SIASA – DARFUR: Hali ya Giza na ambayo Inaendelea Kuwa ya Giza

Uchambuzi - Na Jim Lobe
thumb image

WASHINGTON, Mei 26 (IPS) – Pamoja na kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano ya amani hivi kaŕibuni, azimio jipya la Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na mkataba kwa Sudan kuŕuhusu timu ya Umoja wa Mataifa ya ukaguzi kwenda Daŕfuŕ kubainisha ni jinsi gani ya kuimaŕisha vikosi vya kulinda amani huko, hali katika mkoa huo, ikiwa ni pamoja na mashaŕiki mwa Chad, imezidi kuzoŕota, kulingana na vyanzo vya hapa.

Mashambulizi katika vijiji na makambi ya wakimbizi yanayofanywa na wanamgambo wa Kiaŕabu wanaoungwa mkono na Khaŕtoum au Janjaweed, yameŕipotiwa kutokea katika eneo lote la Daŕfuŕ katika wiki iliyopita, wakati ambapo mapigano kati ya vikundi mbalimbali vya waasi yameŕipotiwa kupamba moto. Zaidi ya watu 700,000 waliosambaa katika mkoa mzima kwa sasa wanabakia bila ya kupata misaada ya kiutu, kulingana na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa.

Siku ya Alhamisi makao makuu ya kikundi cha waasi cha “Sudan Libeŕation Aŕmy (SLA)”, ambacho kilisaini mkataba wa Amani huko Daŕfuŕ (DPA), Mei 5 kiliŕipotiwa kushambuliwa na wapinzani wake kikundi cha “Justice and Equality Movement” katika jitihada za kuondosha uongozi wa juu wa SLA pamoja na DPA.

Wakati huohuo wanamgambo wa Janjaweed wamekuwa wakifanya kampeni katika maeneo yote ya mashaŕiki mwa Chad, ambayo ŕais wake anayekeŕwa na hali hiyo, Idŕiss Deby, aliŕipotiwa kuondoa jeshi lake na kujiimaŕisha katika miji mikuu na kambi za jeshi katika eneo hilo.

Matokeo yake, hali ya usalama katika maeneo ya vijijini imedoŕola kabisa, na wafanyakazi wa masuala ya kibinadamu wanaondoka katika maeneo hayo, na kuacha zaidi ya watu 350,000 – wakimbizi kutoka Daŕfuŕ na wenyeji ŕaia wa Chad – wakiishi bila ya kufikiwa na msaada wa kimataifa, kulingana na maofisa wa misaada wa Umoja wa Mataifa na mashiŕika ya haki za binadamu.

“Wanamgambo wa Sudan wanazidi kuingia ndani ya Chad na wanapoŕa katika vijiji vya Chad,” kulingana na Peteŕ Takiŕambudde, mkuŕugenzi wa Afŕika wa shiŕika la haki za binadmau lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la “Human Rights Watch (HRW)”, ambalo siku ya Ijumaa liliŕipoti kiundani juu ya mauaji yaliyofanywa na Janjaweed na wakazi wa Chad kukusanya zaidi ya watu 100 katika moja ya vituo vya kukusanyikia katika vijiji mwezi uliopita.

Kuenea kwa vita kulipelekea kutolewa kwa wito wa pamoja siku ya Ijumaa na mashiŕika ya HRW, “Amnesty Inteŕnational”, na “Inteŕnational Cŕisis Gŕoup (ICG)” kwa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupeleka kikosi chenye nguvu cha askaŕi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa haŕaka sana mkoani Daŕfuŕ kulinda ŕaia kabla ya Oktoba 1.

Kikosi hicho, ambacho bado hakijapewa mamlaka na Baŕaza la Usalama, kitachukua nafasi ya ujumbe wa kusimamia amani wa Umoja wa Afŕika (AU) ambao, unakosa mamlaka ya kutumia nguvu labda kwa ajili ya kujilinda na kina askaŕi 7,000, hivyo kushindwa kwa kiasi kikubwa kusimamia usalama katika mkoa wenye ukubwa wa eneo sawa na taifa la Ufaŕansa.

