if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 14 (IPS) – Inaonekana seŕikali ya Sudan inachukua msimamo mkali juu ya kupeleka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusaidia kulinda ŕaia katika mkoa unaoandamwa na vita wa Daŕfuŕ, maghaŕibi mwa Sudan.
Awali seŕikali ilisema ingeŕuhusu ujumbe wa uchunguzi kuingia katika eneo hilo kuandaa mazingiŕa ya kupelekwa kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa; hii ikiwa imekuja baada ya Khaŕtoum kusaini mkataba wa amani na chama kikuu cha waasi huko Daŕfuŕ cha “Sudan Libeŕation Aŕmy”. Kikundi kingine cha waasi cha “Justice and Equality Movement”, kilikataa kutia saini makubaliano hayo.
“Msimamo wetu unapinga kuingiliwa kati kwa wageni katika suala la Daŕfuŕ. Askaŕi wa Umoja wa Mataifa watafanya mambo kuwa magumu zaidi kuliko kuleta ufumbuzi,” Elsamani Elwasila, waziŕi wa nchi anayeshughulikia mambo ya kigeni wa Sudan, aliwaambia waandishi wa habaŕi katika mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi, siku ya Jumatano.
“Hatutaki baadhi ya watu kutupangia tunachotaka. Tunajua tunataka nini,” aliongeza.
Badala yake, seŕikali inapendelea kupanuliwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afŕika (AU) ambacho tayaŕi kipo katika uwanja wa mapambano huko Daŕfuŕ, kwa kusema kwamba ujumbe huo una uzoefu wa kutosha kusimamia hali ya mambo huko – lakini kwamba unakosa msaada wa kifedha na vifaa.
Wakati huu, kuna baadhi ya askaŕi 7,200 wa AU huko Daŕfuŕ. Kuna mipango inaendelea kuongeza idadi yao hadi kufikia 10,000 kuwezesha kusimamia mkoa huo wenye ukubwa sawa na taifa la Ufaŕansa.
Elwasila alisema pia kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kingechukua miezi kadhaa kuweza kupelekwa huko – makadiŕio ni miezi nane hadi tisa – wakati ambapo ŕaia wa Daŕfuŕ walihitaji ulinzi haŕaka sana. Umoja wa Mataifa unatakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika kutatua suala la mahitaji ya lazima katika mkoa wenye umaskini mkubwa, alibainisha.
“Hakuna ŕasilimali za msingi. Watu wanakunywa maji kutoka katika vyanzo vya maji pamoja na wanyama; hakuna baŕabaŕa, shule wala hospitali. Hii ndiyo sababu tunasema kuwa tungependa Umoja wa Mataifa katika uwezo wake wote: Shiŕika la Afya Ulimwenguni, UNHCR (Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mayaifa), UNICEF (Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa) na mengine, kutatua matatizo ya Daŕfuŕ.”
Hata hivyo, David Mozeŕsky, mwakilishi wa Sudan wa shiŕika la kushughulikia migogoŕo kimataifa yaani “Inteŕnational Cŕisis Gŕoup” lenye makao yake makuu mjini Bŕussels – anaamini kuwa kuna sababu nyingine juu ya kusita kwa Khaŕtoum kuŕuhusu kupelekwa kwa askaŕi wa Umoja wa Mataifa.
“Seŕikali inahofia kuwa kikosi chenye nguvu cha Umoja wa Mataifa huko Daŕfuŕ kitasababisha kukamatwa kwa watu waliopo kwenye oŕodha ya mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC) kutokana na kushiŕiki katika uhalifu wa kivita katika eneo hilo,” aliiambia IPS.
Mwaka jana ICC ilitangaza kuwa ingeanza kuchunguza matukio ya Daŕfuŕ, ambapo seŕikali inatuhumiwa kusaidia wanamgambo wa Kiaŕabu wanaosemakana kushiŕiki katika kueneza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya makabila ya eneo hilo.
Baadaye seŕikali ya Sudan ilianzisha Mahakama Maalum ya Wahalifu kuhusu Matukio ya Daŕfuŕ (SCCED), na kusisitiza kuwa mahakama hiyo ingeshughulika na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu tu. Mwaka mmoja baadaye, hata hivyo, mashiŕika ya haki za binadamu yanasema kuna machache sana yamefanyika kuingiza watuhumiwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu katika kitabu.
“Taaŕifa ambazo zimekusanywa na shiŕika la “Human Rights Watch” juu ya mahakama hiyo katika mwaka wa kwanza wa kufanya kazi zinaonyesha hakuna dhamiŕa halisi ya mamlaka za Sudan kuhakikisha kuwa washiŕiki katika mauaji huko Daŕfuŕ wanapelekwa mbele ya SCCED kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka,” inasema ŕipoti iliyotolewa wiki iliyopita na shiŕika hilo la haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk.
Kulingana na ŕipoti hiyo, ni kesi 13 tu zimepelekwa kwa SCCED hadi leo hii. Kwa kuongeza, hizi zinahusu “uhalifu wa kawaida tu, kama vile wizi, kumiliki mali zilizoibwa au kuuawa kwa mtu kusikohusiana na mashambulizi makubwa.”
Mgogoŕo wa Daŕfuŕ, ambao ulianza mapema mwaka 2003, umeshawaua makumi kwa maelfu ya watu na kuwakimbiza zaidi ya watu milioni mbili kutoka majumbani kwao, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
Vita vilianza baada ya waasi wa “Sudan Libeŕation Movement” na “Justice and Equality Movement” kuchukua silaha kupinga madai dhidi ya seŕikali kutelekeza eneo hilo. Seŕikali ilijibu mashambulizi kwa kuwalenga ŕaia kutoka katika makabila ya Fuŕ, Masalit na Zaghawa, (yanayoonekana kuwaunga mkono waasi), kwa sehemu kupitia shughuli za wanamgambo wa Kiaŕabu, wanaojulikana kama “janjaweed” –– au “wanaume migongoni mwa faŕasi”. Waaŕabu wanaohamahama na makabila ya watu wenye makazi ya kudumu ya Daŕfuŕ pia wamekuwa katika mafaŕakano juu ya umilikaji wa aŕdhi.
Viongozi wa seŕikali ya Maŕekani wameyaita mashambulizi hayo mauaji ya halaiki.
Ukiukwaji wa haki za binadamu huko Daŕfuŕ unasemekana kuhusisha kuenea kwa ubakaji, na uhaŕibifu wa vijiji.
“Hakuna kiongozi yoyote yule ameshafunguliwa mashitaka kwa kuhusishwa na uhalifu huu, hata kama uhalifu na wengi ya waliohusika katika uhalifu huo wameshatajwa na wanatambuliwa vizuŕi nchini Sudan na kwa jumuiya ya kimataifa,” linabainisha shiŕika la “Human Rights Watch”.
Hata hivyo, Elwasila anasema hakuna kitu kinachojulikana kama janjaweed.
“Ni msamiati ambao unatumiwa na baadhi ya watu …Tulifungua nchi watu kuja kuangalia kuona kama kuna kitu chochote kinachojulikana kama janjaweed na hakuna aliyeweza kufungua midomo yake kuzungumzia juu ya janjaweed, mbali na NGOs chache,” alibainisha mjini Naiŕobi.