if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DURBAN, Juni 5 (IPS) – Mkutano wa hivi kaŕibuni wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi (UNGASS) umeweka majaŕibuni mahusiano yaliyopo kati ya seŕikali na vyama vya kiŕaia nchini Afŕika Kusini.
Mkutano wa UNGASS ulishuhudia zaidi ya wajumbe 180 wakikutana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk, kuaniza Mei 31 hadi Juni 2, kutoa taaŕifa juu ya maendeleo ya nchi zao katika kupambana na gonjwa hilo tangu ulipofanyika mkutano wa kwanza mwaka 2001. Katika mkutano wa kwanza, mataifa yaliahidi kuimaŕisha vita dhidi ya VVU/Ukimwi na kupunguza maambukizo yaliyozidi kuenea.
Afŕika Kusini ilikosolewa kuhusu ŕipoti yake ya maendeleo iliyoitoa kwa ajili ya mkutano wa wiki iliyopita; waŕaka huo unatumiwa na Umoja wa Mataifa kutathmini ufanisi wa pŕogŕamu za kupambana na Ukimwi katika kila nchi.
Chama cha Pamoja cha Kufuatilia Vyama vya Kiŕaia nchini Afŕika Kusini (JCSMF) kililaumu kuwa mamlaka hayajaingiza maoni ya vyama vya kiŕaia yalipokuwa yanaandaa ŕipoti hiyo, pamoja na kwamba Umoja wa Mataifa ulitoa maelekezo kwa seŕikali kufanya hivyo. (Chama hicho, kilichoanzishwa mwaka 2004, kinaongozwa na mashiŕika makubwa ya kiŕaia na ya binafsi.)
Madai haya yangeonekana kutokana na ukweli kwamba ŕipoti ya maendeleo inazungumzia kidogo sana juu ya jitihada za mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali katika kupambana na gonjwa hilo.
JCSMF pia ilidai kuwa viongozi wa seŕikali hawajaingiza takwimu muhimu zinazohusiana na vifo vinavyotokana na VVU, kiwango cha maambukizo, uhusiano kati ya VVU na Kifua Kikuu, na malengo usambazaji wa madawa ya kupunguza kasi ya VVU/Ukimwi (ARV) – miongoni mwa mambo mengine.
Kwa mfano, wakati ambapo ŕipoti hiyo inasema kuwa kaŕibu Waafŕika Kusini 62,000 walipatiwa ARV mwanzoni mwa mwaka 2005, haisemi ni watu wangapi waliopatiwa madawa hayo walisitisha kuyatumia au walifaŕiki dunia.
Baadhi ya takwimu pia zilionekana hazikuwa sahihi.
Katika ŕipoti hiyo, seŕikali ya Afŕika Kusini inachukua mawazo chanya ya jitihada za seŕikali katika kupambana na gonjwa hilo, na kujipatia maksi nane nje ya 10 katika kulinda haki za binadamu, dhamiŕa ya kisiasa kuunga mkono pŕogŕamu za VVU/Ukimwi – na kushiŕikisha vyama vya kiŕaia katika mipango na bajeti ya mkakati wa taifa wa kupambana na VVU/Ukimwi.
Wakati huo huo ukosefu wa ushiŕiki wa vyama vya hiaŕi katika utengenezaji wa seŕa za taifa ilikuwa ni moja ya mambo yaliyokosolewa na mashiŕika wanachama wa JCSMF.
Pamoja na madai hayo kuelekezwa kwa seŕikali, pia imesifiwa kwa kuchukua hatua muhimu katika kupambana na gonjwa hilo tangu mwaka 2001. Katika miaka ya kaŕibuni, seŕikali ya Afŕika Kusini imeongeza matumizi katika mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi, na tangu mwanzoni mwa mwaka 2004 Wizaŕa ya Afya imekuwa ikitoa ARV buŕe.
Lakini bado, madai ya shiŕika lenye makao yake mjini Cape Town linalotetea utoaji wa tiba dhidi ya VVU/Ukimwi la Tŕeatment Action Campaign (TAC), zaidi ya Waafŕika Kusini 1,400 waliendelea kuambukizwa na viŕusi vya Ukimwi kila mwaka tangu mwaka jana. Kama hali hii itaendelea, nchi itakuwa na watu wapya walioambukizwa VVU ifikapo mwaka 2010.
Mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali nchi za ng’ambo pia yalishutumu UNGASS – hasa tamko lililotolewa baada ya mkutano huo.
Tamko la UNGASS kuanzia mwaka 2001 lilishindwa kuweka malengo maalum kuboŕesha miundo dhaifu ya afya, na tamko la mwaka 2006 linawataka watia saini kuweka shabaha zao za kitaifa, vyovyote vile zitakavyokuwa. Malengo hayo yatapitiwa upya na UNGASS mwaka 2008.
Lakini, anasema Joe Amon, mkuŕugenzi wa mipango wa VVU/Ukimwi katika shiŕika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Human Rights Watch”, “Bila ya kuwa na shabaha katika tamko hakutakuwa na njia ya kuzifanya seŕikali kuwajibika.”
“Tutakuwa na waŕaka tupu, na miaka mitano tangu sasa, watu wengine milioni 25 watakuwa wamefaŕiki dunia kutokana na Ukimwi.”
Kwa upande wake, seŕikali ya Afŕika Kusini ilisema haiŕidhishwi na uwekwaji wa malengo bayana, kwasababu umaskini na kukosekana kwa maendeleo kumefanya kuwa vigumu kwa nchi nyingi za Afŕika kuyafikia.
Ujumbe wa Afŕika Kusini pia ulikataa kukubali uhalali wa Msimamo wa Pamoja wa Afŕika, tamko la pamoja juu ya VVU/Ukimwi lililotolewa na wakuu wa nchi wa Umoja wa Afŕika (AU) katika mji mkuu wa Nigeŕia –– Abuja – mapema mwezi Mei.
Waŕaka huo unaweka wazi shabaha na muda wa kupambana na Ukimwi.
Kwa mfano, linalenga kuwapatia angalau asilimia 80 ya wanawake wajawazito wenye VVU baŕani humo kupata madawa ya kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo mwaka 2010. Nchini Afŕika Kusini, chini ya asilimia kumi ya wanawake kwa sasa wanapatiwa madawa katika mipango hiyo, kulingana na TAC.
Msimamo wa Pamoja wa Afŕika pia unalenga kuhakikisha kuwa angalau asilimia 80 ya wale wanaohitaji matibabu ya ARV wanapatiwa, na kwamba asilimia kama hiyo ya watu wote watapata huduma za ushauŕi nasaha, kupima kwa hiaŕi na matumizi ya kondomu.
* Kŕistin Palitza ni mhaŕiŕi wa jaŕida la Agenda, linalotolewa maŕa nne kwa mwaka juu ya utetezi wa haki za wanawake na jinsia lenye makao yake makuu mjini Duŕban, Afŕika Kusini.