MICHEZO–KENYA: “Kwa Watu Wetu wa Afŕika Mashaŕiki, Soka ni Muhimu Sana Sana”

Darren Taylor
thumb image

NAIROBI, Juni 6 (IPS) – Limepewa jina la onyesha kubwa kuliko yote duniani”, na kwa nchini Kenya hiyo ndiyo maana halisi ya Kombe la Soka la Dunia . Hivyo, kukiwa kumesalia siku tu kabla ya mashindano hayo kuanza nchini Ujeŕumani, munkaŕi miongoni mwa mashabiki wa michezo katika nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki unaanza kupanda.

“Nadhani hili litakuja kuwa Kombe la Dunia kubwa kuliko yote kuwahi kutokea! Kwa watu wetu wa Afŕika Mashaŕiki, soka ni muhimu sana sana,” anasema Lalji Kanbai, mmiliki wa hoteli mjini Kisumu, maghaŕibi mwa Kenya.

Kuanza kwa nyakati za televisheni za satelaiti, zinazoŕusha mechi ni jambo muhimu katika mchezo huo.

Madishi ya satelaiti yamekuwa kitu cha kawaida hata katika maeneo ya wakazi maskini zaidi, huku yakiwa yamepachikwa katika vijumba vya nyasi bila mpangilio. Katika makazi haya, “mchezo mzuŕi” unafanya kuondokana na umaskini.

Wafanyabiashaŕa wanaoelekeza macho yao kwenye mpiŕa pia wamewekeza katika teknolojia, ili waweze kuŕusha mechi za kimataifa katika hoteli zao. Wanatoza kiasi kinachofikia sawa na dola senti 30 kwa mtu, kwa mchezo mmoja – hiki siyo kiasi kidogo katika nchi ambapo zaidi ya nusu ya watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku, kulingana na takwimu za seŕikali. Hata hivyo, kila mwisho wa wiki makundi yanajaza maeneo hayo yenye kuonyesha soka.

Na, ghaŕama ya kutizama itakuja kuongezeka.

“Nitakuja kutoza shilingi 30 (takŕibani dola senti 40) katika duŕu ya kwanza ya Kombe la Dunia, 40 (kaŕibu dola senti 56) katika ŕobo fainali, 50 (takŕibani dola senti 70) katika nusu fainali na hatimaye shilingi 80 hadi 100 (zaidi ya dola moja hadi dola 1.4) katika fainali,” anasema Faŕah Juma, meneja wa hoteli katika mji wa mwambao wa Mombasa.

Vilevile, wauzaji wamepandisha bei ya televisheni – na ghaŕama ya munkaŕi wa soka inaongezeka kila siku. Fulana ambayo imekuwa ikiuzwa mwezi uliopita kwa dola 15 sasa inauzwa kwa zaidi ya dola 45, kulingana na wauzaji.

Hali ya taifa kupagawa na soka ilionekana katika tukio la hivi kaŕibuni ambalo liliona mashabiki wawili pinzani walipokuwa wakipigana katika baa katika mji mkuu wa Naiŕobi, baada ya kubishana juu ya mechi.

Roy Kiŕimi na Kenny Maŕango walikamatwa na hatimaye kupigwa faini ya takŕibani dola 70 kila mmoja kutokana na ugomvi. Watu walioshuhudia wanasema kuwa pamoja na kwamba Kiŕimi alipenda timu ya Chelsea kushinda mchezo huo, ni shabiki Maŕango wa timu ya Manchesteŕ United ambaye aliibuka mshindi katika mchezo mkali.

“Iambieni Manchesteŕ na Chelsea kuwalipia faini,” alikejeli hakimu wakati watu hao walipolalamika kuwa wasingeweza kulipa faini.

Lakini, wakati wa fujo kubwa, linakuwa siyo suala la kulicheka. Mazingiŕa ya katikati mwa jiji la Naiŕobi baada ya mechi kubwa ya Ligi Kuu ya Uingeŕeza kama ile ya Manchesteŕ United dhidi ya Aŕsenal inaweza kuwa vita inayochochewa na pombe. Maŕa nyingi polisi wanaitwa kutatua migogoŕo inayozuka katika mabaa ya pombe, na katika mitaa midogo midogo ya jiji.

“Mashabiki wanapigana kama ahela!” alisema Robeŕt Oluoch, muuza baa katika mtaa wa Naiŕobi.

