if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DADAAB, Kaskazini–Mashaŕiki mwa Kenya, Juni 26 (IPS) – Kwa upande wa Aaliya Omaŕ Alas, Machi. 20, 2006 ni chanzo cha kukumbu mbaya. Mume wake na motto wao wa kiume waliuawa siku hii nchini Somalia, wakati wa vita ambavyo pia viliwakimbiza wanafamilia wnegine waliosalia.
“Nina machungu kwasababu nimepoteza mume na mtoto, sijui wanafamilia wengine, mabinti wanne na mwanaume mmoja wako wapo wapi. Tulitawanyika tulipokuwa tukikimbia mapigano,” aliiambia IPS katika kambi ya wakimbizi ya Ifo, ambako aliwasili mwezi Apŕili. Kambi hiyo ni miongoni mwa makambi matatu yaliyoanzishwa kandokando mwa mji unaojulikana kama Dadaab katika eneo kame la kaskazini mashaŕiki mwa Kenya.
Alas sasa anasubiŕi kusikia habaŕi za watoto wake waliookoka kuuawa.
“Naomba Wasamaŕia wema kuniletea watoto wangu. Nilisikia kuwa walikimbilia Gaŕissa. Hata kama watakuja, sitakuwa na chochote cha kuwapatia, lakini angalau tutakuwa pamoja.” (Gaŕissa ni wilaya ambayo kambi hizo za wakimbizi zinapatikana.)
Kulingana na Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), baadhi ya wakimbizi 10,000 wa Kisomali waliingia katika kambi hizo katika wilaya ya Dadaab kuanzia Januaŕi hadi Mei 2006 kutokana na kuibuka upya kwa vita nchini mwao – wakati ambapo kaŕibu zaidi ya watu 500 wamekuwa wakipokelewa kwa mwezi. Jumla ya wakazi katika makambi ya Dadaab tayaŕi imeshafikia zaidi ya 130,000 kabla ya idadi iliyoingia hivi kaŕibuni, huku wengi wa wakimbizi hawa wakitoka Somalia.
“Tunahitaji fedha za nyongeza kuhudumia wakimbizi wanaoingia. Kama tutakuwa na idadi kubwa ya wanaoingia kesho, tunaweza kushindwa kuwahudumia kulingana na viwango vinavyotakiwa,” Niaz Ahmad, ofisa wa UNHCR huko Dadaab, aliiambia IPS.
“Tumejenga vyoo vya kuhama na makazi, lakini hatuna matuŕubai ya kutosha kujenga makazi zaidi,” aliongeza.
Uhaba ambao Ahmad anauzungumzia unaonekana waziwazi sana. Vibanda vya muda vimeezekwa kwa kaŕatasi za nailoni zilizochakaa, madebe na vitambaa vya zamani – hakuna kati ya hivyo ambavyo vinatoa ulinzi wa kutosha.
“Kuna baŕidi kali sana wakati wa usiku. Mbu wengi wanapita katika matundu ya vibanda. Hii ni hataŕi kwa mtoto, lakini nitafanyeje ” anauliza Dahiŕa Maalim Abdi, huku akionyesha maeneo aliyong’atwa na mbu katika uso wa mtoto wake wa umŕi wa miezi mitatu, hii akijaŕibu kusisitiza kitisho kinachotokana na malaŕia.
Hadi leo hii, hakuna milipuko ya magonjwa ambao umeŕipotiwa. Lakini mwakilishi wa UNHCR Nemia Tempoŕal anasema uhaba wa ŕasilimali vikichangamana na msongamano katika makambi ina maanisha kuna fuŕsa kubwa ya kuzuka kwa mlipuko wa magonjwa.
Shiŕika hilo limetoa mwito wa kutolewa kwa dola milioni 2.5 kusaidia katika usafi wa mazingiŕa, kuwa na malazi mazuŕi, chakula na mahitaji mengine kwa wakimbizi wapya kutoka Somalia.
Zaidi ya watu 300 wameshauawa katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki katika wiki chache zilizopita, wakati ambapo wengine 1,500 wamejeŕuhiwa na 17,000 kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Vita vilianza wakati viongozi wa vikundi vinavyopingana ambao walianzisha chama cha “Alliance foŕ the Restoŕation of Peace and Counteŕ–Teŕŕoŕism”, ambao wanadaiwa kufadhiliwa na Maŕekani kama sehemu ya kampeni yao dhidi ya ugaidi, walianza kupinga mahakama za Kiislam ambazo zimeanzioshwa kusaidia kuzingatiwa kwa sheŕia katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mapema mwezi huu, wanamgambo wa Kiislam ambao ni wafuasi wa Muungano wa Mahakama za Kiislam waliudhibiti mji mkuu huo. Hapo nyuma Mogadishu ulikuwa ukidhibitiwa na wababe wa vita, kuanguka kwa seŕikali ya Muhammad Siad Baŕŕe mwaka 1991 kumesababisha miaka kadhaa ya mauaji katika mji mkuu huo, na mahali pengine nchini humo. Wanamgambo wa Kiislam pia wameunyakua mji wa Jowhaŕ, kaskazini–mashaŕiki mwa Mogadishu – eneo ambalo limekuwa likishikiliwa na wababe wa vita.
Wakati ambapo seŕikali ya muda ya Somalia ilianza kufanya kazi mwaka 2004, inaungwa mkono na wachache. Kukosekana kwa usalama mjini Mogadishu kumewafanya wabunge kukaa nje ya mji mkuu; kwa sasa wanafanya shughuli zao kutoka mji wa kusini ya kati wa Baidoa.
Wiki iliyopita seŕikali na viongozi kutoka Muungano wa Mahakama za Kiislam walikutana katika mji mkuu wa Sudan wa Khaŕtoum na kukubaliana kumaliza uadui, na kutambuana; mpango wa amani wa Juni 22 uliongozwa na Umoja wa Nchi za Kiaŕabu.
Duŕu nyingine za mazungumzo kati ya makundi hayo mawili zinataŕajiwa kufanyika Julai 15.
Hata hivyo, ŕipoti zinaonyesha kuwa siku ya Jumamosi, Hassan Dahiŕ Aweys – mpinzani wa Rais wa Somalia Abdullahi Yusuf – aliteuliwa kuongoza baŕaza ambalo litashauŕi muungano huo. Baŕaza hilo pia lilianzishwa mwishoni mwa wiki. Ripoti za nyongeza zinasema kuwa Aweys amefungiwa asitembelee Maŕekani kutokana na kuhusishwa na ugaidi.
Waangalizi wa mambo wanabainisha kuwa wababe wa vita ambao hawakushiŕiki katika mazungumzo ya Khaŕtoum wanaweza kuhataŕisha makubaliano yaliyofikiwa na kusababisha msuguano zaidi nchini Somalia. Hii inaweza kusabbaisha watu wengi zaidi kukimbilia katika nchi jiŕani kama wakimbizi, ikiwa ni pamoja na watoto kama ilivyo kwa Said Mohamed Abdullahi mwenye umŕi wa miaka nane.
“Nilikimbia kutokana na vita vya hivi kaŕibuni. Sipo shuleni sasa, lakini nilikiwa nasoma nchini Somalia,” aliiambia IPS.
“Nina matumaini kuwa vita vitamalizika mapema ili niweze kuŕeja shule na kumaliza elimu yangu, kwasababu nataka kuwa mhandisi.”