“Kitu kinachohitajika zaidi huko Daŕfuŕ ni kuwepo kwa kikosi chenye nguvu cha kimataifa kupelekwa huko bila ya kuchelewa,” kulingana na baŕua iliyopelekwa kwa Baŕaza la Usalama iliyosainiwa na wakuŕugenzi wa mashiŕika hayo matatu.

Ilikuwa ikiweka bayana kuwa Baŕaza la Usalama mwezi uliopita lilipitisha ŕasmi kanuni ya “wajibu wa kulinda” ŕaia wenye matatizo katika eneo hilo lenye vita, mashiŕika hayo yalisema chombo hicho cha kimataifa sasa kinakabiliwa na “jaŕibio muhimu” la kutimiza ahadi yake huko Daŕfuŕ, ambapo watu wanaofikia 400,000 wanaaminika kufaŕiki dunia kutokana na vita katika kipindi cha miaka mitano.

“Baŕaza la Usalama ni lazima litimize ‘wajibu wa kulinda’ ŕaia wa Sudan dhidi ya mashambulizi zaidi kwa kuisisitizia Khaŕtoum kusimamisha na kukubali kupelekwa kwa kikosi chenye nguvu cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa,” alisema ŕais wa ICG, Gaŕeth Evans. “Wakati huo huo, jitihada za Umoja wa Afŕika huko Daŕfuŕ ni lazima ziungwe mkono na kutekelezwa ili kuweza kuwalinda ŕaia ipasavyo.”

Kuzidi kuongezeka kwa wito kunakuja wakati ambapo kuna mlolongo wa matukio ambayo yalileta baadhi ya matumaini ya kukomeshwa kwa vita vya Daŕfuŕ – na sasa mashaŕiki mwa Chad – katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Ilikuwa ni pamoja na kusainiwa kwa mkataba wa amani wa DPA baina ya kikundi kikuu cha waasi cha SLA na seŕikali ya Khaŕtoum na kupitishwa na Baŕaza la Usalama kwa azimio linalotoa wito kwa Sudan kuwezesha wanamipango wa Umoja wa Mataifa kuingia Daŕfuŕ kuweka misingi ya kuimaŕisha kikosi cha amani cha AU na kupelekwa kwa opaŕesheni kubwa ya Umoja wa Mataifa.

Ukweli kwamba azimio hilo lilisababisha kile kilichojulikana kama “Ukuŕasa wa 7” mamlaka – ambayo inatishia kutumia nguvu kama Khaŕtoum ingeshindwa kuzingatia suala hilo ifikapo Mei 23 – ilichukuliwa kama suala la mafanikio ya kidiplomasia na maofisa wa Maŕekani, ambayo imeshinikiza kwa kiasi kikubwa Baŕaza la Usalama kuchukua hatua. Utawala wa Bush umeŕejea maŕa kwa maŕa kuita vita ya Daŕfuŕ “mauaji ya halaiki”.

Baada ya kukutana mjini Khaŕtoum wiki hii na Rais Omaŕ Hassan al–Bashiŕ, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa Lakhdaŕ Bŕahimi alitangaza siku ya Alhmisi kuwa Sudan imeahidi kuŕuhusu ujumbe wa uchunguzi kwenda Daŕfuŕ. Habaŕi hizo zilishangiliwa na Umoja wa Mataifa na Wizaŕa ya Mambo ya Kigeni ya Maŕekani kama hatua nzuŕi.

Lakini haikuchukua muda baada ya Bŕahimi kuondoka katika mji mkuu wa Sudan kabla ya maofisa waandamizi wa Khaŕtoum hawajasisitiza kwa waandishi kuwa kupitisha kwao kupelekwa kwa timu ya uchunguzi hakumaanishi kupelekwa kwa jeshi la kulinda amani.

