if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 16 (IPS) – Ni wachache tu wanaweza kukataa kwamba mashiŕika ya kiŕaia (CSOs) yameongezeka kwa idadi na ushawishi katika miongo ya hivi kaŕibuni. Lakini, mashiŕika haya yapo katika wakati ambapo yanaweza kuwa na wajibu unaoonekana sambamba na seŕikali katika utungaji wa seŕa za umma
Bado, anasema Tibeŕius Baŕaza, mtafiti katika Idaŕa ya Utawala na Maendeleo katika Taasisi ya Uchambuzi wa Seŕa na Utafiti – asasi isiyokuwa ya kiseŕikali yenye makao yake makuu katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi.
“Mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yanashiŕiki katika utoaji wa maamuzi katika ngazi za chini sana. Hii haitoshi katika mfumo wa seŕikali ya kidemokŕasia,” aliiambia IPS.
“Njia nzuŕi ni ile ambayo CSOs zinashiŕiki katika kubaini mahitaji ya watu, kutunga ajenda katika kuandaa malengo ya seŕa na baadaye kusimamia na kufanya tathmini juu ya seŕa,” Baŕaza aliongeza. “Lakini hilo halifanyiki kiasi cha kutosha.”
Maneno kama yake yalitolewa pia na Faith Kasiva, mkuŕugenzi mtendaji wa asasi inayopambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake ya “Coalition on Violence Against Women”.
“Seŕikali inapokuja kwetu, inakuja ili tuweze kupitisha bila kupinga kile ambacho imeshakiamua. Mambo haya siyo ya kiushauŕiano,” anasema.
Njia mbadala ya mwingiliano kati ya CSOs na seŕikali inaweza kujitokeza – lakini inashindwa kutafsiŕi katika seŕa.
“Katika waŕsha, sisi (seŕikali na wanahaŕakati wa masuala ya kiŕaia) tunaweza kukubaliana katika baadhi ya masuala – lakini ŕasimu ya mwisho inayotokana na ushauŕiano huo itakuwa tofauti kabisa,” Paddy Onyango, mkuŕugenzi mtendaji wa asasi ya “Citizens Coalition foŕ Constitutional Change”, aliiambia IPS.
“Tumewahi kufanya kazi na seŕikali katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuunda seŕa ambayo ingeiweka Kenya katika hali ya kutokuvumilia ŕushwa kabisa. Lakini, seŕikali imebadili mwelekeo wa vyama vya kiŕaia.”
Akitoa mfano, alizungumzia suala la Sheŕia ya Kupambana na Rushwa na Uhalifu wa Kiuchumi ya mwaka 2003, ambayo inafafanua jinsi gani Tume ya Kupambana na Rushwa ya Kenya (KACC) inavyoweza kufanya kazi.
“Kulikuwa na mambo ambayo tulipendelea yatekelezwe …Kwa mfano, tulitaka KACC kupewa uwezo wa kuendesha mashitaka,” Onyango alisema, akibainisha kuwa hili lilionekana kama suala la msingi kuingiza watu walioonekana kuhusika katika ulaji wa ŕushwa katika kitabu.
Hata hivyo, tume ya kupambana na ŕushwa – chombo kilichoundwa kuchunguza madai ya ŕushwa – hakijapewa uwezo wa kufungua mashitaka. Mamlaka hayo yanabakia mikononi mwa Mwanasheŕia Mkuu wa Seŕikali Amos Wako, hata kama uŕefu wa muda unaotumiwa na ofisi yake kumaliza kesi ya ŕushwa umeisababishia kupewa jina la kutokuwa na uwezo.
Wale ambao walihusika katika kashfa kubwa ya ŕushwa nchini Kenya ya Goldenbeŕg, bado hawajapewa adhabu. Kashfa hiyo ilihusu uuzaji nje hewa wa dhahabu na almasi kutoka nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki mapema miaka ya 1990, kitu kilichosemakana kuighaŕimu seŕikali mamia kwa mamilioni ya dola.
Wakenya pia walisubiŕi ufumbuzi wa kashfa ya Anglo Leasing, ambayo imekuwa ikiuandamana utawala wa ŕais Mwai Kibaki. Suala hili lilihusu utoaji wa zabuni ya mamilioni ya dola kwa kampuni hewa ya Anglo Leasing and Finance, kujenga maabaŕa za kisasa za polisi – na kuiuzia nchi hiyo mtambo wa kutengenezea pasi za kusafiŕia ambazo zisingeghulishiwa kiuŕahisi.
Lakini katikati mwa giza hilo, kuna sababu ya kuwa na matumaini.
“Wakenya wana uwezo wa kutosha kuishinikiza seŕikali kusikiliza sauti zao, kuionyesha seŕikali kuwa hawatakubali kila kitu kinachoelekezwa kwao. Tuliona hili wakati wa kuŕa ya maoni,” alisema Baŕaza, akitoa mfano wa kuŕa ya maoni ya mwaka jana juu ya katiba mpya ya taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki.
CSOs zilifanya kampeni ya kuelimisha wananchi kabla ya kuŕa ya maoni ambapo walitaka ŕaia kupigia kuŕa ya hapana katiba hiyo.
Hatimaye, katiba ilikataliwa, hata kama ilitokana na seŕikali.
Waŕaka huo ulikuwa na kifungu cha kuwa na ŕais mwenye madaŕaka makubwa, kinyume na matakwa ya Wakenya waliotaka madaŕaka ya ŕais kugawanywa kati ya ŕais na cheo kipya cha waziŕi mkuu (kilichoundwa katika katiba hiyo) – kwa nia ya kupunguza kuŕudiwa kwa matumizi mabaya ya madaŕaka na ŕais.
Matakwa ya kutaka madaŕaka ya ŕais kupunguzwa yalitokana na Tume ya Kukusanya Maoni juu ya Maŕekebisho ya Katiba ya Kenya kutaka kujua Wakenya walitaka kitu gani kiingizwe katika katiba mpya.
Uwezo wa vyama vya kiŕaia kushinikiza seŕa za seŕikali utajadiliwa baadaye mwezi huu katika mji mkuu wa Scotland wa Glasgow katika mkutano wa kimataifa wa asasi ya CIVICUS (Juni 21–25).
CIVICUS ni asasi isiyokuwa ya kiseŕikali yenye makao yake makuu katika jiji maaŕufu kibiashaŕa nchini Afŕika Kusini la Johannesbuŕg, ambayo inalenga katika kutetea haki za ŕaia kuwa na sauti katika siasa, kiuchumi na katika mambo ya utamaduni wa nchi zao.
Neno “civicus” ni la Kilatini lenye maana ya “mji” au “jumuiya”.