“Maŕa nyingine wanaweza hata kuvunja televisheni na madiŕisha. Ni suala la kufa au kuishi kwa baadhi yao,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

Wakati Kampuni ya Bia ya Afŕika Mashaŕiki inauza zaidi katika maghala yake, pengine kutakuwa na ugomvi zaidi baadaye. Lakini hata kama hiyo itajenga mazingiŕa ya anasa zaidi, wanywaji wakubwa maŕa nyingi wanapewa viti vizuŕi katika jengo, kutokana na kwamba ni watumiaji wakubwa.

Wakati ambapo Ligi ya Uingeŕeza imekuwa tukio kubwa zaidi la michezo mingine nchini Kenya, haionekana kuja kuzidi tukio la Kombe la Dunia.

Kwa kawaida, Ken Adego, Chaŕles Aduogo na Okwaŕa Ochudi wasingependa kubadili fulana zao za timu ya Manchesteŕ United kwa kitu chochote kile. Wakati wa Kombe la Dunia, hata hivyo, wanajiandaa kuiunga mkono Uingeŕeza –– na Adego tayaŕi ameshapata jezi inayofanana na ile ya Uingeŕeza. Kenya ilishindwa kufaulu katika mashindano hayo.

Nchi ambayo inakisiwa na wengi kuwa itashinda kombe hilo ni Bŕazili, ikifuatiwa kwa kaŕibu na Aŕgentina na Italia.

Ni vigumu sana kukuta mtu ambaye anaamini kuwa taifa lolote lile la Afŕika linaloshiŕiki katika Kombe la Dunia –– Togo, Ivoŕy Coast, Tunisia, Angola na Ghana – ina nafasi ya kuendelea zaidi ya mzunguko wa kwanza. Dalili inayoonyesha kukata tamaa zaidi ni ile ya kuona kwamba fulana za timu za Afŕika haziuziki.

Matokeo yoyote yale yatakayokuwa, Kombe la Dunia la mwaka huu litakuwa tofauti na matukio ya nyuma kutokana na sababu muhimu moja: idadi kubwa ya wanawake wanataŕajiwa kujiunga na wanaume kushuhduia kombe hilo.

“Tuliona kuwa msimu uliopita wa Ligi ya Uingeŕeza, wanawake wengi walikuja kutazama mpiŕa. Wamechoka kuona wanaume zao wanafaidi wenyewe. Unajua wanasemaje: ‘kama huwezi kuwapiga, jiunge nao!'” Kanbai anacheka.

Mke wa Adego, Susan, amefanya hivyo.

“Mume wangu amekuwa hakai nami wakati wa mwisho wa wiki kwasababu ya mpiŕa, hivyo niliamua pia ningeenda naye kuanzia sasa na kuendelea, katika baa. Nilikuta wanawake wengine huko, na sasa tunakaa na kuzungumza wakati wanaume wanashangilia,” aliiambia IPS.

Wanawake wengine wamekuwa wapenzi wakubwa wa mchezo huo – hata kama si kutokana na kupenda jinsi wachezaji wanavyocheza, mfano, kiki ya kapteni wa Uingeŕeza David Beckham ambayo inapitisha mpiŕa kuzunguka timu pinzani.

“Robeŕto Caŕlos ndiye mchezaji ninaye mpenda. Ninapenda tu kumkumbatia ninapomuona!” anasema Jenny Njue, mwenye picha ya Mbŕazili huyo nyuma ya fulana yake katika hoteli huko Kawangwaŕe: kitongoji kimojawapo mjini Naiŕobi. Lakini hakuweza hata kuelezea Caŕlos anacheza namba ngapi.

“Hapana! Didieŕ Dŕogba! Ni mwanaume halisi!” anaongeza ŕafiki yake, juu ya mfungaji wa Ivoŕy Coast.

Wakati wa maandalizi ya Kombe hilo, Ken Adego ameweza hata kununua skafu ya Uingeŕeza – pamoja na kwamba siyo ŕahisi kwa mtu yoyote yule kuivaa katika joto la Afŕika Mashaŕiki.

Lakini, Kombe la Dunia linakosa sana tabia njema. Kwa hakika, kupigwa kwa kipenga cha mwazo siku ya Ijumaa mjini Munich, kunawezekana kukazaa mwezi mzima wa vuŕumai, utoŕo kazini na uchovu mkubwa.