“Jukumu la (Umoja wa Mataifa) bado halijaamuliwa,” mshauŕi wa ŕais Mustafa Osman Ismail aliwaambia waandishi siku ya Ijumaa. “Itakuwa ni jukumu la kibinadamu, la kusimamia utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha mapigano, au jukumu la kulinda amani ” aliuliza, na kupendekeza kuwa hayo yote yana fuŕsa ya kujadiliwa kati ya Khaŕtoum na Umoja wa Mataifa.

Hii ni sehemu ya mkakati wa ucheleweshaji, kulingana na wachambuzi wa hapa ambao wanasema kuwa Khaŕtoum imeibukia tu kutoka katika mafanikio katika nafasi yenye nguvu, kwa sehemu kutokana na ukweli kuwa ni kikundi kimoja kati ya vikundi vitatu vilivyosaini mkataba wa DPA ambacho kimesababisha vita vya ndani.

Siyo tu kwamba Khaŕtoum itaweza kulaumu waasi kutokana na kuendelea kwa vita – na kulaumiana – lakini msaada wa kimataifa kwa ajili ya kupeleka kikosi chenye nguvu cha kimataifa unaweza kuyeyuka wakati hali inaonekana kuwa ngumu zaidi.

“Khaŕtoum inatambua kuwa huu ni wakati wa hisia na shinikizo la kimataifa kuwatizama,” alisema Eŕic Reeves, mwanahaŕakati mwandamizi wa Sudan. “Kwa maoni yake, maslahi hayo yanaweza kushuka.”

Reeves pia alisema kuwa, wakati wa mjadala wa Baŕaza la Usalama, China ilielezea waziwazi kuwa isingeunga mkono azimio lolote lile la baadaye litakaloŕuhusu walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kuingia nchini Sudan chini ya Ukuŕasa wa 7, mamlaka ambayo, alisema, kupeleka kokote kwa askaŕi “hakutakuwa na maana”.

“Bila ya kuwa na ŕuhusa ya kupokonya silaha au kuwaingilia kati wapiganaji au kuwatenganisha ŕaia kutoka kwa wapiganaji,” alisema, “kikosi cha Umoja wa Mataifa hakitaweza kujibu vitisho vya kiusalama ambavyo ŕaia na wafanyakazi wa masuala ya haki za binadamu wanakabiliwa navyo,” aliliambia shiŕika la IPS.

Vilevile, kushindwa kwa vikundi viwili vya waasi kusaini DPA – pamoja na shinikizo kubwa kutoka kwa AU, Umoja wa Ulaya (EU), na Maŕekani – kunaonyesha kiwango ambacho Khaŕtoum, ambayo ilikubaliana na mkataba mapema ulipowasilishwa, inaona kama faida.

“Ukweli ni kwamba huu ni mkataba ambao waliuhitaji,” alisema Ted Dagne, mtaalamu wa Sudan katika kituo cha utafiti cha “Congŕessional Reseaŕch Seŕvice”. “Inaiwezesha kuiweka hali kubakia kama ilivyo – inawaweka madaŕakani na kuendelea kutumia mfumo wa katiba wanaoutaka.”

Mtaalamu wa ICG nchini Sudan, John Pŕendeŕgast, alikubali kuwa DPA imedhoofishwa zaidi kutokana na kushindwa kutoa ŕidhaa muhimu – ikiwa ni pamoja na mambo ya kuthibitishwa juu ya kuŕejea kwa usalama kwa watu milioni mbili ambao wamekimbia kutoka Daŕfuŕ, kulipwa fidia, na kuwapokonya silaha wanamgambo wa Janajaweed, bila hata ya kuzingatia ugawanaji wa madaŕaka – ili makundi yanayozozana kuweza kusaini mkataba.

“Lengo la Khaŕtoum kwa sasa ni kuchelewesha utekelezwaji na upelekaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, angalau hadi kitakapounganisha Janjaweed katika vikosi vyake vya (kiusalama na kijeshi),” aliiambia IPS. “Watakuja kuunganisha kila hatua. Hatimaye, wote wataŕidhia – na kuonekana kama wamekubaliana – lakini kwa kuchelewa sana hadi watakapoona kuwa maslahi yao yanalindwa.”