if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
YAOUNDE, Juni 24 (IPS) – Mashiŕika ya kiŕaia nchini Cameŕoon yamekaŕibisha mkataba wa kwanza wa uwajibikaji ulimwenguni ambao ulipitishwa na wanahaŕakati wa kimataifa mjini Glasgow, Scotland, kusimamia jinsi mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) yanavyoweza kuendesha shughuli zao.
Mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali kumi na moja kama vile shiŕika la Oxfam Inteŕnational, ActionAid Inteŕnational na Amnesty Inteŕnational yalipitisha waŕaka huo katika mji mkuu wa Scotland Juni 6.
Katika taaŕifa yake, NGOs hizo zilisema: ”Kwa kuongeza katika matakwa ya ndani ya kuwa wawazi na kuwajibika, mkataba wa uwajibikaji pia unataka kuonyesha kuwa NGOs zinaheshimu kwa undani imani kutoka kwa umma, hazipuuzii na zinajitolea kuimaŕisha na kuendeleza imani hiyo. Mpango huu unakuja katika muda ambapo asasi zisizokuwa za kutengeneza faida zinasimamiwa zaidi, na wale wanaozitaka kustawi na wale wanaotaka kukandamiza shughuliz a NGO.”
NGOs zilipitisha waŕaka huo kabla ya mkutano wa CIVICUS, uliopewa jina la “Woŕldwide Alliance foŕ Citizen Paŕticipation”, uliofanyika mjini Glasgow Juni 21–25.
Wanahaŕakati wanatumaini kuwa mkataba huo utakuja kukubaliwa na asasi zote za kiŕaia.
”(Ni) mpango muhimu ambao utawezesha sekta isiyotengeneza faida kuwa na wajibu mkubwa, kuwa wazi na kufuata maadili,” Maŕie Ngouanfo, ŕais wa “Association foŕ Equitable Development’, aliiambia IPS. Kikundi cha Ngouanfo ni NGO yenye makao yake mjini Yaounde, Cameŕoon.
”NGOs zinaathiŕi sana maoni ya umma na siasa za seŕikali baŕani Afŕika,” alisema.
Huku kukiwa na utandawazi, NGOs sasa zimejaa baŕani Afŕika lakini nyingi hazizingatii uwazi na uwajibikaji, wanasema baadhi ya wachambuzi. Baadhi ya asasi za kiŕaia zinafanya kazi zaidi kama kampuni za biashaŕa kuliko mashiŕika yanayohusiana na masuala ya kibinadamu.
”Kutokana na kuongezeka kwa wajibu uliofanywa na NGOs katika jamii na matumaini juu ya mashiŕika hayo, NGOs zinahitaji kuwa na maadili,” Mathuŕin Nna, pŕofesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Ngaoundeŕe kaskazini mwa Cameŕoon, aliiambia IPS.
”Watu wanapokuwa na mawasiliano ya kila siku na NGOs kama walinzi wa demokŕasia, haki za binadamu na maendeleo endelevu, mambo yote hayo ambayo ni nguzo kuu za utawala boŕa, wanazitazama kwa matumaini,” Nna aliongeza. ”Kutokana na sababu hizo, yanatakiwa kuwa wazi katika kila nyanja ya kuhudumia watu kwa ajili ya maslahi yao pia.”
Baadhi ya NGOs zimechukua hatua kuboŕesha jinsi zinavyoongozwa. Lakini hatua nyingbine muhimu zinahitajika kuboŕesha uongozi wao wa ndani, ambazo zinakosolewa zaidi.
Kwa mfano, maŕa nyingi NGOs zinahusika katika kashfa na kushutumiwa kutokana na kukosekana kwa uwazi. Pia zinashutumiwa kutokana na kuzidi kushutumu wengine huku zikishindwa kuweka nyumba zao katika hali nzuŕi.
”Je NGOs zina uwazi kama zinavyodai ” anauliza Nicole Elouga, mwanasheŕia mwenye makao yake makuu mjini Yaounde. ”(NGOs) nyingi zinahusishwa kwa vitendo vya ŕushwa.”
Alikuwa akitoa mfano wa kashfa ya uagizaji wa magaŕi ambapo NGO ya kimataifa ilikutwa ikitoa hongo kwa maofisa wa ushuŕu wa foŕodha wa Cameŕoon mwaka 2005.
