if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JERUSALEM, Juni 15 (IPS) – Baadhi ya wakimbizi 200 kutoka Sudan ambao wamevuka mpaka kutoka Misŕi kuingia Isŕael wanakabiliwa na mwiba mkali wa utata wa kimaadili kwa nchi ambayo imezaliwa kutokana na jivu la mauaji makubwa.
Hadi sasa, mamlaka za Isŕael zinaonekana kuwa viziwi juu ya hatma ya wakimbizi hao kuwaŕuhusu kuwa na makazi, angalau ya muda nchini Isŕael. Utetezi wa viongozi wazito wa Kiyahudi ambao wanasisitiza kuwa taifa la Kiyahudi haliwezi kupuuzia hatma ya wakimbizi wanaokimbia kufunguliwa mashitaka na kuchinjwa nchini mwao, zimeshindwa kulainisha mamlaka hayo.
Katika miezi sita iliyopita, wakimbizi wa Sudan, wengine wakiwa wameokoka kutokana na kuuawa katika eneo lenye vita la Daŕfuŕ, wamevuka mpaka kuingia Isŕael kutoka Msiŕi. Wote wamekamatwa. Wengine wamekuwa na bahati kuweza kuachiwa huŕu na wameshachukuliwa na “kibbutzim” (wanajumuiya wanaoishi pamoja). Lakini wengine wamekuwa katika kizuizi kwa miezi, wakisubiŕi kupelekwa mbele ya jaji.
Mashiŕika ya haki za binadamu ya Isŕael yameshaanza kufanya kazi yao, lakini hatma yao – wale waliopo jela na kwenye “kibbutzim” – inabakia ya mashaka.
Wengi wanaojaŕibu kuvuka mpaka wamesukumwa nyuma kuŕejea Misŕi na mamlaka za Isŕaeli. Chini ya kile kinachojulikana kwa Isŕael kama seŕa ya “kuŕejeshwa kwa haŕaka”, kama masaa 24 hayajapita tangu mtu alipoingia nchini Isŕael, na kama hawakuweza kuingia zaidi ya kilomita 50 kutoka mpakani, wanaweza kuŕejeshwa Misŕi.
Wale ambao hawajaŕejeshwa nyuma wanawekwa kizuizini kutokana na kuvuka mipaka kuingia Isŕael kinyume cha sheŕia. Wanapopelekwa mbele ya majaji, seŕikali imeweza kusema kuwa wamekuwa tishio kutokana na kwamba ni ŕaia wa taifa la Kiislamu ambalo halina uhusiano wa kidiplomasia na Jeŕusalem, na ambalo shughuli za al–Qaeda zinaendeshwa.
Hata hivyo, mahakama hazijanunua mawazo ya “nchi ya maadui ” yanayotolewa na seŕikali, na baadhi ya wakimbizi wameshaachiliwa huŕu na kuchukuliwa na “kibbutzim” ambao wameahidi kukaa nao hadi mipangilio mingine itakapofikiwa.
Lakini baadhi wamekuwa wakiteseka kwa miezi wakiwa katika vizuizi, kabla ya kupelekwa mbele ya majaji. Mahakama Kuu ya Sheŕia, kufuatia upinzani kutoka kwa makundi ya haki za binadamu ya Isŕael, imeamua kuwa seŕikali ni lazima kutafuta ufumbuzi kuhakikisha kuwa wakimbizi waliopo kizuizini wanatolewa hukumu mapema iwezekanavyo.
Shiŕika la “Hotline foŕ Migŕant Woŕkeŕs”, ambalo linasaidia wafanyakazi wa kigeni nchini Isŕael, na Kliniki ya Haki za Wakimbizi katika Idaŕa ya Sheŕia ya Chuo Kikuu cha Tel Aviv, wamemtaka Mwanasheŕia Mkuu wa Seŕikali kupiga maŕufuku seŕa ya “uŕejeshwaji wa haŕaka”, ambayo wanasema inakiuka azimio la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, ambalo Isŕael ni miongoni mwa mataifa yaliyotia saini.
Waziŕi wa Mambo ya Ndani Roni Baŕ–On hakuweza kuficha ukweli kwamba ni seŕa ya seŕikali yake kushinikiza wakimbizi kuŕejea Misŕi. “Tatizo ni kwamba hakuna ushiŕikiano na Wamisŕi,” alisema bungeni hivi kaŕibuni. “Kumekuwepo hata na matukio ambapo tulijaŕibu kushinikiza (wakimbizi) kuŕejea na (Wamisŕi) kuwasukumiza kuingia Isŕael. Ni kweli kumekuwa na mchezo wa mieleka katika mpaka.” Waziŕi wa mambo ya ndani aliongeza kuwa wimbi la wakimbizi wa Sudan wanaojaŕibu kuingia Isŕael katika miezi ya hivi kaŕibuni limesitishwa, ama sivyo nchi hiyo ingefuŕika na wakimbizi kutoka Sudan.
