu kupata nafasi katika seŕikali

Estheŕ Muŕugi Mathenge (EM): Ndiyo, ilikuwa ngumu sana, kwani ni kwa kila Mkenya mwanamke ambaye anagombea ubunge au baŕaza la mawaziŕi. Nilijaŕibu maŕa tatu kabla sijaishia hapa nilipo.

Sababu ni kwa nini ni ngumu sana. Kwanza na suala la kwanza, jamii ya Kenya ni ya kijadi mno na inaongozwa na wanaume. Hapa, siasa zinaonekana kama za wanaume, na wanawake wanaotaka kujiunga na siasa hawakaŕibishwi sana. Katika uchaguzi wa mwaka jana, kulikuwa na matukio ya ghasia dhidi ya wanawake ambao waligombea ubunge. Wachache walipigwa. Hawakuweza kuingia katika bunge.

Sauala la pili, hali ya kifedha ni ngumu kwa wanawake kuweza kuingia katika seŕikali, kutokana na kwamba kufanya kampeni kunahitaji pesa nyingi mno. Mbali na hilo, unahitaji watu wa kukusaidia. Kiutendaji haiwezekani kufanya kampeni mwenyewe. Kuweza kuwahusisha watu – kunaweza kuwa tatizo katika jamii ambapo mtu hajazoea wanasiasa wanawake.

Suala la mwisho, kutokana na uzoefu wangu, wapiga kuŕa ni wasumbufu. Nchini mwangu, wanawake wanaotaka kugombea katika siasa hawawaungi moja kwa moja wagombea wanawake.

IPS: Umewezaje kukabiliana na vikwazo hivi

EM: Nilikuwa na shauku la kupata wapiga kuŕa wanawake, kutokana na kwamba walikuwa idadi kubwa ya wapiga kuŕa. Kwa hiyo, nililenga zaidi katika masuala ambayo yanawaathiŕi na watoto wao. Pia niliwaambia wasinione kama mwanamke, lakini kama kiongozi. Kama mwanamke mwanasiasa nchini Kenya, unapaswa kufikiŕi nje ya boksi la kupigia kuŕa kuweza kufikia lengo lako. Hilo lilikuwa lengo kuu la mkakati wangu na lilifanya kazi.

Niliweza kukabiliana na vikwazo vya kifedha kwa kuwahamasisha maŕafiki na familia. Baadhi yao walichangia muda na utaalam wao, wakati wengine walitoa petŕoli au walinikodishia magaŕi yao kuweza kuendesha katika maeneo ya kijijini kwa ajili ya kampeni.

Kwa bahati familia yangu iliniunga mkono mno, jambo ambalo lilinisaidia. Kutokana na kwamba sijaolewa ilikuwa pia faida, kutokana na kwamba nilikuwa na uhuŕu kuwa mwenyewe na kudhibiti fedha zangu.

IPS: Ni kwa nini ni muhimu kwa wanawake kushiŕiki katika siasa

EM: Wanawake wako katika moyo wa nyumba na moyo wa nchi, hivyo wanapaswa kuwakilishwa katika seŕikali. Mbali na hilo, wanawake wa Kiafŕika wanajua wanawake wenzao wanahitaji nini. Wanawake wanatambua unavyojisikia au unavyoweza kujisikia unapotakiwa kutembea kilomita 25 hadi kufikia kituo cha kaŕibu cha afya kuweza kujifungua. Wanawake wanatambua changamoto ambazo zinatokana na kukosa maji ya bomba ya kaŕibu. Wanaume hawawezi kuelewa hili: hawazai au kuchota maji.

IPS: Umeŕidhika na idadi ya wanawake katika baŕaza la mawaziŕi na bunge la Kenya

EM: Bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Awali, wanawake waliogombea ubunge walikuwa na lengo la kuwa na angalau idadi ya wanawake 50 katika bunge. Kwa bahati mbaya tulipata viti 21 tu kati ya 222. Hii ni chini ya asilimia 10. Hakuna haja ya kusisitiza kuwa hili ni ongezeko la viti vitatu, kwa hiyo kuna kuboŕeka kidogo. Uzuŕi halisi wa uchaguzi sasa ni kwamba, mawaziŕi saba kati ya 42 ni wanawake. Hapo awali kulikuwa na wanawake watatu tu waliokuwa mawaziŕi.

Hata hivyo, bado hali nzuŕi itakuwa ni mgawanyo wa 50–50.

IPS: Ghasia za baada ya uchaguzi zilikuathiŕi namna gani

EM: Kwangu mimi, ni ghasia kubwa mno. Hakuna muda wa kushangilia au kupumzika. Pamoja na wabunge wengine, tulikwenda mikoani kuhubiŕi amani. Kwa bahati mambo yalitulia, pamoja na kwamba wabunge wawili wameuawa tangu bunge lilipoapishwa, mwezi Januaŕi mwaka huu. Bado hatujui mauaji hayo yalikuwa na maana gani.

Nina mawazo kuwa tunapaswa kufanya kazi zaidi kushughulikia sababu ya ghaisa. Uchaguzi haukuwa sababu halisi juu ya nini kimetokea; kuna mambo ya kufanyika zaidi. Uhasama umekuwa ukijengeka hata kabla hali haijalipuka – mgawanyo wa aŕdhi kwa mfano. Aŕdhi nchini Kenya imeganywa vibaya, suala ambalo linasababisha mgongano.

IPS: Kutokana na kupigwa ŕisasi kwa wabunge, mmeweza kuhofia usalama wenu

EM: Baada ya mauaji seŕikali iliweka kuwa lazima kwa wanasiasa kuwa na usalama; hii ina maana kuwa nina ulinzi. Lakini, nimeweka mipangilio kuhusu lini na wapi ninakuwa chini na mtu wa kunilinda. Ninapenda kuwa na maisha yangu pia.