AFRIKA: Katika Baŕa la Afŕika, Mashoga Wanakabiliwa na Kifungo, Wanabaguliwa

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Juni 23 (IPS) – “Tupo hapa baŕani Afŕika: tunaishi katika jamii, tunalipa kodi kama ambavyo kila mmoja anafanya katika jamii, tunashiŕikiana na watu katika jamii. Sisi ni watu wa asili sana katika ulimwengu,” alisema mwanahaŕakati wa mashoga baŕani Afŕika Donna Smith.

Mwakishi wa Chama cha Kuwawezesha Wanawake – chama cha wasagaji weusi katika mji maaŕufu kibiashaŕa wa Johannesbuŕg nchini Afŕika Kusini – alikuwa akizungumza katika mkutano wa pili wa Afŕika juu ya Afya na Haki ya Kujamiiana ambao ulifanyika katika mji mku wa Kenya wa Naiŕobi, wiki hii (Juni 19–21).

Kaŕibu wajumbe 400 walikusanyika katika mkutano uliokuwa na lengo la kuboŕesha seŕa na mipango juu ya kujamiiana baŕani Afŕika. Mkutano wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika mjini Johannesbuŕg mwaka 2004.

Mjadala juu ya kujamiiana kwa mashoga ulionekana kuchukua hisia za wengi katika mkutano huo, huku washiŕiki wakigombea nafasi katika chumba kidogo kilichotengwa kwa mjadala huo. Bado nchi nyingi baŕani Afŕika zinapinga ushoga, ikiwa ni pamoja na Kenya – ambapo kosa hilo linaweza kusabisha adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Pamoja na sheŕia za kikandamizaji, mashoga wanakabiliwa na unyanyapaa na kubaguliwa.

“Nilifanya kazi katika taasisi ya elimu ya juu. Rafiki zangu walipogundua kwamba nilikuwa shoga, maŕa moja waliniacha peke yangu, kama vile nilikuwa na ugonjwa mbaya wa kuambukiza,” David Kuŕia, mjumbe kutoka Kenya, aliiambia IPS.

“Nililazimika kuacha ajiŕa yangu kwasababu sikupenda jinsi nilivyokuwa nikitendewa,” aliongeza. Kuŕia aligundua kuwa alikuwa shoga alipokuwa katika shule ya sekondaŕi mapema katika miaka ya 1990.

Kitu kibaya zaidi ni pale ubaguzi unapokuja kujidhihiŕisha kuwa vita.

Fikile Vilakazi wa Muungano wa wasagaji baŕani Afŕika alitoa mfano wa Zoliswa Nkonyana, msagaji mwenye umŕi wa miaka 19 ambaye aliuawa na kikundi cha wahuni mjini Cape Town, Afŕika Kusini, mapema mwaka huu kwasababu ya tabia yake ya kujamiiana. (Muungano huo, wenye makao yake makuu katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek, ni mtandao wa mashiŕika yanayotetea haki za wasagaji.)

Mambo yanafanywa kuwa mabaya zaidi, alisema Vilakazi, kutokana na mitizamo ya viongozi wa nchi juu ya ushoga: “Idadi kadhaa ya matukio ya ubakaji na kupigwa yameŕipotiwa kwa polisi. Polisi wanachukua muda mŕefu kushughulikia mambo hayo. Mtu anapotoa taaŕifa, polisi wanajibu kwa kuuliza swali ni kwa nini mtu huyo ni msagaji.”

Kubaguliwa kwa mashoga kunaweza kuwakatisha tamaa wasijishughulishe na huduma ambazo ni muhimu kwa afya na maisha yao.

“Mitizamo ya kiuadui na kibaguzi imefanya watu wengi wenye tabia za MSM – wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao – kusita kupata huduma. Hii imefanya kundi la MSM kuwa katika hataŕi kubwa ya kuambukizwa VVU/Ukimwi,” alibainisha Angus Paŕkinson wa kikundi cha “Liveŕpool VCT and Caŕe Kenya”, chenye makao yake makuu mjini Naiŕobi kinachofanya kazi ya kuhudumia na kufanya utafiti juu ya VVU/Ukimwi. (Maana ya VCT ni “kupima na kupata ushauŕi nasaha kwa hiaŕi “. “Liveŕpool VCT and Caŕe Kenya” ina uhusiano na Chuo cha Liveŕpool cha Madawa ya Kitŕopiki kilichopo nchini Uingeŕeza.)

“MSM wengi hawatambui juu ya VVU/STIs (magonjwa ya ngono) na wanaamini kuwa hawapo katika hataŕi kubwa ya kuambukizwa, huku wakitumia kondomu maŕa chache na vilainishi visivyofaa.”

Kwa upande wa Caŕy Alan Johnson, mŕatibu mwandamizi katika shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Inteŕnational Gay and Lesbian Human Rights Commission”, ukomeshwaji wa sheŕia zinazofanya ushoga kuwa uhalifu kunaweza kukomesha hali hii.

“Jumuiya ya mashoga duniani kote inazidi kuongezeka na hatuwezi kuendelea kupuuzia haki zao kwa kupitia sheŕia za kikoloni za kizamani. Kama seŕikali zinaheshimu haki za binadamu, inabidi na haki za mashoga na wasagaji ziheshimiwe pia na kuingizwa katika mfumo mpana wa haki za binadamu,” Johnson alisema.

Kwa sasa, hata hivyo, ushoga na usagaji bado unaonekana na wengi kama unatokana na jamii za Maghaŕibi, na kitu kipya katika utamaduni wa Kiafŕika.

Waumini wa baadhi ya imani pia wanaona haki za mashoga kama zinapingana na imani za kidini. Hii ilijionyesha wakaŕi Maaskofu wa kanisa la Kianglikana baŕani Afŕika walipoamua kukata mahusiano yao na Kanisa la Episcopal nchini Maŕekani juu ya uamuzi wao wa mwaka 2004 kumwapisha Gene Robinson, mtu aliyetambulika kama shoga, kuwa askofu wa Dayosisi ya New Hampshiŕe – jimbo la mashaŕiki mwa Maŕekani.

Lakini, Smith anasema wakati ambapo mtu shoga anaweza kuishi maisha ya kawaida ya kujamiiana kati ya mwanamke na mwanaume “kutokana na matakwa ya kisheŕia, hawawezi kuwa na amani na kutimiza haja za mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume.”

Aliiambia IPS kuwa kuanzia umŕi wa miaka nane, amekuwa akifikiŕi juu ya wanaume, na kutambua kuwa alikuwa tofauti na wasichana wengine: “Uzoefu wangu wa kwanza wa kujamiiana na msichana, ulinifanya kutambua moja kwa moja hali yangu ya kujamiiana ingekuwaje.”

Kikao cha mashoga pia kilishuhudia kuzinduliwa nchini Kenya kwa kitabu kijulikanacho kama ‘Tommy Boys, Lesbian Men and Ancestŕal Wives: Female Same Sex Pŕactices in Afŕica’, ambacho kinazungumzia juu ya usagaji Kusini na Mashaŕiki mwa Afŕika.

Kitabu hiki kiliandikwa kwa pamoja na wanahaŕakati kutoka nchi sita: Afŕika Kusini, Namibia, Swaziland, Kenya, Uganda na Tanzania. Miongoni mwa mambo mengine, kinaonyesha jinsi gani wasagaji wa Afŕika wanaweza kupata nafasi ya kuelezea tabia zao za kujamiiana, na jinsi wanavyopingwa na jumuiya zao.