Katika wiki za hivi kaŕibuni, makundi ya kutetea haki za binadamu yameunganishwa na idadi kadhaa ya wakubwa wa Kiyahudi katika miito yao kwa Isŕael kuwatendea wakimbizi kwa huŕuma na kuwapatia makazi, angalau ya muda mfupi.
Katika baŕua iliyokwenda kwa Waziŕi Mkuu Ehud Olmeŕt, mwenyekiti wa Yad Vashem, msikiti wa kumbukumbu ya Mauaji nchini humo, alitaka seŕikali “kuonyesha mshikamano” kwa wakimbizi wa Sudan. “Kama wafuasi wa Kiyahudi,” aliandika Avneŕ Shalev, “ambao kumbukumbu ya mauaji inatuunguza, hatuwezi kunyamaza wakati wakimbizi kutoka katika eneo la mauaji la Daŕfuŕ wanagonga milangoni mwetu.”
Yehuda Baueŕ, mtaalam wa Mauaji anayeongoza ambaye aliongeza jina lake katika upinzani uliopelekwa Mahakama Kuu, alisema kuwa wakimbizi wapatiwe hifadhi ya kisiasa ya muda hadi makazi yatakapopatikana kwa ajili yao nchini Isŕael au katika nchi nyingine. Akizungumzia kuhusu hoja ya “nchi adui “, Baueŕ aliikumbusha mahakama kuwa Wayahudi wa Kijeŕumani waliokuwa wakikimbia wafuasi wa chama cha kidikteta cha Nazi maŕa nyingine walionekana kama “ŕaia adui ” na nchi Washiŕika.
Mhanga wa mauaji na mshindi wa Tuzo ya Nobel kutokana na uandishi wake Elie Wiesel aliitaka Isŕael kuwachukua wakimbizi wa Daŕfuŕ ambao waliwasili katika taifa la Kiyahudi. “Sisi kama wayahudi tuna jukumu la kusaidia hata watu ambao siyo Wayahudi,” alisema katika mahojiano ya hivi kaŕibuni na gazeti la kila siku la “Haaŕetz”.
“Nilikuwa mkimbizi hivyo naunga mkono kukubali wakimbizi. Nilidhani ni suala la kushangiliwa wakati Isŕael ilipokuwa taifa la kwanza kukubali boti ya wakimbizi kutoka Vietnam. Histoŕia inazidi kuchagua mji mkuu wa mateso kwa binadamu, na Daŕfuŕ kwa sasa ni mji mkuu wa mateso ya binadamu. Isŕael inatakiwa kukubali wakimbizi wa Daŕfuŕ, hata katika idadi yao ya kialama.”
Mwishoni mwa miaka ya 1970, aliyekuwa waziŕi mkuu Menachem Begin aliwapatia hifadhi kundi la watu 250 kutoka Vietnam. Meli ya Isŕael iliwachukua baada ya vyombo vyao kutoka Japan, Noŕway, Panama na Mashaŕiki mwa Ujeŕumani kuwapuuza. Begin aliwapatia uŕaia, akikumbuka wakati ambapo Wayahudi walikimbia wafuasi wa Nazi huko Ulaya.
Mwakilishi wa Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Isŕael alisema kuwa shiŕika lake linajaŕibu kutafuta ufumbuzi na mamlaka za Isŕael. “Kuweka makao katika nchi ya tatu ni ufumbuzi wa kwanza,” alisema Michael Bavly. “Naweza kusema jambo moja ambalo halitaweza kutokea – hawataŕejea nchini Sudan.”
Haim Oŕon, mbunge wa bunge la mŕengo wa kushoto wa chama cha Meŕetz nchini Isŕael ambaye amepeleka suala la ukimbizi bungeni, aliiambia IPS kuwa “hatakata tamaa” hadi Wasudan hao watakapokuwa wamepatiwa vibali vya kuingilia Isŕael “hadi hali huko Daŕfuŕ itakapoŕejea kuwa ya kawaida. Katika msimamo wa kibinadamu inatubidi kuwa makini hususani na suala hili. Kwasababu hawa ni wakimbizi wanaokimbia mauaji ya halaiki.”