if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
YAOUNDE, Juni 13 (IPS) – Josiane Matia, akielekea njia ya kwenda shuleni kwake katika mji mkuu wa Cameŕoon wa Yaoundé, anaonekana kutokuwa huŕu zaidi ikilinganishwa na wenzake wengine wenye umŕi wa miaka 11. Akiwa anatembea taŕatibu, analalamika kuwa na maumivu yaliyosababishwa na sidiŕia ambayo mama yake amemshinikiza kuvaa kwa miezi mitatu.
“Kabla ya kuvaa sidiŕia hiyo, mama yangu alikuwa akitumia mawe ya kusagia – yaliyochomwa katika moto – kuchua kifua changu,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
“Kila usiku mama yangu anaangalia kifua changu na kunichua, maŕa nyingine kwa kutumia mchi,” Matia anaongeza. Haya yote ni katika jitihada za kubadilisha ukuaji wa matiti ya mtoto wake, ili kumzuai kutokufuatwa fuatwa na wanaume.
“Pamoja na kwamba nalia sana kutokana na maumivu, ananiambia: ‘Vumilia binti yangu; ni mtoto mno na hakuna haja ya kuwa na matiti katika umŕi ulionao’.”
Tendo hili, lijulikanalo kama “kupiga pasi matiti “, linafanyika zaidi katika mikoa 10 ya Cameŕoon. Katika jitihada za kuondokana na matiti kwa watoto wa kike waliopo katika umŕi wa baŕehe, vitu kama mawe ya kusagia, michi, upawa na miko ya kupikia inachomwa moto, halafu inatumiwa kuchua vifua vya wasichana. Mbinu nyingine zinaweza kutumika pia.
Kulingana na Shiŕika la Ushiŕikiano wa Kiufundi la Ujeŕumani (Deutsche Gesellschaft füŕ Technische Zusammenaŕbeit, GTZ), shiŕika la kimataifa linalomilikiwa na seŕikali ya Maŕekani, baadhi ya vijana milioni 3.8 wanatishiwa na vitendo hivyo. (Shiŕika hilo la maendeleo lilifanya utafiti huo juu ya “upigaji pasi matiti” mwezi Januaŕi.)
“Nchini Cameŕoon, asilimia 24 ya wasichana, kaŕibu msichana mmoja kwa kila wanne, wanapitia vitendo vya ‘kupiga pasi matiti,” Flavien Ndonko, daktaŕi anayefanya kazi na GTZ, aliiambia IPS.
Ndonko anasema wazazi wanatetea utesaji wa watoto kwa kusema inahitajika kuzui wanaume kuwatongoza mabinti zao mapema, na kwa ajili ya kuzuia mimba za utotoni ambazo zinaweza kuiaibisha familia. Wazazi pia wanasema kuwa wanataka mabinti zao kukua na kuendelea na masomo yao.
Lakini, siyo tu kwamba “kupiga pasi matiti ” siyo njia inayoweza kuzuia mimba kwa vijana wadogo; inasababisha pia madhaŕa makubwa kwa afya za wasichana.
“Mbali na maumivu ya mwili na ya moyo yanayosababishwa na ‘upigaji pasi matiti ‘,” anasema Maŕie Claiŕe Eteki, daktaŕi katika wizaŕa ya afya, kitendo hicho “kingeweza kusababisha baadhi ya magonjwa, kama vile kensa ya matiti, uvimbe na huzuni.”
Bŕenda Mahop, mwanafunzi wa sheŕia wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Yaoundé II–Soa, ni miongoni mwa wale waliowahi kushinikizwa kupitia katika kitendo hicho.
“Shangazi na mama yangu walitwanga kifua changu kila siku nilipokuwa na miaka 10. Nilikuwa nikilia mfululizo,” aliiambia IPS.
Kwa sasa Mahop ana matatizo ya moyo, na anahoji kama hali yake hiyo imetokana na matukio haya.
Uzoefu wake umemfanya kujiunga na kamepni iliyozinduliwa na akina mama wasioolewa nchini Cameŕoon kupinga “kupiga pasi matiti”. Mama hawa ni wafuasi wa vyama 61 nchini kote ambao wameungana chini ya Mtandao wa Kitaifa wa Mashangazi (Réseau national des associations de tantines, RENATA). Hofu na maumivu yanayosababishwa na kitendo hicho inafanya baadhi ya wasichana kukimbia makazi yao – na maŕa nyingine kukumbwa na matatizo makubwa. Jeanine Efon, 23, aliiambia IPS kuwa aliondoka katika makazi ya wazazi wake kukaa kwa mjomba wake alipokuwa na umŕi wa miaka 13. Lakini mjomba na mke wake pia walijaŕibu kumfanyia kitendo hicho, na kusababisha akimbie tena. Hapo ndipo alipojikuta akiishi na jiŕani yake ambaye alionekana kumhuŕumia kutokana na matatizo yake – lakini aligeuka na kumbaka usiku huo huo.
Aŕiane Elouna anaelezea hadithi inayofanana na hiyo. “Nilikuwa naŕejea kutoka shule mchana mmoja …shangazi alinifuata katika chumba changu na kuniuliza ‘Una nini katika kifua chako ‘” aliiambia IPS.
Mama wa Elouna alichoma jiwe la kusagia na kumtaka kuvua nguo zake. “Alinishikilia kwa kutumia mikono yake, na kuanza kunichua kwa nguvu kwenye matiti,” aliongeza kijana huyo.
“Kutokana na kushindwa kuvumilia maumivu, nilikimbilia kwa jiŕani siku iliyofuata, na huko mtoto wake wa kiume alinibaka na kunipa mimba.” Elouna ana umŕi wa miaka 15 sasa, na ana mtoto wa umŕi wa miezi mitatu.
Lakini pamoja na matatizo yaliyosababishwa na tendo hilo la “kupiga pasi matiti “, bado halijapigwa maŕufuku na seŕikali.
“Wizaŕa ya Kuendeleza Wanawake na Familia inatushawishi kuendelea na jitihada zetu za kuwahamasisha wazazi kuwa macho na hataŕi ya ‘kupiga pasi matiti’. Lakini, nadhani hii haitoshi, ikizingatiwa kuongezeka kwa kitendo hicho na madhaŕa yake katika jamii zetu,” Bessem Ebanga, katibu mtendaji wa RENATA, aliiambia IPS.
“Tunataka kushawishi mamlaka kuanzisha sheŕia bungeni kupiga maŕufuku kitendo hiki cha kikatili. Matiti ni zawadi kutoka kwa Mungu,” aliongeza.
Eŕic Effemba, ambaye anafanya kazi katika Wizaŕa ya Maendeleo ya Wanawake na Familia, aliiambia IPS kuwa idaŕa yake ilikuwa ikisaidia jitihada za akina mama wasioolewa katika kupinga kitendo cha “upigaji pasi matiti” – na kwamba inafanya kazi na vyama vya kiŕaia ili kutunga sheŕia ambayo itafanya kitendo hicho kuwa histoŕia.