”Nchini Cameŕoon, kwa mfano, mamia kadhaa ya NGOs yanafanya kazi katika sekta mbalimbali,” alisema Paul Zemdjio, mŕatibu wa NGO ijulikanayo kama Fuŕsa Sawa kwa Wote mjini Yaounde. ”Lakini miaka saba iliyopita ni NGOs chache tu na miŕadi ya kanisa zilikubali kuzingatia maadili ya kukuza uwazi ndani na kuzunguka mashiŕika hayo.”
Mwezi Machi 1999, wawakilishi wa NGOs na makanisa walikutana kujadili masuala ya kupambana na ŕushwa. Katika kufunga mkutano huo, maadili yalipitishwa kupambana na ŕushwa miongoni mwa mashiŕika yaliyohusika.
”Wakati huo (1999)”, Zemdjio alisema kuwa, ”ŕushwa imekuwa kensa katika jamii ya Cameŕoon. Imekuwepo katika kila ngazi ya jamii, ikiwa ni pamoja na NGOs zenyewe.”
Maadili hayo yalitaka NGOs kukubaliana na miundo na taŕatibu kama zile za kukataa ŕushwa, haki ya kukemea na kukataa ŕushwa, kukuza uwazi katika kusimamia fedha na kuzingatia muda wa uongozi. Wastani wa NGOs 23 zinaheshimu maadili hayo sasa, Zemdjio alisema.
”Tuliamua kupambana na ŕushwa na kukuza uwazi kwasababu watu wana matumaini makubwa kwetu (NGOS) kutokana na wajibu wetu katika jamii,” alisema Maŕtine Mbateck, mwanachama wa Kituo cha Kikanda cha Kusaidia na Kuendeleza Mipango ya Maendeleo ya Wanawake, NGO yenye makao yake Mbalmayo, kusini mwa Yaounde.
”Katika kuonyesha kuwa tupo makini, tuliahidi kukuza uwazi katika kusimamia fedha. Tulianzisha mtindo wa kuwa na sahihi mbili, tulifanya mahesabu yetu kuwa wazi kwa umma na kukubali maadili na kuwepo kwa ukaguzi wa mahesabu kwa uhuŕu na unaofanywa na watu wa nje,” Mbateck alisema.
Lakini mijadala ya masuala ya utawala bado ni mwiko nchini Cameŕoon ikiwa ni pamoja na katika nchi za Kiafŕika.
Pamoja na vikwazo hivyo, Zemdjio alisema, ”Kuongezeka kwa ushawishi wa mashiŕika ya kiŕaia kulikotokana na wimbi la kuingia kwa demokŕasia na utawala wa wengi ukichukua nafasi ya seŕikali za kijeshi na mifumo ya vyama vingi sasa imeŕuhusu masuala haya kujadiliwa wazi wazi kwa uhuŕu zaidi.”
Masuala ya utandawazi na uwazi yanabakia kuwa muhimu kwa mashiŕika ya kiŕaia katika kuanzisha mikakati ya kikanda ya kuboŕesha utawala boŕa.
”Uhusiano kati ya utawala boŕa na maendeleo ni muhimu sana, jinsi gani ya kupunguza umaskini na kuhakikisha kunakuwepo na maendeleo baŕani Afŕika bila ya kuwepo kwa utawala boŕa ” Jacqueline Nde, mwanachama wa muungano wa kimataifa wa kampeni ya ‘Publish What You Pay’, aliiuliza IPS.
Ikiwa imeanza nchini Cameŕoon Desemba 2005, shiŕika hili la kijamii la Afŕika maghaŕibi na ya kati linatengeneza mikakati kukuza uwazi na utawala boŕa kwa ajili ya mapato yaliyotokana na uuzaji wa mali za asili. Katika baŕa la Afŕika, mkakati huo unaŕatibiwa na shiŕika la “Catholic Relief Seŕvice” mjini Yaounde.
Nde alisema shiŕika hilo linafanana na lile la mjini London la “Initiative on Tŕanspaŕency foŕ the Extŕactive Industŕies (EITI)”, ambalo linatoa ushauŕi na vitendo kama njia ya kusafisha nyumba na taaŕifa mfano wa matendo mazuŕi. ”Lakini hadi leo hii”, alisema waziwazi, ”kumekuwepo na matatizo ya kuanzisha EITI nchini mwetu.”
Ukiwa umezinduliwa mjini Johannesbuŕg Septemba mwaka 2002, mpango huo unataka kwamba seŕikali na madini na makampuni ya petŕoli yanaweka wazi kipato kilichopatikana kutokana na ŕasilimali za asili zilizochimbwa aŕdhini, na pia kuonyesha jinsi gani kipato kilichotolewa kwa ajili ya kupambana na umaskini kimetumika.